Waziri Kundo Mathew asisitiza miradi ya TEHAMA iguse Watanzania, agusia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew amewataka wafanyakazi wa Wizara yake kuielewa miradi ya kitaifa inayotekelezwa na Wizara hiyo na kutafsiri ili kuhakıkisha utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo yanakuwa na manufaa yanagusa maisha ya Watanzania na inaleta fursa za kijamii, kiuchumi na kiteknolojia kwa wananchi.

Naibu Waziri huyo aliyazungumza hayo juzı, 2022 akitunga baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dodoma kwa kusisitiza watumishi wa Wizara kuelimishana kuhusu miradi inayotekelezwa na Wizara ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; mfumo wa anwani za makazı, na mradi wa Tanzania ya Kidijitali ili kila mtumishi aifahamu na kuwa balozi mzuri kwa wananchi.

“Tunatakiwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati, weledi, uadilifu, viwango na ubora unaohitajika na tunapoenda kuitambulisha miradi tunayotekeleza kwa jamii tunatakiwa kuelezea mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa jumla," alifafanua Mhandisi Kundo.

Mhandisi Kundo alizungumzia haki na wajibu kwa mtumishi wa umma kuwa vinaenda pamoja na ametoa rai kwa wafanyakazi wa Wizara wanapodai haki na maslahi yao pia wakumbuke kuwa wanapaswa kuhakikisha wanaitendea haki miradi inayotekelezwa chini ya Wizara hiyo kwa kuwa wafanyakazi hao ndiyo wanaotengeneza taswira nzuri ya Wizara ambayo ndiyo atakayoibeba.

"Nasisitiza haki bila kupinda, haki hiyo ishuke mpaka kwenye utekelezaji wa miradi, tuitendee haki miradi yetu kwa kila mfanyakazi kulitendea haki eneo läke kitaalamu kulingana na taaluma yake," alisisitiza Mhandisi Kundo.

Aidha, Naibu Waziri huyo ametoa wito kwa Menejimenti ya Wizara hiyo kujali na kutengeneza mazingira ya wasaidizi wao kuona fahari katika nafasi zao za kiutumishi na mchango wanaotoa katika utekelezaji wa majukumnu kwa kuwa mafanikio ya Wizara yanajumuisha watumishi wote mpaka ngazi ya wasaidizi.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Teddy Njau amesema kuwa kikao hicho cha baraza la wafanyakazi kimefanyika kwa siku mbili ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha 2021/22 ambapo kati ya shilingi bilioni 83 zilizoelekezwa kwenye miradi hiyo, tayari shilingi bilioni 76 zimeshatumika hadi mwezi Februari, mwaka huu 2022.

Naye Mwenyekiti wa TUGHE wa Tawi la Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Laurencia Masigo amempongeza Naibu Waziri huyo kwa kuendelea kuitangaza Wizara na kuiwakilisha vema kwa wananchi pamoja na wakurugenzi, wa WIzara hiyo kwa kuendelea kusimamia miradi ya kitaifa inayotekelezwa chini ya Wizara hiyo.

Akitoa salamu zake kwa Naibu Waziri, Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Rugemalira Rutatina amesema kuwa amefurahishwa na mwenendo mzima wa baraza hilo ambalo imetimiza wajibu wake kwa kujadili hoja za baraza la wafanyakazi na siyo hoja binafsi.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi, Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma, Samwel Nyungwa amesema maelekezo aliyoyatoa Naibu Waziri huyo yamepokelewa na anaamini wafanyakazi wa Wizara hiyo wanaenda kutekeleza kwa kutafsiri miradi ya maendeleo kwa wananchi, kutambua mipaka yao katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa viwango na muda unaohitajika.

Source: Majira
 
Mkongo wa taifa una undugu gani na ule Mkongo wa Congo?
 
Back
Top Bottom