Waziri Lugola: Halmashauri ya Jiji la Dar itafute njia mbadala ya kusimamia usafi badala ya Mgambo wa RC Makonda

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Wizara wa Mambo ya Ndani ya nchi imekemea kushamiri kwa matukio ya watu kujichukulia sheria mkononi ikiwemo kupiga, kujeruhi na kuuawa.

Waziri Lugola amesema hayo jana Jumapili Septemba 2, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.

Ametaja matukio ya walimu kuwaadhibu, kujeruhi na kusababisha vifo vya wanafunzi wao pamoja na mgambo wa Jiji la Dar es Salaam kuwajeruhi wananchi wanaposimamia suala la usafi kuwa miongoni mwa matukio yasiyokubalika mbele ya macho ya sheria.

"Suala la mgambo waliowekwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwapiga na kuwajeruhi wananchi limewaondolea sifa ya kuendelea kuwatumikia wananchi, ni vema halmashauri ikatafuta njia mbadala ya kushughulikia suala hilo la usafi na kudhibiti matukio hayo," amesema Waziri Lugola

Ameagiza halmashauri nchini kuanzisha kitengo cha huduma ya askari polisi chini ya sheria sura ya 322 ili kupunguza matukio ya mgambo ambao baadhi hawajui namna ya kusimamia utekelezaji wa sheria kutumika na hatimaye kukiuka sheria.

Akizungumzia adhabu kwa wanafunzi, Waziri Lugola amewataka walimu kutoa adhabu kwa mjibu wa sheria kwa lengo la kuwarekebisha wanafunzi na si kuwakomoa.

Ameuhakikishia umma kuwa Serikali kupitia mamlaka husika itachukua hatua dhidi ya wote waliohusika katika matukio yote ya kujichukulia sheria mkononi.

"Mahakama pekee ndicho chombo cha kutoa adhabu kwa mujibu wa Katiba na sheria. Tutawashtaki wote waliohusika bila kujali vyeo, majina wala umaarufu wao kwa sababu hakuna aliye juu ya sheria," amesema Lugola.

Chanzo; Mwananchi
 
Watu wamepata mafunzo ya awali ya kijeshi ndiyo unawatumia kwenye kazi za kiraia aisee maagizo ya makonda anayajua mwenyewe
 
'Ninja' wakati mwingine yuko fresh sana maana sasa kila mtu anaamua atakavyo mwisho wa siku watu wataondokana na unyonge na kitachofuata na shida juu ya shida,itakuwa nipige nami nikupige,patachimbikaaaa
 
Amamkosoa mkuu msaidizi? Hajui hata uwaziri huo kaupata kwa kushauriana Makonda na Magu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom