Waziri kawambwa ofisi umeichoka - TRL wafanyakazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri kawambwa ofisi umeichoka - TRL wafanyakazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 16, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,414
  Likes Received: 5,686
  Trophy Points: 280
  WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wamepinga kauli ya Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, kwamba kampuni hiyo inaendesha shughuli zake vizuri.
  Wamesema kauli hiyo ya Dk. Kawambwa iliyotolewa katika vyombo vya habari hivi karibuni, ina kasoro kwa sababu TRL inakabiliwa na matatizo mengi na kasoro nyingi za kiuendeshaji na kiutendaji.
  Kauli ya wafanyakazi imetolewa ikiwa ni siku chache baada ya Dk. Kawambwa kuwasilisha hotuba bajeti ya wizara yake, alipotoa ufafanuzi kwa wabunge waliochangia kuwa kampuni hiyo haina matatizo makubwa, bali madogo madogo ya kiufundi.
  Akitoa tamko la wafanyakazi wa TRL, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), Sylvester Rwegasira, alisema maelezo yaliyotolewa na Dk. Kawambwa yana kasoro nyingi na kwamba hali ya kiuendeshaji na kiutendaji katika shirika hilo ni mbaya sana.
  Alisema hoja zilizotolewa na wabunge wengi walioshangazwa na uchakavu wa injini za treni za abiria pamoja na kuishiwa mafuta njiani, ni za kweli na kwamba kampuni hiyo inakabiliwa na madeni makubwa ambayo haina uwezo wa kuyalipa.
  Akizungumzia uwezo wa kusafirisha mizigo na abiria ambao waziri alisema ni wa wastani, alisema uwezo wa TRL ni mdogo ikilinganishwa na TRC, kwani katika kipindi cha miaka 10, kati ya 1998 na Septemba 2007, TRC ilisafirisha wastani wa tani milioni 1.1 wakati TRL ilisafirisha tani laki 4.5.
  Alisema upungufu huo pia unaonekana zaidi katika mapato na matumizi ambako kwa mwezi ni sh bilioni 3.4 zinazokusanywa, lakini matumizi ni zaidi ya bilioni 4.5 na zaidi ya bilioni 1 hurudi India kwa ajili ya malipo ya injini, mabehewa na manejimenti iliyokodishwa kutoka nchini humo.
  Rwegasira alisema hadi sasa mwekezaji huyo (Kampuni ya RITES kutoka India) ana deni la zaidi ya sh bilioni 25 na kuongeza kuwa wafanyakazi wana wasiwasi kuwa huenda mzigo wa deni hilo ukabebeshwa serikali.
  Kuhusu menejimenti, alisema haina kanuni wala taratibu za uthibiti wa mapato na matumizi ya fedha, kwa kuwa mkaguzi wa ndani wa fedha haruhusiwi kukagua matumizi, sipokuwa mapato pekee.
  Aliongeza kuwa mkataba wa ukodishaji injini na mabehewa ya abiria kutoka India, unaotumia mamilioni ya shilingi, unaongeza gharama zisizo na maslahi kwa kampuni na serikali kwa jumla.
  Mwaka 2007 serikali ilitiliana mkataba wa kukodisha lililokuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Kampuni ya RITES kutoka India, ambako katika makubaliano yao selikali ilichukua asilimia 49 na mwekezaji kuchukua asilimia 51 na kuitwa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).   
Loading...