Waziri Kawambwa ashindwa kujieleza juu ya Mgomo wa Walimu

Kwa propaganda kama hizi, walianza kupandikiza hasira na chuki kwa madaktari, sasa wamekuja kwa walimu na wanafunzi, wanaendelea tena kwa wafanyakazi wote kupitia mifuko ya hifadhi ya kijamii (SSRA). Watakapowafikia wakulima basi ujue nchi haita tawalika tena.

Unataka WAKULIMA wawafikie mara ngapi?

Soma habari bodi ya Korosho jinsi akina Anna Abdallah, Mudhihir Mudhihir na Mkewe, Jerome Bwanausi wanavyokula bila kunawa!

Soma madudu yaliyopo Bodi ya Pamba uone UFISADI wa kutisha? Msimu huu Pamba inaunzwa kwa Tsh 600/- @Kg Wakulima wamegoma kuuza pamba yao. Je, unataka WAKULIMA wanyonywe vipi ndiyo utambue?
 
Kwa kweli jamaa nilimuona jana kwenye press conference, naona kama ana tatizo la kuongea kwenye public..alishindwa kuongea kabisa.. yaani kama kuna kitu kinamzuia kuongea sawa sawa.
inawezekana ni mcha mungu sana anaogopa kusema uongo ni dhmbi pia anaogopa kusema ukweli ataharibu kazi yake hivyo anajikanyaga tu cha kusema
 
Hii wizara sio saizi yake.

Mkirua, Dk Kawambwa si mwanasiasa kabisa, angalia Wizara zote alopita, ameacha legacy gani? Bila shaka ndiye Waziri aliyebailishwa kwenye Wizara nyingi zaidi ktk utawala wa JK.
Nadhani Jk anamvuta tu maana nasikia ni mpwa wake.
 
Bado ninaendelea kushangazwa sana na aina ya Viongozi tulionao Tanzania. Jana Naibu Spika alikataa Mgomo wa Walimu usijadiliwe Bungeni kwa sababu eti Upo Mahakamani. Leo hii Waziri wa Elimu, Mh. Shukuru Kawambwa katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, ndio topic aliyokuwa anaizungumzia.

Amekwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba kuna rafiki yake wa Temeke alimpigia simu kumtaka aje awaone wanafunzi wa shule ya Msingi wakishuka kwenye Madaladala kuelekea ofisi za Afisa elimu! Eti Wanafunzi hawa wamepata wapi pesa za kuweza kupanda daladala kwenda kupeleka madai yao?

Hapa Anataka kutuaminisha kwamba kuna Chama cha Siasa ( na si kingine kwa mawazo yao ni CDM) kipo nyuma ya mgomo huu wa Walimu na Wanafunzi.

Swali:
Kama kweli Chadema kina nguvu kiasi hicho au kinakubalika kiasi hicho mpaka kuweza kuwashawishi Madaktari kwanza na sasa Walimu na wakakubali kugoma, basi ni kwanini hawa wasiokubaliwa wasiwapishe wanaosikilizwa na wananchi ili wawaongoze?

Je ni mpaka lini hawa viongozi wa Magamba wataendelea kuudanganya Umma kuhusu matatizo halisi yanayosababisha migomo ya wafanyakazi badala ya kukaa na kuyatatua badala ya kuendekeza kupiga siasa?
 
Huyu Waziri kila wizara anayopewa mambo yanamshinda, asaidiwe kuacha uwaziri akawatumikie wapiga kura wake.
 
kaka hapo kweli mie huwa unaingia tarehe 26 net,bila kuchelewa lakin hapa cjajua kwanin wamenicheleweshea mpaka tarehe hii. Serikali imefulia jaman. Hakika jaman
Si ndo maana imeamua kutumia pesa za wafanyakazi kwenye social security funds na kuzuia fao la kujiondoa eti mpaka ufikishe miaka 55.

 
Huyo kawambwa ni kilaza tu,ndiyo maana wantuibia ili tusiweze hata kupanda daladala mpka watu pesa wao,sasa imekula kwao,wao pia wanaamini chadema ndio mbadala wa mambo yote kwa mstakabali wa watz.
 
Kama kuna waziri incompetent kabisa ni Kawambwa, lakini ni unajua ni wa kwetu Bagamoyo?

Kule kwao wakina Ntamaholo na Nyakageni wanasema wachu-wachu. Yaani huyu ni wa kwetu.
Na ndio maana tuko hapa na itatuchukua muda mrefu sana kujiondoa hapa.
 
inawezekana ni mcha mungu sana anaogopa kusema uongo ni dhmbi pia anaogopa kusema ukweli ataharibu kazi yake hivyo anajikanyaga tu cha kusema

nimeelewa kinachomsumbua jamaa si mwanasiasa, sasa ukishakuwa engineer na kudanganya danganya mbali mbali... ndio tatizo. Yaani si muongeaji kama akina Shibuda.
 
Uwezo wa akili yake ni mb 100 na wizara alopewa inabidi uwe makini na kichwa chako kisiwe cha kuegesha, huyu mshkaji ni kilazaa anaongoza watu makini, je tutarajie nini. Alichotakiwa kusema ni kuwaomba walimu warudi tena kwenye meza ya makubaliano sio kuleta visingizio visinyo na maana.
 
inawezekana ni mcha mungu sana anaogopa kusema uongo ni dhmbi pia anaogopa kusema ukweli ataharibu kazi yake hivyo anajikanyaga tu cha kusema

Kusema kweli ni mtu wa watu, hana makuu na hajui kudanganya hivyo anapewa peach ya kusema ndo maana anababaika.
Mwanakwetu uongo, siasa na uongozi waachie wenyewe. wewe ni mtu safi tafuta chuo ufundishe! good luck.
 
nimeelewa kinachomsumbua jamaa si mwanasiasa, sasa ukishakuwa engineer na kudanganya danganya mbali mbali... ndio tatizo. Yaani si muongeaji kama akina Shibuda.

Kusema kweli ni mtu wa watu, hana makuu na hajui kudanganya hivyo anapewa peach ya kusema ndo maana anababaika.
Mwanakwetu uongo, siasa na uongozi waachie wenyewe. wewe ni mtu safi tafuta chuo ufundishe! good luck.
sasa afanyanje wakuu
 
Huyu mtu hajielewi kama hata binadamu au ni kuku, yaani haelewi chochote kinachoendelea hapa duniani
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom