Waziri Katambi: Vijana ambao hawajapata mikopo ya Halmashauri pengine ni Wakenya

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,192
20220518_114330.jpg

Si kweli kwamba vijana wa nchi hii hupata mikopo bali mikopo yote ihusuyo vijana hugawanwa na Viongozi wa chama tawala na vijana wao nao ni wale tu walio na connection.

Katambi acha dharau na hilo litakukosesha jimbo.

===
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 18, 2022, bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Sophia Mwakagenda, alilohoji kuhusu vijana kutopata ajira kwa zaidi ya miaka 6 sasa pamoja na kwamba mfumo wa utoaji wa mikopo katika Halmashauri kwa vijana mfumo umewatupa nje.

"Sisi kama serikali tunazotakwimu za vijana hawa, na wale wote wanaofanya application za ajira, vyuo vikuu vyote tumekuwa tukipata taarifa, tunao vijana zaidi ya laki mbili wanaoingia kwenye soko la ajira kutoka vyuo mbalimbali, pia tuna mifumo na programu tunazoziandaa ikiwa ni pamoja na internship, kuangaliziwa ajira ndani na nje ya nchi,"amesema Katambia

Aidha Katambi ameongeza kuwa, "Tumekuwa tukiendelea kutoa mikopo na zaidi ya bilioni 150 zimekwishakutolewa kwa vijana mbalimbali, kama kuna vijana ambao wapo labda pengine sio Watanzania ni Wakenya utanisaidia niweze kuwaingiza hapa tuone namna gani tunawasaidia,"
 
View attachment 2229138

Si kweli kwamba vijana wa nchi hii hupata mikopo bali mikopo yote ihusuyo vijana hugawanwa na Viongozi wa chama tawala na vijana wao nao ni wale tu walio na connection.

Katambi acha dharau na hilo litakukosesha jimbo.
Of course alipewa jimbo na yule jini jambazi mkuu! kukiwa na fair game huyu ni mchunga ng'ombe fulani tu!
 
Naibu Waziri-OWM, Vijana, Kazi na Ajira, Patrobas Katambi amesema kwamba, zaidi ya bilioni 150 zimekwishatolewa kwa vijana kama mikopo na kusema kama kuna kijana yeyote ambaye hajapata mkopo itakuwa pengine ni Mkenya.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 18, 2022, bungeni jijini Dodoma

20220518_122529.jpg
 
Weka taarifa vizuri, anamaanisha mikopo ya wanavyuo(boom). Japo ukweli ni kuwa wengi tu hawajapata
 
Vijana katika hili ni vigumu kujitetea kwa kuwa wenyewe hawajulikani ukomo wa umri wao.
Hata hivyo tukubali tu kwa kuwa huku mtaani kuna ambao tunaona wanakopeshwa na Vijana wenzao/vikundi.
 
Back
Top Bottom