Waziri Kombani: Historia ya nchi haipelekwi mnadani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Kombani: Historia ya nchi haipelekwi mnadani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 11, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wanajamii Forums nimevutiwa na uchambuzi huu kuhusu mipango ya kubomoa jengo la Kihistoria la Mahakama Rufani Tanzania.


  Ndugu zangu,
  Tumesikia, kuwa Serikali kupitia Wizara yake ya Katiba na Sheria iko kwenye mazungumzo na mwekezaji ili mwekezaji huyo apewe jengo la kihistoria la Mahakama yetu ya Rufani. Tunaambiwa, kuwa badala yake, mwekezaji huyo atatujengea Mahakama mpya ya Rufani Mtaa wa Chimala eneo la Kivukoni.

  ” Jengo la Mahakama ya Rufani halina hadhi ya kukaa majaji wetu”- Alisema Waziri wa Sheria na Katiba Mheshimiwa Celina Kombani. Na kwamba hiyo ndio moja ya sababu ya kutaka jengo hilo apewe mwekezaji atakayetujengea jengo jipya la mahakama.

  Kama nchi tumefikia mahali pabaya. Mahali ambapo tuko tayari kuuza na kubinaifsisha hata visvyotakiwa kuuzwa na kubinaifsishwa. Kamwe historia ya nchi haipelekwi mnadani na kukabidhiwa dalali ainadi.

  Majuzi hapa, kupitia mtandao wangu; MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo, niliwauliza watembeleaji wa mitandao wajibu swali la ’Pima- Maji ya Mjengwa’, kwamba; Je, Jengo la Mahakama ya Rufani apewe mwekezaji? Na swali hilo liliambatana na maelezo husika kuwa mwekezaji angejenga jengo jipya la mahakama.

  Zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wa mtandaoni waliopiga kura walipinga jengo hilo la Mahakama ya Rufani kupewa mwekezaji. Ni dhahiri, kuwa walielewa umuhimu wa kulihifadhi jengo hilo na ndio maana walipinga.
  Ebu, ona historia ya Jengo la Mahakama yetu ya Rufani. Miaka hiyo ya enzi za ukoloni ilikuwa ni hoteli maarufu mjini ikiitwa ’Forodhani Hotel’. Inasemwa, kuwa hata Watanzania wasomi waliopata nafasi ya kwenda Ulaya walitakiwa, kabla ya kuruka na ndege, wafike hotelini hapo kwanza ili wajifunze namna ya kula kwa kutumia uma na kisu! Hii nayo ni historia yetu.

  Na mawaziri wetu hawa wanasafiri hata nchi za wenzetu. Hivi , hawajui kwamba wenzetu wanahifadhi na kulinda majengo yao ya kihistoria? Kwamba miji mikubwa duniani ina kinachoitwa ’ Mji mkongwe’ ambapo huwa ni sehemu ya kuingiza mapato kutokana na utalii. Dar es Salaam pia ni Mji Mkongwe wa tangu mwaka 1866, enzi za Sultan Seyyid Majid aliyeujenga mji huu. Wakaja Wajerumani, wakaja na Waingereza. Wote hao wameacha kumbukumbu za kihistoria kupitia majengo.

  Na si tunajua? Kuwa jengo la Mahakama ya Rufani ni la kihistoria kwa mujibu wa sheria . Ndio, limefanywa rasmi kuwa la kihistoria kwa mujibu wa tangazo la Serikali namba 498 la mwaka 1995. Na jengo hilo linalindwa kwa sheria ya nyara za Serikali namba 10 ya mwaka 1964 na ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 1979 kulifanya jengo hilo kuwa moja ya vivutio katika Jiji la Dar es Salaam kwa wanaotembelea jiji. Sasa basi, kwa nini leo tunavunja sheria tulizoziweka wenyewe?

  Tumesikia kwamba, Waziri Kombani anadai jengo hilo halina hadhi ya kukaa majaji wetu. Ndio, yawezekana kuwa kwa sasa ni jengo dogo. Ushauri ni huu, laweza kujengwa lingine, lakini si kuvunja lililopo. Maana, kihistoria jengo hilo lina hadhi kubwa sana .

