Waziri Kitila Mkumbo: Mgomo wa madereva wa kiwanda cha Dangote umeisha, uongozi umekubali kuwalipa stahiki zao

RtsHjcq

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,753
5,504
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo, jana amekutana na kufanya mazungumzo na Madereva takribani 500 wa Kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara, waliokuwa wamegoma kwa siku 12, baada ya majadiliano Uongozi wa Kiwanda hicho umekubali kuwalipa stahiki zao ikiwemo mishahara na kuahidi kurejea kazini leo.

"Tutasimamia kuhakikisha Kiwanda cha Dangote kinaendelea na uzalishaji na kupata faida, lakini kinatekeleza wajibu wake kwa Watu wetu, hatutaki watanzania wanyanyasike katika Nchi yao”

“Nchi hii ni huru, tutalinda haki za Madereva, nanyi pia mtulindie heshima yetu kwa Mwekezaji kwa kuwa Waaminifu”-Kitila Mkumbo
 
Madereva wa Kampuni ya Dangote Tanzania wasitisha mgomo na kurudi kazini

Waziri wa Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe kwa pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo wamaliza mgomo wa Madereva wa kiwanda cha Dangote Tanzania Kilichopo Mtwara

Kampuni ya Dangote Tanzania na FOS wote kwa pamoja wamekubali kushughulikia kero mbalimbali zilizopelekea Madereva hao kugoma.

 
Back
Top Bottom