Waziri Kiongozi kaamua kuwa mfagiaji... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Kiongozi kaamua kuwa mfagiaji...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibunango, Feb 21, 2009.

 1. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Waziri Kiongozi wa SMZ ameamua kuwa mfagiaji wa barabara katika Halmashauri ya Manispaa ya Zanzibar. Hatua yake hii imetokana na barabara katika halmashauri hiyo kukithiri wa michanga kiasi cha kushindwa kutofautisha iwapo ni za lami au la!

  Aidha watafiti wa mambo ya siasa wanasema hatua hiyo ni sehemu ya mpango wake wa kujiweka karibu na wananchi wa visiwa hivyo katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, huku baadhi ya watendaji wa Manispaa wakidai ni njia yake ya kukwamisha ununuaji wa mtambo wa kisasa wa kusafisha barabara visiwani humo... Kwa maelezo zaidi cheki hapa
   
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Watafitiwa wa mambo ya siasa wakisema na wewe kibungo kwa kutuwekea blog yako ya propaganda ni sehemu ya mkakati wako wa kugombea uwakilishi ili uchukue nafasi ya Shamsi 2010 au umenunuliwa kumchafua utapinga?
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hapo hakuna kununuliwa wala propaganda, Waziri Kiongozi ameamua kufagia barabara, labda ni kutokana na kupungukiwa na kazi za kufanya katika Ofisi yake. Hii si mara yake ya kwanza kuweka majukumu yake pembeni na kukimbilia kufanya kazi za manispaa ingawa manispaa hiyo haipo chini ya Ofisi yake.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  Du.... Kama WK kaamua kufagia barabara hiyo mbona poa tuu. Nikiwa shule ya msingi iliyoko jirani na Ubalozi wa China, ambapo ubalozi ndio hapo hapo na makazi ndio hapo hapo.
  Mesenja mmoja akatumwa apeleke ujumbe wa siri kwa balozi ila ahakikishe anampa balozi mwenywe mkononi.
  Mesenja kufika, kupitia geti la grill, aliona wachina wengi wanafanya shughuli za usafi ubalozini hapo, ndipo akabonyeza kengele na kuja kufunguliwa na mmoja wao huku ameshika ufagio mkononi.
  Mchina huyo akamkaribisha kwa lugha ya Kiswahili na kumuuliza shida yake.
  Mesenja akajibu namuhitaji balozi mwenyewe, Mchina akamjibu "sawa, sema shida yako". Jamaa akasita baadaye akajibu siwezi kukwambia wewe hii shida anatakiwa aisikilize balozi mwenyewe na sio mfanyakazi wa ubalozini.

  Ndipo Mchina akamjibu "Mimi ndiye balozi mwenyewe". Jamaa akapigwa na butwaa na kubaki ameduwaa asijue la kufanya ndipo Mchina akamwambia tena sema shida yako, ndipo mesenja akaomba msamaa na kukabidhi ujumbe.

  Hivyo ya WK kufanya usafi poa sana tena afike mpaka soko kuu hapo darajani na kuelekea ule upande wa soko la samaki, atakuwa ameisaidia sana ZnZ na 2010 rais yeye!.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Patakuwa hapakaliki hapo Zenj...
   
 6. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mmmh mambo hayo !

  usiombe kipooo poo cha jino kikagunda
   
 7. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Huyu WK ni nationalist mno. Akigombea na akapata tusahau muungano
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  MMhm, hapana ila itakuwa ni kinyume chake, Zanzibar kama nchi itatoweka na kuwa mkoa fulani hivi.... Tatizo hana ubavu wa kusimama mbele ya Watanganyika... hivyo atakuwa akiburuzwa tu!
   
 9. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kibunango acha propaganda...

  Kama unamjua vizuri Nahodha ni wazi utakubalia this is more that political expedience. This guy has always been simple person hata alipokuwa mwakilishi wa kawaida alikuwa na kibaskeli kake na mpanda daladala. Uteuzi wake ulimkutia njiani akikokota baiskeli.Na hii ni hulka ya kizanzibari ambayo tunaiona kwa viongozi wengi watokao huko. Hulka hii ndio asset muhimu ya wazanzibari hadi sasa inayowafanya kuaminika zaidi kuliko wanasiasa wengine nchini. Ingawa wakati mwengine huwa sababu ya kuzorota kwa mikakati ya kimaendeleo na kwa wengine kuonekana kama kujirahisisha mbele ya jamii ya enzi za "waheshimiwa"

  Kwangu mimi huu ni ujumbe mkali kwa watendaji wa manispaa ya Zanzibar kuwajibika ipasavyo.

  Omarilyas
   
 10. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kuwa Zanzibar Nationalist hakuna maana ya kutokuwa na muungano isipokuwa kuhakikisha kuwa na muungano wenye kuheshimiana na ku-recognize all union parties interests and aspirations.

  omarlyas
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Iwapo anataka Manispaa iwajibike angeweza kufagia mara moja tu na kuwataka waheshimu kazi zao. Hii ni mara ya pili kwa waziri kiongozi kufagia barabara huku akiweka kando matatizo ya msingi ambayo yanasababisha barabara hizo kuendelea kuwa chafu.

