Waziri kawambwa akwaa kisiki udsm---mgomo unaendelea

MASAMBI

Member
Feb 4, 2011
19
3
Baada ya kukawia kufika chuoni leo kama alivyo ahidi angfika saa 5,amefika saa sita na saa saba akaelekea viwanja vya chuo kikuu kutimiza ahadi ya kuja kuwasikiliza wanafunzi,waziri leo amejiondokea chini ya ulinzi wa polisi na usalama wa taifa baada ya kushindwa kujibu hoja za wanafunzi akitoa majibu mepesi huku akizomewa muda wote. Ameambulia walichokipanda ccm kujaribu kuingiza siasa ktk maisha ya watu hasa sekta mama ya elimu. Baada ya kuondoka chuoni muda dakika tano nyuma vijaa wa said mwema wakapinga mabomu ya machozi na risasa bandia lakini solidaruty la vijana bado linaendelea.kuna kila dalili chuo kufungwa, amani iko nusunusu hakuna mwanafunzi kutoka nje hasa wale wa mabibo......tutazidi kujulishana
 
Mkuu huna baadhi baadhi ya maswali na majibu ya Mheshimiwa katika mkutano huo?
 
Nimejikuta napayuka soledarityyyyyy! mzuka ushanipanda.
Vijana gomeni mpaka kieleweke.
 
waliwapuuza october. wakaona hoja za wasomi ni nyepesi na za kipuuz. acha na wao wapuuzwe kwa hoja na majibu yao mepesi
 
Mfano, aliambiwa kuwa hela ya kujikimu imekwisha, hivyo wana UDSM wanataka sh laki moja ya dharura ili semester iishe. Akadai wanafunzi ni elfu 98, hakuna pesa za ghafla za kuwapa wote. Akaulizwa za Dowanz zingetoka wapi ghafla ile, akasema tusilete siasa... Na ****in shit zingine kibao tu!
 
Shukuru Kawambwa hana uwezo wa kuongoza wizara yeyote ile, popote atakapopelekwa atakuwa ni mzigo tu!! Kuna wabunge wengi wenye uwezo lakini Jakaya bado anamshikilia huyu jamaa; kisa sababu ya kutoka wote Bagamoyo!! The guy is a non-performer period.
 
Amepata fundisho na viongozi wengine wajifunze kwamba watu wanapokuwa na serious issue viongozi wetu wasiwe na majibu mepesimepesi.
 
duh,kawambwa kweli leo kawambwika nimemnukuu wakati anaanza hotuba eti hajui alichoitiwa pale chuo,kweli matope kichwani
 
Endeleeni kutujuza what is happeng there kumbukeni waliwatosa oct na nyie msiwe wepesi kukubali porojo its time to make change
 
Mfano, aliambiwa kuwa hela ya kujikimu imekwisha, hivyo wana UDSM wanataka sh laki moja ya dharura ili semester iishe. Akadai wanafunzi ni elfu 98, hakuna pesa za ghafla za kuwapa wote. Akaulizwa za Dowanz zingetoka wapi ghafla ile, akasema tusilete siasa... Na ****in shit zingine kibao tu!

Wanafunzi (jobless watarajiwa) elfu 98?! Hapa serikali inatengeneza bomu kubwa. Wataajiriwa na nani?/watajiajiri kivipi hapo TZ? watupa hela yetu (kodi yetu) chooni.
 
Nataka kujua nini kinaendelea leo jumanne hapo mlimani je hali ni shwari au mambo yaleyale.?
 
Madai mengine yaliyotolewa na wanafunzi hao ni kumtaka Waziri huyo wa elimu kutoa tamko la kufuta kesi inayowakabili wanafunzi wenzao waliokamatwa Ijumaa ya wiki iliyopita wakishinikiza Serikali kusikia madai yao.

Akijibu hoja hizo, Dk Kawambwa alisema kuwa Serikali imekwishapokea malalamiko na hoja zao, lakini maombi hayo hayawezi kutekelezeka hadi ipitishwe bajeti ijayo ya Serikali jambo lililowafanya wanafunzi hao kupandisha jazba na kumtaka ashuke kwenye jukwaa aondoke kwa kile walichokieleza kuwa alikuwa akipiga siasa.

Wanafunzi walifikia hatua hiyo baada ya mwanaharakati chuoni hapo, Rich Mwita kusimama na kumweleza waziri kuwa alikuwa hajaeleweka na kumtaka atoe majibu ya mwisho ili wao waweze kuona hatua za kuchukua.

Waziri akawajibu kwa kifupi kuwa kesi zilizoko mahakamani hana uwezo wa kuzifuta sababu ule ni mhimili mwingine, kuhusu ongezeko la Sh 5,000 ili kufikia Sh 10,000 akawaambia Serikali imekubali.

Kuhusu kiwango cha Sh10,000 alisema hadi hazina ifanye ukokotoaji na kuhusu fedha za dharura akasema kiwango hicho ni kikubwa na hakiwezi kupatikana kwa dharura.

Kutokana na kauli hizo, wanafunzi walipandwa na jazba na ndipo walipozidi kupiga kelele za kumtaka ashuke na aondoke katika eneo hilo.

Hata hivyo, wanafunzi hao walimuuliza maswali ambayo Waziri alionekana kuyakwepa kujibu na kuonekana kuwa na hofu kutokana na jazba walizozionesha wanafunzi hao.

Aliposema kuwa suala la malipo ya posho kutoka sh 5000 hadi 10,000 lisubiri bajeti ya mwaka ujao walimuuliza kuwa "Mbona suala la Dowans halikusubiri bajeti sasa iweje suala letu linasubiri bajeti?,"walihoji wanafunzi hao.

Swali lingine aliloulizwa Waziri ni kwamba kipindi cha uchaguzi kuna baadhi ya wafanyakazi waliongezewa mishahara bila kupitisha kwenye bajeti nalo hakulijibu "Unasema mpaka bajeti ipitishe nyongeza hiyo mbona kipindi cha uchaguzi baadhi ya wafanyakazi waliongezewa mishahara fedha zilitoka wapi?," walihoji.

Dk Kawambwa alifunga mkutano huo na kuondoka bila kuafikiana na wanafunzi hao hali hiyo ilileta uvunjifu wa amani kwa kuwa wanafunzi walirusha chupa za maji na mawe na kuwapiga askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).

Wanafunzi watano wazirai
Baada ya kurushiwa mawe na chupa za maji hali ilibadilika chuoni hapo kwani askari walijihami na kurusha mabomu ambapo wanafunzi watano walizirai papo hapo na kubebwa kupelekwa katika zahanati ya chuo hicho bila kujitambua.

Wanafunzi hao walimwambia Waziri kuwa hadi sasa hawana fedha za kumaliza muhula na kumuomba atoe ufafanuzi wa kuweza kuwasaidia hadi kumaliza muhula huku wengine wakisikika wakiongea kwa sauti "Njaa inatuua, tunaomba utunusuru" walisikika wakitoa sauti.

Wakizungumza mbele ya Waziri, wanafunzi hao walisema kuwa hawaendi nyumbani wala chuo hakitafungwa ila wanataka fedha hiyo ipatikane haraka iwezekanavyo vinginevyo waliahidi kujipanga upya na kuhakikisha wanafika Ikulu.

"Tunaongea mbele yako mheshimiwa Waziri kama utaweza kutupa majibu yanayojitosheleza tutajipanga vizuri na kuhakikisha tunafikisha kilio chetu sehemu husika maana unaonekana umeshindwa kutuweka wazi," alisema Rich Mwita mwenyekiti wa wanaharakati.
 
Shukuru Kawambwa hana uwezo wa kuongoza wizara yeyote ile, popote atakapopelekwa atakuwa ni mzigo tu!! Kuna wabunge wengi wenye uwezo lakini Jakaya bado anamshikilia huyu jamaa; kisa sababu ya kutoka wote Bagamoyo!! The guy is a no-performer period.

Hiyu jammaa ninasadikika ni ndugu yake .....!!
 
Ilikuwa nyomi!
02_11_0z82yn.jpg
attachment.php

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwenye viwanja vya chuo hicho wakati wakikitoa malalamiko kuhusu kuongezewa fedha za kujikimu kutoka Sh. 5,000 hadi Sh.10,000. Picha kwa hisani ya HabariLeo
 
Hakuna mtu ambaye anaweza kukubaliana na maamuzi ambayo ni kinyume na matakwa yake. Wanaharakati na wanasiasa wa UDSM wanasema wanataka 100,000/- siyo hata ombi lakini hawajaandika matakwa hayo rasmi kuelezea kuwa ni janga la kitaifa na pia hawaoneshi kuwa kiuhakika hiyo wanayotaka itawatosha kwa muda uliobaki. Lazima vitu vingine viendane na watu wao ni wasomi watoe madai kisomi.

Swala la dowans na mashangingi, unadhani wizara husika inahusiana vipi na hilo? Hayo ni siasa na wanafunzi walimwambia toka mwanzo hawataki siasa.

Swala la majibu mepesi. Naomba kusaidiwa kujua wepesi wa jibu ni upi!! Yaani mnataka atoe jibu kuwa sawa mtapata hiyo hela kisiasa alafu kesho wanasiasa wamwite fisadi? hela siku zote ina utaratibu wa kutoka na hakuna serikali yoyote duniani inaweza kutoa hela kama wasomi hao wanavyolazimisha maana utatengeneza janga la kitaifa siyo kwa vyuo vikuu na wafanyakazi wote tutasema ni janga maana bei ya vitu ni ghali kila pahala.

swala la msingi. Katika mambo ya msingi tuache propaganda za kisiasa tuweke sayansi mbele maana hapa itakua right siasa itumike tu kusukuma sera ikae vyema.

Tuache kuropoka tu eti majibu mepesi, askari wamewpiga mabomu, bila ya kujiuliza kikundi cha wanafunzi kimewapiga askari mawe, kinawachapa wenzao, kinapora mali za watu kwa kingizio cha kuishiwa. Shule za msingi na sekondari hela ya chakula ikiisha shule zinafungwa kwanini wasiombe chuo kifungwe au hayo ni maswali mepesi??? Kuna watu wa kawaida kabisa mtaani kwangu sinza kwa mtogole mtu analipwa 2000 kwa siku kwa mhindi kiwanda cha sabuni na ana familia analipa kodi etc lazima tuwafundishe wanetu kupanga matumizi maana bila hivyo hata boom likipanda hadi 20,000/= njaa itatutafuna tu..... nasilisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom