Waziri KAPUYA na bendi yake

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,545
837
Hivi huyu waziri ambaye ni AL-HAJI naye ana bendi ya Muziki?
Kapuyadance.jpg

ama kweli usilolijua litakusumbua
 
Sina uhakika kama ana bendi, nijuavyo hiyo picha ilipigwa kwenye hafla moja pale Dom
 
Sina uhakika kama ana bendi, nijuavyo hiyo picha ilipigwa kwenye hafla moja pale Dom

Ndiyo Masatu huyu jamaa ana bendi ila si hii ya pichani . Bendi yake ni Akundo Impact .Kila weekend iko Msasani ndani ya kambi ya jeshi sasa si waziri wa huko labda itaondolewa ama PR njema itabakia sijui .
 
Sina uhakika kama ana bendi, nijuavyo hiyo picha ilipigwa kwenye hafla moja pale Dom

anayo bendi ya muziki huyu Alhaji kapuya inaitwa AKUDO BAND na style yao ya kucheza inaitwa baiskeli..sasa tatizo si kuwa waziri ana bendi la hasha bali swali langu ni je inaruhusiwa kwa AL HAJI kuwa na bendi?
 
Brazameni....HAIFAI DUNIA inatuhangaisha...

ila tukishafika huko inabidi hii thread ipelekwe kule ktk DINI wachambue zaidi...ila kama kuuliza wazir anafaa kuwa na bendi...silijui

Tunamuombea DUA bendi yake IFE arudi kwa yale aloyaendea huko HIJJA-AMeen
 
Sidhani kama kuwa alhaj kuna uhusiano wowote na bendi, kwa mtazamo wangu naona ni poa tuu
 
anayo bendi ya muziki huyu Alhaji kapuya inaitwa AKUDO BAND na style yao ya kucheza inaitwa baiskeli..sasa tatizo si kuwa waziri ana bendi la hasha bali swali langu ni je inaruhusiwa kwa AL HAJI kuwa na bendi?

Jee, umewahi kumsikia Al-Hajaj Yusuf Islam, Al-Haj Jermaine Jackson, nimewataja hao kwani nadhani ni kati ya watu maarufu sana duniani, kuna musicians wengi sana ma Al-Haj na wenye bendi wengi tu ma Al-Haj.

Kuwa na bendi si tatizo isipokuwa bendi yenyewe ina-perform wapi na inaimba nini, ndio ina matter.
 
anayo bendi ya muziki huyu Alhaji kapuya inaitwa AKUDO BAND na style yao ya kucheza inaitwa baiskeli..

Nadhani current style yao inaitwa 'pekecha pekecha' na hawa vijana kwa sasa mambo yao iko juu kuliko Twanga na Ngwasuma, si unajua hizi bendi zinatesa kwa msimu?
 
Nadhani current style yao inaitwa 'pekecha pekecha' na hawa vijana kwa sasa mambo yao iko juu kuliko Twanga na Ngwasuma, si unajua hizi bendi zinatesa kwa msimu?

Mmmmh hii pekecha pekecha ndio ikoje nimetoka kapa hapo...
 
Wacheni chuki. Wangapi wana bendi mbona hamsemi? Ntawashukia mimi nyinyi shauri yenu. Nadhani bora nianze kuwapitua memba wa JF mmoja baada mwingine ndiyo mtajua popobawa maana yake nini. Nikimaliza bungeni next stop ni JF

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

MAPINDUZI DAIMA!!!!!!
 
JF kuna ubaguzi hasa wa diniangalia watu wanavyochangia Kapuya kuwa na bendi. Hairuhusiwi si kapuya (alhaj) bali waislamu wote. eti mtu anachangia anasema unatakiwa upekeche kiuno haijali ni Alhaji, Ustaadh au Hajat mbona hajasema sister, padri au kasisi. mnasema watu waache kashfa za dini lakini wakisema wakristo hamsemi ila waislam wakiamua kujibu inakuwa ugomvi,
acheni udini
 
acheni udini waislamu wakijibu mnapiga kelele, pekecha mauno haijalishi ni Alhaj, Ustaadh au hajat mbona hukusema sister padri au kasisi na ndio kutwa wanaimba ndombolo ya yesu
 
Lakini ndugu zangu sijui maana lap top yangu ilikuwa na tatizo kidogo lakini kama tatizo kama ltakuwa ni kueleza tu kuwa ni bendi ya al haji kapuya sidhani kama hilo ni tatizo wa udini
 
JF ni kutoa uwazi na ukweli, tatizo si kueleza nisemacho mimi ni jinsi watu walivyochangia. haikuishia kwa kapuya na u alhaj wake watu wamefikia hadi kwa ustaadh na hujat hii moja kwa moja ni uukashifu uislam ndio maana nikauliza mbona haikutajwa padri au sister ili watu wajue mchangiaji alikuwa ni kurekebisha umma wote
 
acheni udini waislamu wakijibu mnapiga kelele, pekecha mauno haijalishi ni Alhaj, Ustaadh au hajat mbona hukusema sister padri au kasisi na ndio kutwa wanaimba ndombolo ya yesu
Wewe ndo umejaa udini. Kwa nini ikuume kama si mdini? Umejuwaje kama wazo lake ni hilo?

JF ni kutoa uwazi na ukweli, tatizo si kueleza nisemacho mimi ni jinsi watu walivyochangia. haikuishia kwa kapuya na u alhaj wake watu wamefikia hadi kwa ustaadh na hujat hii moja kwa moja ni uukashifu uislam ndio maana nikauliza mbona haikutajwa padri au sister ili watu wajue mchangiaji alikuwa ni kurekebisha umma wote
Peleka mada hii kwenye dini/imani huko utapata majibu yako. Hapa kinachozungumziwa ni Vibweka vya Wakubwa.
 
Iko poa tu... binadamu na muziki tangu enzi hizo haina noma wala nini afterall sidhani kama ina-interfer na kazi yake.. Ni kama Berlusconi huko Italy na soka. ... Tulieni..
 
Back
Top Bottom