Waziri Lugola kathibitisha kauli ya Lissu kuwa Tanzania ni mara mia kumkashifu au kumkejeli Mungu kuliko Rais Magufuli

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,551
2,000
Kwa kauli aliyoitoa leo lugola naona ni ya kishamba na kujipendekeza zaidi kwa rais kuliko watanzania. Hii ni nidhamu ya uwoga wa kupoteza tumbo (uwaziri) sio kuwa na uchungu na wananchi (uzalendo)

Nashindwa kuelewa ivi kumkosoa rais sio haki ya raia? Yaani waliomwajiri hawaruhusiwi kusema mambo wasiyo yataka ila ni kusikiliza aliyeajiriwa anachokitaka.

Ivi kangi lugola anaweza kuyataja baadhi ya matusi ambayo alishatukanwa rais? Na kati walimtukana ni yupi alishawai kufungwa?

Nachokiona nchi hii ukimkosoa rais ambaye ni zaidi ya malaika mkuu unaitwa uchochezi then yanageuka kuwa matusi, kejeli, na uasi.

Mara ngapi huyo malaika mkuu anatukana raia? Yeye ni ruksa?

Mara ngapi anakosoa raia kwake yeye ni ruksa?

Nathibitisha kauli ya Lissu ni heri ukutwe unamkosoa Mungu kuliko kukutwa unamkosoa magufuli
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom