Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 677
Waziri Kiongozi awakoromea wapinzani
2008-06-29 12:26:42
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imesema kamwe haiwezi kuwakaribisha wapinzani katika Kamati ya Mazungumzo ya kutatua kero za Muungano.
Akifunga mjadala wa makisio ya bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka wa fedha wa 2008/09 Waziri Kiongozi Bw. Shamsi Vuai Nahodha, alisema baadhi ya viongozi wa upinzani ndio wahusika wakuu wa hizi zinazoonekana sasa kuwa kero za Muungano hivi sasa.
Alisema suala la mafuta liliingizwa katika orodha ya mambo ya Muungano wakati huo kiongozi wa hivi sasa wa upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Bw. Abubakar Khamis Bakar, akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar miaka ya 1980.
Waziri Kiongozi alisema wakati ule Waziri Kiongozi wa serikali ya Zanzibar alikuwa Maalim Seif Sharif Hamad ambaye hivi sasa ni Katibu Mkuu wa Chama cha CUF.
Alisema kutokana na hali hiyo, anaamini viongozi hao na wengine wa upinzani, walichangia kuongezeka kwa kero za Muungano zinazopigiwa kelele hivi sasa na wao wakiwa mstari wa mbele.
Hata hivyo, alisema serikali ipo tayari kupokea maoni yao, na utaratibu unaotumika sasa wa kuzungumzia kero za Muungano ndio utakaoendelea kutafuta ufumbuzi wa matatizo yaliopo.
Akigusia kero hizo, Waziri Kiongozi alisema kwa vile suala la mafuta liliingizwa ndani ya Muungano kinyemela, basi njia nzuri ya kulitoa ilikuwa ni ile ya kinyemela.
Kauli hiyo ya Waziri Kiongozi ilikuwa ikijibu maswali yaliyotolewa na kiongozi wa upinzani, Bw. Bakara aliyesema kuwa kero za Muungano ni masuala ya kitaifa, hivyo ni vyema na watu wengine wakakaribishwa katika mazungumzo hayo.
Alisema inashangaza kuwa Tume ya Pamoja ya Fedha haijatoa ripoti yoyote ya shughuli zake tokea kuundwa kwake miaka mitatu iliyopita.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa upinzani, inaonekana ni vyema na hiyo tume ikaundiwa tume kuchunguza shuguli zake.
Waziri Kiongozi alisema kuwa mgao wa mafuta na gesi, ripoti yake inatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, mwaka huu.
Lakini kabla ya mshauri elekezi kuanza kazi, atakutana na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ili kubadilishana mawazo na kupata maoni yao.
Alisema jumla ya shilingi 328 milioni zinatarajiwa kutumika kwa hizo shughuli za mshauri elekezi za kufanya utafiti na kuweka utaratibu wa mgao wa mapato ya mafuta na gesi kati ya pande mbili za Jamhuri ya muungano.
Alisema kwa hivi sasa Kamati ya Mazungumzo inaendelea kufanyia kazi utaratibu wa kuchangia gharama za Muungano.
Hata hivyo, akaunti ya pamoja kati ya Serikali ya Muungano na ya Zanzibar itayosimamia suala hili bado haijaanzishwa.
Waziri Kiongozi alikiri kuwa ni kweli Tume ya Pamoja ya Fedha imechelewa kutoa ripoti yake juu ya mgawanyo w amapato,lakini hii inaeleweka kwa kuwa suala hili ni zito na linahitaji kufanyiwa kazi kwa umakini.
Hivi sasa, alidokeza, yapo maoni tafauti juu ya mgao huo. Baadhi ya watu wanasema Zanzibar ipewe asilimia 10 na wengine wanaona ni vyema ikapatiwa asilimia 15, badala ya mgao wa asilimia 4.5 unaotumika hivi sasa.
Nahodha alikataa kuwepo ubaguzi wa ina yoyote kati ya Visiwa vya Unguja na Pemba isipokuwa bajeti ya kisiwa ya Unguja inaonekana kuwa kubwa kwa vile ndio makao makuu ya nchi.
SOURCE: Nipashe