Waziri Kigwangalla: Walishindwa kuniua wakati ule! Naingia vitani kwa silaha zote na vita ni asili yangu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,325
Anaandika Waziri wa Maliasili na Utalii kupitia ukurasa wake wa Instagram;

"Kuna limit kwenye uvumilivu. Uvumilivu ni hekima. Uvumilivu unakuandaa kuwa mtu mwema na bora zaidi mbeleni. Uvumilivu wako usionekane kuwa ni ugoigoi ama upuuzi.

Kuna watu wamenijaribu kwa muda mrefu sana. Kwa kweli sasa wamefanikiwa kunifikisha ukomo wa uvumilivu wangu, naogopa uongo usijegeuka ukweli. Nafahamu watu wema, wachapakazi, watenda haki, wana mageuzi wamewahi kuumizwa kwa sababu ya uvumilivu wao.

Kuna wakati nilikata tamaa nikataka kujiuzuru uongozi wa Umma lakini nikaja kufikiri upya, hivi ni nani atafanya kazi hizi? Kama watu wema wanaopigwa fitna na majungu wakisusa na kuacha kazi za Umma za kujenga nchi? Ni nani atakayefanya? Siyo itakuwa ni kukubali uongo ushinde ukweli?

Ukiwa Waziri wa Maliasili na Utalii ukakuza idadi ya Watalii kwa kasi, ukaongeza mchango wa sekta yako kwenye pato la Taifa, ukadhibiti ujangili, ukaufanya utalii ikawa kitu ‘fashionable’, ukazuia ubadhirifu/rushwa/matumizi mabaya ya ofisi/uzembe, badala ya kupendwa na kuungwa mkono watu wanakushambulia.

Ukijiuzuru unakuwa umewapa raha na ruhusa ya kuendelea na mambo yao. Kuna watu mfano wananiandika kila siku kwenye gazeti lao, najua wanatumwa kwa kulipwa, wanaandika vitu vya kipuuzi visivyo na ushahidi wala substance, lengo ni kuchafua tu. Na hii ni dalili kwamba hawana cha maana cha kutumia kunichafua ili malengo yao yatimie, wangekuwa nacho ningeomba dunia isimame nishuke!

Kwa kuwa wao na washirika wao wamenifikisha ukomo wa uvumilivu wangu, nimewapeleka Mahakamani, Mahakama itaamua. Washirika wao wamewadanganya kwa rushwa, sasa wakawape ushahidi huko Mahakamani, nitawafilisi kuanzia Kampuni hadi wao binafsi.

Anayewapa taarifa za uongo naye tumemjua. Aliwahi kusema nilipopata ajali kuwa ‘bora ningekufa’ tu. Nilimjua na kumsamehe. Amejiunga wengine wawili, wananishughulikia. Hawa nitawashughulikia kwa namna yangu.

Waliwahi kupanga mbinu za kunidhuru, pengine kuniua. Mungu akanisalimisha. Walishindwa kuniua wakati ule, hawatoweza kuniangusha leo. Naingia vitani kwa silaha zote.

Usiombe kunifikisha hapa. I am the worst enemy you can shop around! Twende kazi sasa.

Kiasili, mimi ni mtoto wa kwanza wa mtoto wa kwanza wa babu yangu, ambaye alikuwa Mtemi/Chifu. Kwa mila zetu, mimi ni Mtemi/Chifu. Mababu zangu hawakupewa utemi, walichukua kwa kupigania. Hivyo, vita ni asili yangu. Kushinda ni asili yangu.

Mimi hupigana vita bila kujali nani atadhurika, iwe mimi ama adui ama collateral yeyote yule, sawa tu. Huwa sijali matokeo ya vita. Aliyenitia kidole jichoni sasa akae sawa. Naanza kujibu mashambulizi.

Aliyetaka vita sasa ameipata! Sijawahi kuwa dhaifu wala mnyonge. Sijawahi kukubali kuonewa, kukandamizwa wala kunyanyaswa maishani mwangu. Huwa napigania haki na heshima yangu. Huyu ndiye mimi.

Hizi nyingine ni tabia tu nilifundishwa na walimwengu na ulimwengu. Asonijua basi afuatilie historia yangu. Twende kazi!"
 
Wanaccm hawaachiani maji mezani - Kikwete .

Watu wameanza kufukua makaburi _joy__joy__joy_ kosa la  @hamisi_kigwangalla amewaambia wa ( 62...jpg


Kigwangwala nenda wizara ya afya kawaombe radhi wale wazee uliokuwa unawafungia geti saa 10 alfajiri waonekane wamechelewa ili upate kiki , lingine ni hili kafagie kaburi la babaako akakusamehe (unalijua hili vizuri )
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom