Waziri Khatib akana kuwa na nyaraka kuhusu Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Khatib akana kuwa na nyaraka kuhusu Muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Oct 14, 2009.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mohammed Seif Khatib amesema hana ushahidi wa nyaraka yoyote ya Mkataba wa Muungano kati ya iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Watu wa Tanganyika, inayoonyesha kusainiwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume au kiongozi yoyote wa Baraza la Mapinduzi ambalo, liliridhia mkataba huo.

  Kauli hiyo, ya Waziri Khatib imekuja wakati kukiwa na mjadala mkubwa kuhusu suala la muungano kati ya Jamhuri hizo mbili, uliosababisha kuzaliwa kwa Jamhuri moja ya Muungano wa Tanzania.

  Suala la Muungano kati ya Jamhuri hizo, mbili limezua mjadala mkubwa katika siku za karibuni hasa baada ya kuzuka fununu za kuwepo kwa mafuta na gesi asilia katika visiwa vya Zanzibar na kutangazwa kuwa mali hiyo ni katika orodha ya mambo ya muungano.

  Jambo hilo, lilisababisha baadhi ya viongozi na wananchi wa Zanzibar kupinga kwa nguvu zote rasilimali hiyo, kuingizwa ndani ya mambo ya muungano huku baadhi yao wakisema wako tayari hata kuvunja muungano.

  Mjadala huo, pia uliibua hoja ya kwamba muungano kati ya jamhuri hizo, si halali kwa sababu hauna misingi ya kikatiba na keshiria wala ridhaa ya wazanzibari kwa kutokuwapo saini za viongozi wao katika mkataba wa muungano.

  Akizungumza na Mwananchi mjini hapa juzi, Wazir Khatibu alisema hana nyaraka yoyote ya mkataba wa muungano inayoonyesha saini ya Rais wa kwanza wa Zanzibar au kiongozi yeyote wa Baraza la Mapinduzi kuridhia mkataba huo.

  "Mimi nafahamu ushahidi wa aina mbili unaonyesha uhalali wa muungano kati jamhuri ya watu wa Zanzibar na watu wa Tanganyika. Moja ni picha waliyopiga Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Karume wakati wakitia saini mkataba huo.

  "Lakini pia nina ushahidi wa picha ambayo viongozi hao walipiga wakati wa kukabidhiana nyaraka za mkataba huo baada ya kusainiwa na walikuwa wameshikana mikono," alisema Waziri Khatib.

  Baada ya waziri Khatibu kutoa ushahidi huo, mwandishi wa habari hii alimuuliza waziri huyo ambaye pia ni mjumbe wa kamati maalum ya serikali ya kushughulikia kero za muungano kama ana nyaraka yoyote ya mkataba wa muungano, inayoonyesha saini ya Mzee Karume au kiongozi mwingine wa baraza la Mapinduzi.

  "Ahh kwanza nsubiri nimalize kwanza, nyaraka ya namna hiyo, sina lakini nafahamu hizo aina mbili za ushahidi kwa maana picha waliyopiga wakati wakisaini na nyingine waliyopiga wakikabidhiana au kubadilishana nyaraka hizo baada ya kusainiwa," alisema Wazir Khatib.

  Suala la kuwapo kwa picha hizo, limekuwa likipingwa na watu wengi wanaofuatilia historia ya muungano huo, wakidai kuwa picha hizo hazithibitishi kuwa kilichokuwa kikisainiwa au kukabidhiwa ni mkataba wa muungano kweli.

  Mwananchi ilibahatika kupata nyaraka mbili za mkataba wa Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika ambapo moja ilisainiwa na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa na nyingine ikisainiwa na baba wa taifa Mwalimu Nyerere huku katika nyaraka zote kukiwa hakuna saini ya mtu wa upande wa Zanzibar.

  Licha ya kasoro hiyo, waziri Khatibu alizidi kuutetea na kuulinda muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika kuwa ni halali.

  Alisema kama kuna watu hawaridhiki na uhalali wa muungano huo, waende mahakamani kuishitaki serikali.

  "Muungano kati ya zanzibar na Tanganyika ni halali, lakini kama kuna watu hawaridhiki na uhalali wa muungano huu, basi waende mahakamani na kama wakishindwa katika mahakama za binadamu waende hata katika mahakama ya Mwenyezi Mungu," alisema Wazir Khatibu.

  Wakati huohuo, waziri Khatib alikataa kuzungumzia taarifa zilizosambaa visiwani hapa kwamba ana nia ya kujitupa katika kinyang’anyiro cha urais wa Zanzibar mwaka 2010, akisema muda wake bado.

  "Hilo la kuhusu urais muda wake bado ukifika nitaweka wazi kama ni kweli au si kweli," alisema Waziri Khatibu.

  Baadhi ya watu ambao wanasemwa kuwa wana nia ya kumrithi rais anayemaliza muda wake visiwani Zanzibar ni pamoja na Waziri Mohammed Seif Khatib, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na mototo wa rais mstaafu wa awamu ya pili Dk Hussein Mwinyi, Waziri Kiongozi mstaafu wa SMZ Dk Mohammed Gharib Bilal na Balozi Ally Karume.

  This is very strange and funny kama hakuna mkataba au makubaliano yeyote ya muungano zaidi ya picha sasa ina maana hakuna muungano wa zanzibar na tanganyika.

  Nataka kucheka huku nikilia mie nadhani wazanzibar wanakaliwa kimabavu kama hakuna kitu kama hicho sidhani kama kuna muungano wowote. Picha si kigezo cha muungano.
   
 2. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mwandishi mbona unatutisha? Eti ipo document ilisainiwa na upande mmoja tu? Sawa tuwasikie wasomi.
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hii imekaaje maana kama walisaini jamaa Tanzania Bara watuambie nini hasa kinachowafanya wawangang'anie wazanzibari. Jamaa wanasema sie bara ndio tunarudisha maendeleo zanzibar sasa huu ni ukoloni mamboleo
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  What is the problem here? Ni kama mtu baada ya miaka 45 ya ndoa anaanza kuuliza juu ya cheti cha ndoa wakati matunda ya ndoa hiyo yako wazi. Kuna watoto waliozaliwa na kuna wajukuu. Sasa cheti cha nini baada ya miaka yote hii?
   
 5. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 784
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 80
  UKO SAWA kwa mantiki hiyo wala hujakosea, lakini tatizo ni kwamba mke aliyeolewa anaamini alichukuliwa bila hiyari yake yaani alikuwa hajui kinachoendelea, alikuwa hajui nini maana ya ndoa japo kavumilia kuishi kwenye hiyo ndoa..kinachomuuna ni kwambwa alilaghaiwa na kwa kuwa alikuwa hana akili na upeo akaingia mkenge kwa kuona'mbona mwenzangu tuu'
  Ndivyo ilivyoitokea zanzibar, ukweli mwalimu alikubaliana na wazo la nkuruma la Afrika kuungana na kuwa moja ila alitaka isianze kwa ghafla bali kwa kuanza na regions alitaka kui- protect Zanzbar kama kiinchi kidogo, alitaka nchi zote ziwe huru.Tunapoyaangalia mapinduzi ya zanzibar unafikiri nani hasa wazanzbar walimpindua?au tuseme walijipindua wenyewe, Karume kwa kutaka madaraka na kwa kuwa alikuwa ameshindwa uchaguzi, na baada ya mwingereza kuwaachia madaraka wapemba waliokuwa akiongoza kwenye ZPPP iliyoshinda(kama zijakosea), ilikuwa rahisi kwake kuingia huo mkenge wa muungano kwani alisaidiwa na Nyerere kuwatoa wapemba wa ZPPP.
  Kingine inasemekana Karume alikuwa hajui kiingereza, hivyo nyerere kwa kutumia kigezo cha kumsaidia kwenye mapinduzi yale batili na kwa kutumia kigezo cha kutoelewa kiingereza alitua na ndege zanzibar akiwa na spika na jaji nafikiri huku karume hana shahidi hata mmoja na kusaini kitu ambacho yy karume alikuwa hakijui maana yake.
   
 6. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ama kweli! Una maana kuwa huenda aliweka dole gumba kwahiyo mzee wakamshauri sahihi yake isionekane pale nini?
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwanza ningependa kujua ni Wazanzibari wangapi wanaoyaona mapinduzi ya 1964 kuwa batili ndipo tuendelee na mjadala. Maana siku moja kwenye mgahawa ilikuwa patashika shati chanika mmoja alipoibuka na kupinga hayo mapinduzi.
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Swala Muungano hili mbona linajirudia rudia sana ?Kwani wanataka nini hawa jamaa ?
   
 9. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni source ya muungano wenyewe ndio kikwazo cha zanzibar. Kama pangelitumika referendum wananchi wote wakakubaliana nayo then tusingelikuwa na haya malalamiko but ni mtu mmoja tu aliyeaamua na alikuwa akiogopa asije kupinduliwa ndio maana akawa anafanya kimya kimya akijua wananchi watakuja kumpinga.

  Isitoshe wazanzibar wamekuwa wakitulalamikia wabongo kuwa tunawanyonya sasa mie kimtazamo wangu ni kwamba ifanyike mchakato ikiwa wengi hawataki muungano basi tuwaachie visiwa vyao na sio kuwang'ang'ania kama wakoloni
   
 10. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Jana tu tumetimiza mika 10 tangu Mwl Nyerere atututoke.

  Swali amabalo huwa najiuliza ni hili Hivi hawa viongozi wetu huwa wanasikiliza Hotuba za Mwalimu hasa kuhusu Muungano, Rushwa, Udini na Ukabila.........ukianza kula nyama ya Mtu basi umekwisha kwani hutakaa uache kuila......

  Haya yaliongelewa na Mwl Nyerere 15yrs back na sasa yanatokea lakini kusikia hatusikii, kuona hatuoni....Kama si laana nin nini?
   
Loading...