  Kuna watoto na vijana wa leo wenye ndoto za kusoma na kuwa mahakimu na majaji wa Mahakama. Kwao wao, kama jengo hilo litabaki katika hali ya sasa na kutengwa chumba cha makumbusho ndani ya jengo hilo, basi, kufika katika jengo hilo na kuingia na kuona viti walivyokalia majaji wa enzi hizo na kupitisha hukumu mbali mbali za kihistoria, yaweza kuwa hamasa kubwa ya wao, sio tu kuongeza juhudi zao kufikia ndoto zao, bali pia kuongeza ari ya uzalendo kwa nchi yao.
  Ndugu zangu,

  Kule Marekani kwenye mji wa Philadelphia kuna nyumba ya kihistoria ya tangu mwaka 1776. Ni takribani miaka 200 iliyopita. Ndani ya nyumba hiyo ambayo mwonekano wake umehifadhiwa tangu miaka hiyo ndimo alimokaa Bibi Betty Ross. Huyu ni mwanammke aliyefuma kitambaa cha kwanza cha bendera ya taifa la Marekani. Mpaka hii leo, watalii kutoka mataifa mbali mbali hufika kuliona jengo hilo. Tujiulize, hivi watoto na vijana wetu wa leo wanajua ni nani aliyebuni na kufuma kitambaa cha kwanza cha bendera yetu ya taifa?


  Tujiulize, hivi watoto na vijana wetu wa leo wanajua ni nyumba gani pale Magomeni ambapo Mwalimu Julius Nyerere alikaa wakati akifanya kazi ya ualimu kule Pugu Sekondari? Siku zote, ukitaka kuwafanya watu wasiendelee, basi, wanyang’anye historia yao, maana , watakosa kujitambua , kujiamini na kuthubutu.

  Kutojitambua kama taifa yaweza kuwa na madhara kwa taifa. Moja ya madhara hayo ni hii hulka ya kupiga bei hata visivyostahili kupigwa bei. Kwa mwanadamu, kupeleka historia yako mnadani ni jaribio la kuikana historia yako. Ni jambo la huzuni na kutia simanzi. Watanzania tusingependa kukumbwa na huzuni na simanzi ya kuliona Jengo la kihistoria la Mahakama yetu ya Rufani likipelekwa mnadani. Ndio, kuliona likibomolewa na tingatinga kama ilivyokuwa kwa jengo la Salamander.

  Na hilo likitokea, tunaamini, kuwa historia itawahukumu wote watakaokuwa wamekaa kwenye meza ya mazungumzo na kuruhusu jengo letu la kihistoria kubomolewa. Na Watanzania wenzetu hao hawatakuwa na mahali pa kuikatia rufani hukumu hiyo ya historia. Nahitimisha.

  CHANZO: Mwananchi, leo Jumapili.
   
 2. K

  Kiti JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi ni huyo Kempiski aliyejenga kwenye sehemu ya immigration ya wanyama kule Serengeti? Ni huyo ambaye wilikeaks wanasema alimfanyia shopping mkulu? Imebaki sasa auziwe ikulu akatujengee ikulu nyingine Kigamboni kwani ikulu yetu haina hadhi ya marais wetu. Nawasilisha!
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mama Kombani simuamini kabisa kwenye ushughulikiaji wa mambo ya msingi tokea kipindi cha Katiba mpya
   
 4. z

  zawadi2007 Member

  #4
  Sep 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nnjii hii!! kila mwenye kupata nafasi anajitahidi kufanya kutuko ambacho historia itamkumbuka. Mama huyu naye kaona mahakama hii ni sehemu ya kukumbukwa kwake miaka ijayo.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  JK na genge lake la wababishaji huwawezi hakika na ni htari kwa Taifa langu kwa kweli .
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Celina Kombani ni mshirika wa Vasco Dagama katika mabo mengi ya kifisadi; mnakumbuka ile scandal ta watendaji wa halmashauri ya bagamoyo ambao Pinda aliwasimamisha bila hata kumualifu Kombani wakati huo waziri wa Tamisemi? Zile fedha watumishi wale waliziiba na kuzila pamoja na Kombani na ndugu wa karibu wa Vasco Dagama; ndio maana kesi yao imepigwa danadana na yule mama akatolewa Tamisemi akapelekwa kwenye wizara ambayo haielewi wacha kutoimudu badala ya kufukuzwa kazi.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tatizo wengi wa viongozi kama akina Celina Kombani na wengineo wameathirika na mfumo zembe wenye kujali maslahi binafsi na kuhemekea walio juu yao ili kulinda nafasi walizonazo. Hawajali kizazi kijacho nini watakikuta katika nchi yetu.
   
 8. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  walipopewa madaraka waliambiwa watavuna vya kutosha,hawajakuta mazao ndo maana wanavuna hata wasipopanda. Cku cyo nyingi tutaambiwa lukuv anauza bunge maana kila waziri anauza kinachomzuka. Eee Mungu walaani viongozi wa hii inji!
   
 9. only83

  only83 JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ..................Sutiiiiiiiiiiiiiiiiii ha sutiiiiiiiiiiiiiiiiiiii jamani! lol!!!
   
Loading...