Waziri kuwapa adhabu askari mbele ya wananchi ndani ya kikosi kuna tafsiri gani kwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
1. Tafsiri ya kwanza ya kile alichofanya kigwangala ni - Waziri ajui majukumu yake na ajawahi kufunzwa au hata kupewa miiko ya kiaskari.

2. Mkuu wa kikosi hajui wajibu wake, analojukumu la kuilinda taasisi pamoja na askari anaowaongoza ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti wale wote wanaotaka kuwadhalilisha askari wake. Huyu mkuu wa jeshi USU anapaswa kuondolewa, ataondolewa kwa internal force au external means vyombo vingine, lengo nikurejesha trust kwa askari wetu.

3.Kitendo kile kwa wazee wale Ni kuwaondolea utu kwa familia zao,

4. Mhe Waziri anapaswa kuadhibiwa kwa kuwavunja moyo wapiganaji, Lugola aliwahi kuyajaribu haya lakini askari walikuja kuonyesha kwamba walikuwa na chuki naye baada ya kuondolewa kwenye uwaziri.

5. Nidham ya jeshi airejeshwi na mfumo wa kiraia bali urejeshwa na askari wenyewe. Unachokiona Kama dharau kwako yawezekana kwao ni manjonjo ya kunogesha sherehe.

Ile fedhea imevuka hadi kwenye majeshi mengine na ikiachwa inamadhara makubwa kwa siku za usoni kwa viongozi wa kisiasa ambao ulinzi wao mkubwa unategemea askari wadogo wanaodharaulika na kudhalilishwa.

Pia soma >Kwa hili, Kigwangalla hufai kuwa hata mbunge
 
It's extremely an extraordinary abuse of power
Hata mi anashangaa hiki kimya kinatoka wapi.
Mkuu mwenyewe pamoja na mambo yote huwa anawaheshimu sana Askari
Hawa mawaziri vijana wanakwama sana na kiukweli wanatuangusha mno
 
Back
Top Bottom