Waziri Kigwangalla naomba uzuie Nyumbu wa Tanzania kuingia Kenya

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,585
3,179
download-2.jpg
Mheshimiwa Kigwangala,ni matumaini yangu kuwa hujambo na nimgependa kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa spidi na kasi uliyoanza nayo katika harakati zako za kuhakikisha hufukuzwi kutoka ofisi za wizara ya maliasili kama wenzako wengi walivyo fanywa.

Bila kupoteza muda ningependa kukushauri tafadhari sana piga marufuku nyumbu wa Tanzania kuhamia nchini Kenya kila inapofika mwezi Julai ya kila mwaka, na kukaa huko hadi October wanapoanza kurejea nchini Tanzania.

Hatua hii mheshimiwa itatufanya kubaki na nyumbu wetu hapa nchini kwa kipindi cha mwaka mzima, hivyo kusaidia ongezeko la watalii nchini. Zaidi ya hapo kwa kuwa nyumbu wetu wamezoea ziara za kitalii kila mwaka nchini kenya, basi isiwe tabu tutatengeneza mzunguko wa ndani kwa ndani kwani robo ya tanzania ni poli la serengeti na ngorongoro, hata wakitembelea maeneo ya Robo hadi ngorongoro kisha wanarejea magharibi hadi ziwa victoria sawa kabisa mzunguko utakuwa umekamilika mheshimiwa, na hapo tayari wakenya watakuwa wameula wa chuya.

Lakini pia tutazuia magonjwa ya wanyama wa Kenya kuvuka mpaka na kuja Tanzania,Mpaka hapo nadhani nitakuwa nimepiga pointi makofi tafadhari.
Najua unaweza kuukataa ushauri wangu kwa kisingizio cha kuwa hilo ni tendo la asili halizuiliki, lakini kama ndio hivyo naomba ukae chini ufikiri mara mbilimbili kuhusu wakurya na wamasai na kwa makabila ya mipakani kwa ujumla wake.

Makabila ya wafugaji wa kimasai na wakurya mifugo yetu haijui mipaka kama walivyo nyumbu,mipaka hii ni kwa binadamu,hebu jaribu kupunguza jaziba lifanyie uchunguzi wa kina hili jambo mifugo wa watanzania wameokoka mara nyingi na ukame kwa kwenda uhamishoni nchini Kenya hali kadharika na wakenya hivyo hivyo kuna immigration kama ya nyumbu hapa, acha kushupaza shingo,hakuna sherehe kubwa tulifanya kama ya Magembe kutemeshwa mzigo,sisi wafugaji huwa tunamlilia Mungu atusaidie na viongozi vipofu na ndio maana tunaamini huwa hamdumu kwenye hizo wizara.

Hebu kaeni chini zungumuzeni kati yenu na ndugu zenu wakenya,tatueni hizi shida ndogondogo,kitendo chako kutaifisha ng'ombe wa wakenya sio cha kiungwana umekosema sisi ni ndugu tunawategemea nasi wanatutegemea, lakini kama unadhani unajitosheleza

Wazuie na nyumbu wa serengeti wasiende masai mara nchini Kenya.
 
Nafikiri tutahitaji ukuta kama ule ambao utajengwa Mirerani ili kupunguza wizi Wa Tanzanite!
 
Tufanye yaliyo ndani ya uwezo wetu mengine tuayaache, maana huku kutakuwa kuingilia uhuru wa wanyama.
 
Back
Top Bottom