Waziri Kivuli wa Habari: Serikali ya Rais Magufuli haina mamlaka ya ‘uhakimu' kufungia vyombo vya habari

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
SERIKALI YA RAIS MAGUFULI HAINA MAMLAKA YA ‘UHAKIMU' KUFUNGIA VYOMBO VYA HABARI

Uamuzi wa Serikali ya Rais John Magufuli wa kulifungia gazeti la kila siku la Tanzania Daima, kinyume cha sheria za nchi, ni mwendelezo wa vitisho na mashambulizi dhidi ya uhuru wa habari na vyombo vya habari, hali ambayo ikiachwa iendelee bila kukemewa na kupingwa itazidisha sintofahamu kubwa inayoendelea nchini kuhusu kupuuzwa kwa taratibu za kuongoza nchi.

Nikiwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, yenye wajibu mkubwa wa kuwa mlezi na msimamizi mwenye sura rafiki wa tasnia hii nyeti, natumia fursa hii kusema yafuatayo;

1. Kulaani na kupinga vikali hatua hiyo ya Serikali kuendeleza tabia iliyo kinyume kabisa na misingi ya utoaji haki, yaani kuwa mlalamikaji, kukamata, kufungua mashtaka, kuendesha mashtaka na kuwa hakimu/jaji wa kesi yake mwenyewe. Hii pia haikubaliki katika misingi ya utawala bora unaozingatia sheria.

2. Serikali imetumia vibaya na kimakosa Sheria ya Huduma za Habari Namba 12 ya mwaka 2016, kulifungia Gazeti la Tanzania Daima. Kifungu cha 54(1) cha Sheria hiyo kilichotumiwa na Serikali ya Rais Magufuli kuadhibu chombo hicho cha habari, hakitoi mamlaka YOYOTE kwa Serikali kuchukua hatua iliyochukua jana. Kutokana na msingi huu, Serikali ifikirie upya uamuzi huo na iubatilishe mara moja na kuvifungulia vyombo vingine ambavyo vimefungiwa.

3. Kitendo cha Serikali kutumia vibaya na kimakosa sheria hiyo, kinadhihirisha kuwa uamuzi huo umesukumwa na chuki na nia ovu dhidi ya gazeti hilo.

4. Aidha, hatua hiyo ambayo iko kinyume na sheria hiyo iliyotumika, ambayo imechukuliwa siku moja tu baada ya Rais Magufuli kusikika akitoa maelekezo akiwa Ikulu, imetulazimisha kuamini kuwa hatua za kufungia vyombo vya habari tangu Rais Maguli aingie madarakani, zinachukuliwa ili kufurahisha utashi, matamanio na matakwa binafsi ya Rais Magufuli.

Hitimisho

Ni vyema Rais Magufuli aache mwenendo wake na Serikali yake wa kutisha, kushambulia na kudhibiti vyombo vya habari, waandishi wa habari na uhuru wa habari kwa ujumla, kwa kila jambo ambalo liko kinyume na matendo, kauli, matamanio, matakwa, fikra, mawazo na maoni yake.

Tunatoa wito kwa wadau wa habari ambao ni Watanzania wote kusimama kidete, wapaze sauti kwa njia zozote kutetea uhuru wa habari nchini na kupinga vikali kauli na vitendo vya Rais wetu dhidi ya vyombo vya habari, hasa kuvifungia, jambo ambalo linaathiri waandishi wa habari wote katika chombo husika, wafanyakazi wengine na familia zao.

Kwa sababu Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 inayotumiwa kufungia vyombo vya habari haitoi mamlaka hayo kwa Serikali, tunasisitiza tena kuitaka Serikali ivifungulie vyombo vyote vya habari vilivyofungiwa hadi sasa, ikiwa ni pamoja na magazeti ya Mseto, Mawio, Mwanahalisi, Raia Mwema na Tanzania Daima.

Joseph Mbilinyi (Mb)

Waziri Kivuli Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Oktoba 25, 2017

Dodoma
 
Tutasikia mengi,tutajifunza mengi,tutajua mengi ?mungu Tuongezee uvumilivu na umasikini
 
Waziri Kivuli!!
Hivi ana kazi gani kisheria nchini
huyu ana mamlaka yeyote kweli!
Isijekuwa anashindwa na Mwenyekiti wa Kitongoji
 
2. Serikali imetumia vibaya na kimakosa Sheria ya Huduma za Habari Namba 12 ya mwaka 2016, kulifungia Gazeti la Tanzania Daima. Kifungu cha 54(1) cha Sheria hiyo kilichotumiwa na Serikali ya Rais Magufuli kuadhibu chombo hicho cha habari, hakitoi mamlaka YOYOTE kwa Serikali kuchukua hatua iliyochukua jana. Kutokana na msingi huu, Serikali ifikirie upya uamuzi huo na iubatilishe mara moja na kuvifungulia vyombo vingine ambavyo vimefungiwa.
Dodoma
.
Waziri kivuli kakisoma na kukielewa kifungu cha 59 cha sheria namba 12 ya mwaka 2016?
 
257e1a406d95b71d3584fe2f62b94d40.jpg

Uamuzi wa Serikali ya Rais John Magufuli wa kulifungia gazeti la kila siku la Tanzania Daima, kinyume cha sheria za nchi, ni mwendelezo wa vitisho na mashambulizi dhidi ya uhuru wa habari na vyombo vya habari, hali ambayo ikiachwa iendelee bila kukemewa na kupingwa itazidisha sintofahamu kubwa
inayoendelea nchini kuhusu kupuuzwa kwa taratibu za kuongoza nchi.

Nikiwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, yenye wajibu mkubwa wa kuwa mlezi na msimamizi mwenye sura rafiki wa tasnia hii nyeti, natumia fursa hii kusema yafuatayo;

1. Kulaani na kupinga vikali hatua hiyo ya Serikali kuendeleza tabia iliyo kinyume kabisa na
misingi ya utoaji haki, yaani kuwa mlalamikaji, kukamata, kufungua mashtaka, kuendesha
mashtaka na kuwa hakimu/jaji wa kesi yake mwenyewe. Hii pia haikubaliki katika misingi ya utawala bora unaozingatia sheria.

2. Serikali imetumia vibaya na kimakosa Sheria ya Huduma za Habari Namba 12 ya mwaka 2016, kulifungia Gazeti la Tanzania Daima. Kifungu cha 54(1) cha Sheria hiyo kilichotumiwa na
Serikali ya Rais Magufuli kuadhibu chombo hicho cha habari, hakitoi mamlaka YOYOTE kwa
Serikali kuchukua hatua iliyochukua jana. Kutokana na msingi huu, Serikali ifikirie upya uamuzi huo na iubatilishe mara moja na kuvifungulia vyombo vingine ambavyo vimefungiwa.

3. Kitendo cha Serikali kutumia vibaya na kimakosa sheria hiyo, kinadhihirisha kuwa uamuzi huo umesukumwa na chuki na nia ovu dhidi ya gazeti hilo.

4. Aidha, hatua hiyo ambayo iko kinyume na sheria hiyo iliyotumika, ambayo imechukuliwa siku moja tu baada ya Rais Magufuli kusikika akitoa maelekezo akiwa Ikulu, imetulazimisha kuamini
kuwa hatua za kufungia vyombo vya habari tangu Rais Maguli aingie madarakani,
zinachukuliwa ili kufurahisha utashi, matamanio na matakwa binafsi ya Rais Magufuli.

Hitimisho
Ni vyema Rais Magufuli aache mwenendo wake na Serikali yake wa kutisha, kushambulia na kudhibiti vyombo vya habari, waandishi wa habari na uhuru wa habari kwa ujumla, kwa kila jambo ambalo liko kinyume na matendo, kauli, matamanio, matakwa, fikra, mawazo na maoni yake.

Tunatoa wito kwa wadau wa habari ambao ni Watanzania wote kusimama kidete, wapaze sauti kwa
njia zozote kutetea uhuru wa habari nchini na kupinga vikali kauli na vitendo vya Rais wetu dhidi ya vyombo vya habari, hasa kuvifungia, jambo ambalo linaathiri waandishi wa habari wote katika chombo
husika, wafanyakazi wengine na familia zao.

Kwa sababu Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 inayotumiwa kufungia vyombo vya habari
haitoi mamlaka hayo kwa Serikali, tunasisitiza tena kuitaka Serikali ivifungulie vyombo vyote vya habari vilivyofungiwa hadi sasa, ikiwa ni pamoja na magazeti ya Mseto, Mawio, Mwanahalisi, Raia
Mwema na Tanzania Daima.

Joseph Mbilinyi (Mb)
Waziri Kivuli Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
25/10/2017.
Dodoma.
 
Ni kuwa serikali haina mamlaka ya kufungia gazette au serikali ya maguFul ndo haina mamlaka ya kufungia magazeti? Maana hili suala la kufungia magazeti halijaanza jana

Lakin pia kwa makosa ya TD nadhan hawana cha kusema wanaonewa tofaut na yale magazeti ya mwanzo wanaweza jtetea

Ila pia ni vema wazir kivuli aka nukuu hcho kifungu cha sheria nasi tujue kinasemaje badala ya kusema serikali haina mamlaka akati suala hili limeanza tangu enzi
 
Umenena vyema sana mkuu. Toka lini serikali ikakosa mamlaka ya kufungia magazeti yanayokiuka utaratibu? Naona siku hizi kila kitu kinaendeswa kisiasa zaidi kuliko kiuhalisia. Huyo waziri kivuli kaweka kifungu ambacho hakihusiki kufungia magazeti ndio anataka kuuaminisha uma kuwa serikali imekosea. Hajui kuwa sheria hiyo hiyo inavyo vifungu vingi vinavyotoa mamlaka kwa serikali!

Tanzania Daima wenyewe hawana la kusema, sasa inashangaza hawa wasemaji wananini. Mbali na hayo kama mtu au gazeti halijaridhishwa na hatua za serikali linayo nafasi ya kufungua kesi mahakamani.
 
Ndio magazeti yameshafungiwa hivyo!!, raia mwema gazeti nilipendalo linaelekea mwezi sasa pasipo kuonekana mtaani.

Ni suala la kuwa makini kwenye weledi wa waandishi na uandishi wenyewe kwa ujumla.
 
Anayoyafanya huyu bwana sidhani hata kama viongozi wenzie wastaafu wanafurahia,,,,,anaipa nchi sifa mbaya kabisa,,,,,, yote haya kayataka Kikwete na roho yake mbaya kwa rafiki yake,,,,bora angemuacha tu rafiki yake apitishwe awe presidaa, ,, aliemtaka yeye awe ameshindwa kupitishwa kwakuwa hakuwa kauzu wakutumia ubabe ili apitishwe, ,, hatma yake ametupa sisi mtihani mkubwa mno,,,
na mpaka yeye uenda ataguswa na huyu Bwana, , iwe kwenye maslai yake au ya jamaa zake
 
SERIKALI YA RAIS MAGUFULI HAINA MAMLAKA YA ‘UHAKIMU' KUFUNGIA VYOMBO VYA HABARI

Uamuzi wa Serikali ya Rais John Magufuli wa kulifungia gazeti la kila siku la Tanzania Daima, kinyume cha sheria za nchi, ni mwendelezo wa vitisho na mashambulizi dhidi ya uhuru wa habari na vyombo vya habari, hali ambayo ikiachwa iendelee bila kukemewa na kupingwa itazidisha sintofahamu kubwa inayoendelea nchini kuhusu kupuuzwa kwa taratibu za kuongoza nchi.

Nikiwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, yenye wajibu mkubwa wa kuwa mlezi na msimamizi mwenye sura rafiki wa tasnia hii nyeti, natumia fursa hii kusema yafuatayo;

1. Kulaani na kupinga vikali hatua hiyo ya Serikali kuendeleza tabia iliyo kinyume kabisa na misingi ya utoaji haki, yaani kuwa mlalamikaji, kukamata, kufungua mashtaka, kuendesha mashtaka na kuwa hakimu/jaji wa kesi yake mwenyewe. Hii pia haikubaliki katika misingi ya utawala bora unaozingatia sheria.

2. Serikali imetumia vibaya na kimakosa Sheria ya Huduma za Habari Namba 12 ya mwaka 2016, kulifungia Gazeti la Tanzania Daima. Kifungu cha 54(1) cha Sheria hiyo kilichotumiwa na Serikali ya Rais Magufuli kuadhibu chombo hicho cha habari, hakitoi mamlaka YOYOTE kwa Serikali kuchukua hatua iliyochukua jana. Kutokana na msingi huu, Serikali ifikirie upya uamuzi huo na iubatilishe mara moja na kuvifungulia vyombo vingine ambavyo vimefungiwa.

3. Kitendo cha Serikali kutumia vibaya na kimakosa sheria hiyo, kinadhihirisha kuwa uamuzi huo umesukumwa na chuki na nia ovu dhidi ya gazeti hilo.

4. Aidha, hatua hiyo ambayo iko kinyume na sheria hiyo iliyotumika, ambayo imechukuliwa siku moja tu baada ya Rais Magufuli kusikika akitoa maelekezo akiwa Ikulu, imetulazimisha kuamini kuwa hatua za kufungia vyombo vya habari tangu Rais Maguli aingie madarakani, zinachukuliwa ili kufurahisha utashi, matamanio na matakwa binafsi ya Rais Magufuli.

Hitimisho

Ni vyema Rais Magufuli aache mwenendo wake na Serikali yake wa kutisha, kushambulia na kudhibiti vyombo vya habari, waandishi wa habari na uhuru wa habari kwa ujumla, kwa kila jambo ambalo liko kinyume na matendo, kauli, matamanio, matakwa, fikra, mawazo na maoni yake.

Tunatoa wito kwa wadau wa habari ambao ni Watanzania wote kusimama kidete, wapaze sauti kwa njia zozote kutetea uhuru wa habari nchini na kupinga vikali kauli na vitendo vya Rais wetu dhidi ya vyombo vya habari, hasa kuvifungia, jambo ambalo linaathiri waandishi wa habari wote katika chombo husika, wafanyakazi wengine na familia zao.

Kwa sababu Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 inayotumiwa kufungia vyombo vya habari haitoi mamlaka hayo kwa Serikali, tunasisitiza tena kuitaka Serikali ivifungulie vyombo vyote vya habari vilivyofungiwa hadi sasa, ikiwa ni pamoja na magazeti ya Mseto, Mawio, Mwanahalisi, Raia Mwema na Tanzania Daima.

Joseph Mbilinyi (Mb)

Waziri Kivuli Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Oktoba 25, 2017

Dodoma
Na ndiyo maana akawa waziri kivuli.
 
Anayoyafanya huyu bwana sidhani hata kama viongozi wenzie wastaafu wanafurahia,,,,,anaipa nchi sifa mbaya kabisa,,,,,, yote haya kayataka Kikwete na roho yake mbaya kwa rafiki yake,,,,bora angemuacha tu rafiki yake apitishwe awe presidaa, ,, aliemtaka yeye awe ameshindwa kupitishwa kwakuwa hakuwa kauzu wakutumia ubabe ili apitishwe, ,, hatma yake ametupa sisi mtihani mkubwa mno,,,
na mpaka yeye uenda ataguswa na huyu Bwana, , iwe kwenye maslai yake au ya jamaa zake
Siyo kidogo
 
Ata ma mvi agombee na kikombe cha kahawa,kwa mtanzania anaye jitambua, asiye na chembe ya shaka kichwani mwake hawezi kumpigia kura.
 
Back
Top Bottom