  Waziri huyo amewahi kuwa miongoni mwa wanzanzibari ambao walishiriki katika programu ya miji endelevu, hivyo anajua nini maana ya kutatua tatizo. Na iwapo anafikili kama yeye ni Waziri Kiongozi na akishika ufagio barabara zitakuwa safi kila siku anakosea sana tena sana. Ni wajibu wake kujua ni kwa nini barabara hizo ni chafu ilhali zinafagiliwa kila siku. Ni wajibu wake kabla ya kukimbilia kushika ufagio kujua kifanyike nini iwapo panahitajika barabara zisizokuwa na michanga mjini humo.

  Awali kitengo cha wasafisha barabara kilikuwa na wafagiaji zaidi ya 60 na sasa wapo ishirini tu. Barabara nyingi zimejengwa katika hali ya kuruhusu michanga kuingia barabarani. Kama kweli alikuwa anataka kuona kuwa tatizo la vumbi barabarani linakwisha ilimpasa kuwashirikisha wataalumu katika fani hiyo na sio kusimama kifua mbele mbele ya Baraza la Wawakilishi na kusema kuwa atafagia barabara zote chafu!

  Ina maana yeye akishika fagio barabara hizo hazitochafuka tena?
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  WK is a down to earth man of the people. Watu wa aina yake kama alivyo RZ na MBM yaani watu wa kupelekwa pelekwa tuu ndio watadumisha Muungano kwa kuvumilia na kustahimilia ubabe wa Bara.
  Kwa wapenda demokrasia ya kweli, alichotaka kufanya Jumbe na Dourado ndicho ZnZ inachotaka. Tuliyaona yaliyomkuta.
  Dr. Gharib Bilal pia ni MZnZ wa kweli, yaliyomkuta tunayajua ndio maana kila siku Seif anashinda lakini hapewi nchi, kisa bara yaogopo Seif hata pelekwa pelekwa.
  2010 kama sio Mwinyi ni Seif Khatib, lazima wabara wawapangie. Walahi WZnz wakichoka, hata wana CCM wataipa CUF, na ndipo Muungano afanyiwe mapitio kwa ZnZ kupewa haki zake stahili kama mbia mwenye haki sawa na sio mmoja kumburuza mwingine.
   
 13. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Ni safi sana WK kufagia na kupata feeling ya kazi za walalahoi.Kuna viongozi ambao wakishachaguliwa tu kumwona kwa karibu ni kwenye gari la 4WD la kiyoyozi.
  Baada ya muda anatakata kama katoka kwenye neema, wacha kibarua kiote nyasi ndo utamwaona akisalimia hata wananchi wake.
  Tuwe karibu na watu, tufanye kazi zao cheo ni dhamana.
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kufagia kwa WK sio kuwa anataka kuwa karibu na walala hoi au kupata feeling au kutoa mfano, bali ni kuwapa taarifa kuwa hawawezi kazi na yeye ndio anayeweza kufagia barabara vizuri zaidi yao.

  Hafagii barabara kama motisha kwa wafanyakazi hao, ambao wanafanya kazi hiyo katika mazingira magumu bali ni sehemu yake ya kukataa wazo la kununuliwa kwa mtambo/mashine/gari la kuweza kusafisha barabara na hivyo kuziba pengo la upungufu wa wafanyakazi katika kitengo cha wasafisha barabara wa Halmashauri ya Manispaa ya Zanzibar.

  Rejea hotuba yake ya kufunga kikao cha Baraza la Wawakilishi aliyoitoa mwishoni mwa mwezi wa kwanza mwaka huu.
   
 15. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duh.Akipigania Kib. kura ya kwanza ya kwangu. Na nitampiogia debe kamanda.
   
 16. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Usipake mafuta kwa mgomgo wa chupa
   
 17. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Du Pasco I like the way u talk.
   
 18. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hata hivyo, Kinu it is all in the positive side kwa wananchi,viongozi wangapi wanjishusha?
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Nahisi ujanifahamu. Kuna tatizo la muda mrefu la uchafu wa barabara, na kinachotakiwa ni uvumbuzi wa kudumu kuona kuwa barabara hizo haziwi chafu tena.

  Sasa iwapo WK atafagia barabara ambapo hardly itakuwa chini ya nusu saa, bado hatakuwa ametatua tatizo hilo ambalo limeripotiwa katika Baraza la Wawakilishi. Anachojaribu kufanya ni sawa na kejeli kwa wafagiaji wa kila siku wa barabara hizo na sio kujishusha kama unavyodai.
   
 20. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kamanda - nafikiri ni kejeli. Kwa kweli kama amedhamiria ilikuwa akae kikao na wafagiaji wamueleze shida zao. Azisikilize. Halafu pamoja na kutumia teknologia ya kisasa (hayo magari ya kuzoa taka na kufagia taka) na nguvu kazi-ya wafagiaji- iliyohamasishwa bila ya shaka mji ungengara. Lakini Shamsi -anapuyanga tu.
   
Loading...