moe junior
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 894
- 853
Salaam! Nikiwa Ni mmoja wa wahanga wa kusotea huduma ya umeme katika halmashauri ya manispaa IRINGA kata ya IGUMBILO, Ni wazi kwamba Meneja wa TANESCO kazi imemshinda. Mteja analipia huduma, TANESCO wanakuja kukagua na kutoa control namba ya kulipia lakini baada ya kuwapa pesa tu mteja atasubiri kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu unless ukawa na mkono mrefu.
Ntatoa mfano, Mimi Nyumba yangu ipo Mita chache sanna kutoka katika nguzo ya umeme kiasi ambacho huhitaji kuwa na nguzo ya ziada lakini Ni mwezi wa pili TANESCO hawajaunganisha Umeme na ukiwauliza majibu yao ni kwamba Kuna matatizo katika mfumo. Mfumo upi? Hawana majibu.
Waziri wa Nishati Msaidie huyu Meneja, kazi imemuelemea. Hii sio hisani ni haki ya mteja baada ya kukamilisha malipo na taratibu nyingine. Huyu meneja anakutukanisha na Wananchi huku.