johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,744
- 141,609
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi a mawasiliano ameitaka mamlaka ya udhibiti usafiri wa ardhini ( Latra) kukutana mara moja na kutoa mwongozo juu ya idadi ya abiria wanaoruhusiwa kusimama ndani ya daladala na Mwendo kasi ili kupunguza msongamano.
Waziri Kamwele ameyasema hayo mjini Dodoma alipokuwa anaelezea hatua zinazochukuliwa na wizara yake ili kujikinga na virusi vya korona.
Chanzo: ITV habari
-----
March 18, 2020
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Eng. Isack Kamwelwe atoa tamko kufuatia Coronavirus Covid-19.
Tamko hilo la Waziri Isack Kamwelwe linahusu sekta ya usafiri wa barabara, reli, anga na majini linataka wenye vyombo vya usafiri na watumiaji kuchukua tahadhari kubwa kufuatia ugonjwa huo kufuatia tangazo la Wizara ya Afya kuthibitisha ugonjwa huo upo Tanzania.
Source: Global TV online

- Kampuni za usafiri wafungue vituo zaidi vya kukatia tiketi nje ya vituo vikuu vya usafiri.
- Tiketi za kieletroniki ziamzishwe kupunguza msongamano.
- Wafanyakazi na abiri watumie sanitizier mara kwa mara kusafisha viganja vyao washikapo nauli, chenji, kushika viti n.k
- LATRA, TBS, na wizara ndani ya siku tatu waamue ni idadi gani ya abiria wawemo katika chombo cha usafiri ili kupunguza uwezekano wa maambukizi.
- TAZARA na TRC wahakikishe vifaa vya kusafisha mikono viwepo stesheni na katika treni.
- Mamlaka za usimamizi wa bandari na zile za viwanja vya ndege kwahakikishe kuwapo na vifaa vya kusafisha mikono n.k katika maeneo yao.
- Taasisi zote za usafiri zishirikiane na wizara ya Afya ili kuweza kuchapisha na kubandika matangazo yenye habari sahihi juu ya namna ya kuwa safi na pia kuzuia kusambaa ugonjwa wa Covid19 Coronavirus.
Source: Global TV online