Waziri Lugola amtimua Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa kwenye kikao kwa kuchelewa

Nguvu za soda hizi zitatulia muda si mrefu, acha kukurupuka mkuu. Tumia akili na busara ni sio vitisho na mikwala mbuzi.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemfukuza kikaoni Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa kwa kuchelewa kufika kikaoni.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amemfukuza kikaoni Kamishna Mkuu wa Magereza, Juma Malewa kwa kuchelewa.

Lugola amemfukuza Dk Malewa leo Julai 6, saa tano asubuhi ikiwa ni dakika chache baada ya kikao hicho kuanza.

Awali, Lugola alisema ikifika saa 5 kamili, mlango ufungwe na kama alivyoagiza, ulifungwa. Ilipofika saa 5:1 mlango ulifunguliwa ili Dk Malewa aingie.

Baada ya kuingia Dk Malewa, Lugola akahoji kwa nini amefunguliwa mlango?

Licha ya Dk Malewa kuomba msamaha, Lugola alikataa kata kata. Pia Lugola ameagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, kumshusha cheo hadi kubaki na nyota tatu, mkuu wa usalama barabarani, Mbeya, Leopold Fungu.

Pia ameagiza Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoa wa Kagera, George Mrutu ashushwe cheo.

Kikao hicho ni cha kimkakati cha viongozi wa vyombo na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo.
Hii inaitwa "For public consumption".
 
Hivi zile foleni tunazokuwa tunamsubiri Raisi au Makamu wake wapite tunawekwa foleni lisaa lizima hapo mnaongeleaje, au hapo muda unakuwa sawa mapapai na sio mali tena?
Ishu ni moja tu, muda ni mali basi na kuzubaa ndo utamaduni tunaotakiwa kudili nao mfano hayo ma fly overs ni katika kutackle hili tatizo
 
Ni uwaziri tu au kuna kitu alifanyiwa na jeshi hivyo anahasira nao analipiza kisasi?
 
Kifungu cha C.3 (1)(2)(3) na (4) cha The Police Force Service Regulations, 1995 kimeelezea bayana taratibu zinazopaswa kufuatwa pale ambao Afisa Wa Cheo kuanzia mkaguzi Msaidizi hadi cha Kamishna Msaidizi Wa Polisi.
Ni pale tu IGP atakapojiridhisha ya kuwa kosa lililotendwa na Afisa linastahili kuchukuliwa hatua ya kuachishwa Kazi, kutengua uteuzi wake ,kushushwa cheo au kupunguziwa Mshahara wake.
Na IGP atakachofanya ni Kuandaa taarifa( report) ya Uchunguzi Wa mashtaka pamoja na maelezo ya kina kuhusiana na zile tuhuma zinazomkabili Mkaguzi/ Afisa pamoja na Maoni yake kwa Katibu Mkuu .
Baadae Katibu Mkuu akiipitia Report husika na ndipo ataelekeza nini kifanyike ,au anaweza kuruhusu uchunguzi Wa kina ufanyike tena dhidi ya tuhuma tajwa na atarudisha shauri kwa IGP ili afanye tena uchunguzi na kumletea tena taarifa zaidi na ndipo ataweza kutoa adhabu na kumjulisha Afisa anaetuhumiwa kuhusiana na Yale yaliofikiwa dhidi yake.
 
N
tunapoelekea tunaenda kuminyiana risasi live bila chenga, nipambane porini na mbung'o na mbu ili nipate hicho cheo alafu leo uje ukishushe tu kama mkeo anavyoshusha kabati au chandarua ya chumbani kwsko, labda hicho cheo kiwe kimekuja kwa njia ya DHL, otherwise siku nitakayoshika chuma na ukapitisha pua yako ubongo naumwaga.

Nakuelewa sana. Usiombe kudhalilishwa na mkuu wako ambaye ni mkuu kwa sababu ya uteuzi tu, ila unamzidi kila kitu. Elimu, umri na hata uelewa wa mambo!

Usipotulia unaweza andika barua ya ku resign!
 
Kukurupuka anakuweza kigwangala tu .yeye pekee ndio mpaka leo hajapata side effects
 
commissioner wa magereza ndie mkuu wa magereza nchi nzima? au wapo wengi ma commissioner?
Commissioner was magereza sio mkuu was magereza nchi nzima, Bali mkuu wake ni " kaminishina generali wa magereza- CGP"

NB: sio kila kamishina wa magereza ni mkuu wa magereza.
 
Back
Top Bottom