Waziri Kingwangwalla, mbona January imefika na kampuni ya waarabu bado wapo Loliondo?

Alikurupuka mno. Tatizo letu ni kuwa hamna continuity Kwenye wizara zetu nyingi, mawaziri hawaoni umuhimu wa kupokezana kijiti kiutendaji. Kila anae ingia Kwenye nafasi anafanya bidii kumdiscredit aliyemtangulia hata kama kuna mazuri machache aliyafanya. Kila wizara ikipata waziri mpya na kila kitu kinaanza upya. Hatuwezi kupanga mambo na kutaka lazima tuone matunda ya mipango yetu ili tu tupate mitaji ya kuturudisha Kwenye nafasi hizo. Huo ni uchoyo na ubinafsi wa hali ya juu kabisa na hata siku moja haiezi kuitwa uzalendo. Let's put Tanzania first!
 
Hapo kuna kampuni nyingi za uwindaji ila hawa waarabu wanajeuri saana.

Thomson, Normad na Dorobo kidogo wanaiheshimu jamii inayoishi pale. Au tatizo ni nature ya mkataba?
Hizo kampuni pia wanawinda?
 
Hizo kampuni pia wanawinda?
Hawawindi. Ila wanatoroka kulipa maduhuli ya serikali ndani ya hifadhi za taifa. Nje ya hifadhi za taifa miundo mbinu ya ukusanyaji fedha kwa shughuli za kiutalii wa picha ni duni kwani vijiji havina uwezo wa kuzungukia kambi zote za kitalii zilizopigwa kwenye ardhi Yao kila siku ili kuhakiki idadi ya wageni waliolala au kuingia katika siku husika hivyo kufanya makampuni ya picha kutengeneza mega profits.
 
Hizo kampuni pia wanawinda?
Thomson hawa wanafanya shughuli za utalii mkuu.

Hawa Dorobo wenyewe ni utalii wa kiikolojia.

[Kleins] ni nchi ndani ya LGCA... zamani walikuwa wanagawa nguo na vyombo mbali mbali kila mwisho wa mwaka siku hizi sijui kama wanafanya hivyo.
 
Back
Top Bottom