Waziri Kijaji: Nasubiri ripoti ya Tume inayochunguza upya tukio la Makonda kuvamia Clouds

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,722
2,000
Ni zamu ya ridhwani kumshikisha adabu, tena ni taratibuuuuu, hakuna haraka, hii itamfanya bashite awe na stresa nyingi mno kabla hajaenda kwa mwenzake Sabaya.

Waje kugusa vyeti feki.

Waje kugusa kesi alizobambikia watu kuuza madawa ya kulevya ili apewe kadi zao za umiliki wa magari ya kifahari.

Waje kugusa ule magendo yake pale bandarini.

n.k

Yaani Bashite alitengeneza uadui na vigogo wengi sana na muda huu watambanika mzima mzima kihalali kabisa bila kumbambikia vya uwongo.

Vuta picha Manji alivyo henya kwasababu ya Bashite, Vuta picha kina Gwajima wamelala polisi, vuta picha kina mbowe walilala huko, vita picha madon kibao walivyo nyanyaswa!!! Bashite kazi unayo aisee!! Hawa watu hawataweza kukusamehe kirahisi rahisi, unayoyaona yote haya ni jitihada zao za kukutia displini.

Bashite huchomoki aisee!!!

Nakushauri utokomee kusikojulikana maana muda bado unao na pesa ulizodokoa ni nyingi, Sepa fastaaaa!!! huko mahakamani huruki aisee, na ukienda huko mahabusu / jela tayari madon watakuwa wamekuandalia vijana wao.l, yani kama dozi ile ya mara 3 kwa kutwa.
 

Tardy

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
816
1,000
Waache chokochoko za kisiasa.
Kisheria hakuna haja ya ripoti ya uchunguzi.
Clouds ndio mashahidi na Nape.
Wizara ya utamaduni ina ripoti yote.

Lissu nae atakujamfungulia kesi
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,721
2,000
Mbona waziri kasema jambo nusu nusu.
Tulitaka kujua haya:

1. Hiyo tume iliundwa lini, na nani na inapaswa kukabidhi hiyo ripoti lini? (Kama ni tume ile ile ya wakati ule iliyoundwa na Nape, ilipewa siku saba na ilipaswa kuwa imekabidhi ripoti kipindi kile kile....)

2. Huyu waziri ana mamlaka gani katika kukabiliana suala la Makonda kuvamia Clauds media. (Kwa mfano kama tume itamuona Makonda alikuwa na makosa, waziri atafanya nini?)

3. Kwanini suala lile halikumalizwa kipindi kile kile na badala yake limekaliwa kimya muda wote?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom