Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
Septemba 16, 2021
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji amesema hatakuwa tayari kuvumilia Vyombo vya Habari na Waandishi watakaoandika habari za kutaka kulichafua Taifa.
Waziri Kijaji ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua mafunzo ya Kamati ya Ukaguzi ya Wizara hiyo jijini Dodoma.
"Lazima katika utendaji kazi wa Waandishi wa Habari watangulize uzalendo kwa Taifa."
"Niwahakikishie, sitakuwa mvumilivu kwa yeyote atakayejaribu kufanya hivyo kuandika habari zenye viashiria vya Uvunjifu wa Amani, tutachukua hatua," amesema.
Chanzo: Dk. Kijaji avipiga mkwara vyombo vya habari