Waziri Luhaga Mpina Aagiza Kuvunjwa Kwa Mkataba Na Wawekezaji Watatu

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
mpina.JPG

Serikali kupitia waziri Luhaga Mpina inayarajia kufuta mikataba yote iliyoingiwa kati ya NARCO na wawekezaji ambao kwa kiasi kikubwa walipelekea kuua utendaji na ufanisi wa Ranchi za Taifa.

Uhujumu huu tuliupigia kelele sana hata humu JF ..sasa chini ya Rais Magufuli tunaenda kushuhudia yale majipu yaliyoshindikana yakienda kutumbuliwa.

Wito wangu ni mmoja tu..kwamba tusisikie mtu kujificha nyuma ya kivuli cha Siasa za upinzani ajidai ameonewa eti kisa yeye ni mpunzani.

SOURCE:ITV HABARI

=========

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ameagiza Mtendaji Mkuu wa Ranchi za Mifugo za Taifa, Profesa Philemoni Wambura kuvunja mikataba ya wawekezaji wa vitalu vyenye jumla ya hekta 68,238 kwenye ranchi ya Mkata na Dakawa ndani ya mwezi mmoja baada kushindwa kuviendeleza vitalu vya ranchi na kushindwa kulipia kwa muda mrefu.Mpina ameyasema hayo jana wakati alipotembelea katika ranchi ya Mkata na Dakawa kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika katika ranchi hizo.

Amezitaja kampuni za wawekezaji ambazo zilizomilikishwa vitalu zinatakiwa kuvunja mkataba kwa kushindwa kuendeleza upande wa ranchi ya Mkata katika Wilaya ya Kilosa kuwa ni pamoja na Kadolo Farm Company Ltd kitalu namba 418 yenye hekta 4005,Bagamoyo Farm kitalu namba 419 yenye hekta 3672.96, A to Z Animal Feeds Company Ltd kitalu namba 420 yenye hekta 3692.97 na Ereto Livestock Keepers kitalu namba 422 yenye hekta 4020.54.

Katika Wilaya ya Mvomero kampuni zilizoshindwa kuendeleza vitalu ni pamoja na kampuni ya Overland kitalu namba 415 yenye hekta19446.28, Katenda yenye hekta 2500, Mollel yenye hekta 2500 na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa (Mtibwa Sugar) chenye hekta 20000 walizomilikishwa toka mwaka 1999 na kushindwa kukiendeleza na kukilipia kwa miaka 18.

Mpina amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilosa kumaliza mara moja migogoro inayoendelea baina ya wakulima na wafugaji. Aidha Waziri Mpina amemtaka Diwani wa kata yaTwatwatwa, Katibu Tawala wa Halimashauri ya Wilaya ya Kilosa pamoja na jamii ya wafugaji kumaliza migogoro inayowasumbua kwa muda mrefu kwa njia ya mazungumzo kabla ya kukimbilia muhimili wa mahakama bila sababu yoyote.

Mpina amesema kama vyombo vya Serikali vingetumika vizuri kuanzia ngazi ya kijiji kungepunguza migogoro ya wakulima na wafugaji katika wilaya hiyo. Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa Wilaya zinaongoza kwa kuwa na migogoro mingi baina ya wakulima na wafugaji hapa nchini.

Kwa upande mwingine, Waziri Mpina amezitaka Halimashauri zote nchini kutotunga sheria kandamizi dhidi ya wafugaji. Akitolea mfano, wa sheria ndogo ya Halimashauri ya Mvomero ya kutoza faini ya shilingi 25, 000/=kwa kila mfugo kuingia katika Wilaya hiyo bila kufuata taratibu badala ya shilingi elfu kumi iliyoelekezwa katika Sheria ya Magonjwa ya Wanyama namba 17 ya Mwaka 2003.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) Magembe Makoye amesema upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya wafugaji kutasaidia kuondoa migogoro baina ya pande hizo na kuendelezwa kwa ranchi hizo za taifa kutawasaidia wafugaji kupata shamba darasa litakalo wasaidia kufuga kwa kisasa na kupata mbegu bora za mifugo.

Chanzo: Michuzi
 
Serikali kupitia waziri Luhaga Mpina inayarajia kufuta mikataba yote iliyoingiwa kati ya NARCO na wawekezaji ambao kwa kiasi kikubwa walipelekea kuua utendaji na ufanisi wa Ranchi za Taifa.

Uhujumu huu tuliupigia kelele sana hata humu JF ..sasa chini ya Rais Magufuli tunaenda kushuhudia yale majipu yaliyoshindikana yakienda kutumbuliwa.

Wito wangu ni mmoja tu..kwamba tusisikie mtu kujificha nyuma ya kivuli cha Siasa za upinzani ajidai ameonewa eti kisa yeye ni mpunzani.

SOURCE:ITV HABARI
Amini usiamini kuna mtu anawekwa kati.Mzeri ranch au Mkata ranch,stay tuned!!
 
Amini usiamini kuna mtu anawekwa kati.Mzeri ranch au Mkata ranch,stay tuned!!
Mzeri ranch itoe hapo,, jamaa kule yuko vizuri mno maana kaweka ng'ombe wa uhakika!! Na bado anaendelea kuwekeza kule kwa kuboresha malisho!!!
 
Mzeri ranch itoe hapo,, jamaa kule yuko vizuri mno maana kaweka ng'ombe wa uhakika!! Na bado anaendelea kuwekeza kule kwa kuboresha malisho!!!

hata mkata ipo vizuri. japo kunauwezekano timing yao ni huko.
by the way wawekezaji ndio waliua ranchi au siasa za MACCM ndio ziliua?

pia nikumbukavyo ni kuwa hizi Ranchi zilikuwa ziuzwe ila Mzee wa Mzeri alikataa zisiuzwe akiwa waziri mkuu.

je lini watarudisha nyumba za serekali ?
 
Serikali kupitia waziri Luhaga Mpina inayarajia kufuta mikataba yote iliyoingiwa kati ya NARCO na wawekezaji ambao kwa kiasi kikubwa walipelekea kuua utendaji na ufanisi wa Ranchi za Taifa.

Uhujumu huu tuliupigia kelele sana hata humu JF ..sasa chini ya Rais Magufuli tunaenda kushuhudia yale majipu yaliyoshindikana yakienda kutumbuliwa.

Wito wangu ni mmoja tu..kwamba tusisikie mtu kujificha nyuma ya kivuli cha Siasa za upinzani ajidai ameonewa eti kisa yeye ni mpunzani.

SOURCE:ITV HABARI
Ya zimbambwe,yule askofu wa Zanzibar ni nabii,alisema wazi kabisa magufuli na mugabe ni sawa
 
Nchi ya visasi
Maaskofu na makanisa mwaka huu wataomba kweli kweli
 
Wito Wangu Kwa Vijana Wanaofanya Siasa, Tafuteni Kuwa na Kazi Za Kipato Halali, Usifanye Siasa Una Njaa
Wengi wanafanya siasa kwasababu ya njaa kuna siku nilihudhuria mkutano Wa siasa nikagundua wengi ambao ni viongozi wanapata uongozi kwa kujitolea lakini Gorofañi hakuna kitu
 
Awamu hii Laigwanani ana kazi.Hadi 2020 hatakuwa na ya kufadhili kampeni ya kumpinga mwenye nyumba.
 
Mzeri ranch itoe hapo,, jamaa kule yuko vizuri mno maana kaweka ng'ombe wa uhakika!! Na bado anaendelea kuwekeza kule kwa kuboresha malisho!!!
Mkubwa ranchi ya mzeri iko wapi? Nimepotea njia
 
Back
Top Bottom