Waziri Kalemani: Mgao wa umeme uishe, matengenezo yakamilike

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
18,512
68,129
Waziri amenukuliwa akisema;

"Matengenezo yakamilike, sitaki kuona kuna mgao wa umeme, matengenezo yakamilike hali ya umeme irejee kama kawaida"

Pia soma >TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

122.jpg

Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani ameagiza kuwa, matengenezo ya mitambo mbalimbali ya kufua umeme nchini yakamilike ndani ya siku Tano ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika.

Dkt. Kalemani ametoa agizo hilo tarehe 2 Machi, 2021 mkoani Dar es Salaam, mbele ya Bodi na Menejimenti za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Songas, baada ya kukagua kituo cha umeme cha Songas ambacho mitambo yake miwili inafanyiwa matengenezo na hivyo kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 115 badala ya 180.

Akiwa ameambatana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja, Waziri Kalemani amesema kuwa, hataki kusikia wananchi wakilalamika kukosa umeme kwa sababu tu ya matengenezo ya mitambo, hivyo matengenezo hayo yakamilike ndani ya siku alizoagiza au kwa siku chache zaidi.

Aidha, kuhusu muda wa kufanya matengenezo ya mitambo ya umeme nchini, Dkt. Kalemani ameiagiza TANESCO na Songas kupishanisha muda wa matengenezo ili kutoathiri hali ya upatikanaji wa umeme nchini.

Vilevile, Dkt.Kalemani alisisitiza kuhusu utekelezaji wa agizo alilolitoa kwa TPDC la kuhakikisha kuwa vifaa mbalimbali vinavyotumika kwenye miundombinu ya gesi nchini kama vile valvu na mabomba vinatengenezwa nchini ili kurahisisha upatikanaji wa vifaa husika.

Vilevile, amesema kuwa, Wizara ya Nishati haitaacha kufuatilia kwa karibu utendaji kazi wa Taasisi zilizo chini yake kwani lengo ni kuhakikisha kuwa Taasisi hizo zinafanya kazi kwa ufanisi na wananchi wanapata huduma wanazostahili.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Songas, Anael Samuel, alimueleza Waziri wa Nishati kuwa, matengenezo ya mitambo miwili ya umeme kwenye kituo hicho, yanaenda sambamba na matengenezo katika bomba la Gesi kutoka Songosongo linalopeleka gesi kwenye mitambo hiyo ya Songas ili kuzalisha umeme.

Alisema kuwa, kutokana na bomba hilo la gesi kutoka Songosongo kufanyiwa matengenezo, kwa sasa megawati 115 zinzozalishwa kwenye kituo hicho zinatokana na mitambo ya gesi ya Shirika la Maendeleo Tanzania (TPDC).

“Nazipongeza Taasisi za TPDC na TANESCO kwa kushirikiana na Songas kwani tulikaa pamoja kama wadau ili kuona namna tutakavyotatua tatizo hili, na ndiyo maana angalau megawati 115 zinaendelea kuzalishwa kwa kutumia mitambo ya TPDC.” Alisema Samuel

Aidha, alisema kuwa, ukarabati wa mitambo hiyo unafanyika kwa ratiba maalum ili kuweza kutoa uhakika wa mitambo hiyo kuendelea kuzalisha umeme kwa muda mrefu zaidi.

Kwa upande wake, Meneja Mitambo wa Songas, Michael Mngodo alisema kuwa kituo cha umeme cha Songas kina mashine Sita ambapo kwa sasa mashine zinazofanya kazi ni nne na zinazofanyiwa matengenezo ni mashine mbili.

Mpekuzi

My take:

Tanesco walikuwa wanaficha kitu gani kama kuna mgao wa umeme uliosababishwa na upunguaji wa Megawati zinazozalishwa kwa siku kutoka megawati 180 mpaka megawati 115 zinazozalishwa sasa.

Siku nyingine wawe professional kwenye kazi zao, mficha maradhi kifo humuumbua.
 
Isingekuwa aliyemweka hapo kuwa na Undugu nae (wa Kiukoo) kwa haya Mauzauza ya Umeme nchini hivi sasa angeshakuwa ameshatumbuliwa Kitambo ( zamani ) sana tu. Kuna tatizo Kubwa mahala au Jambo fulani haliko sawa pia.
 
Labda na yeye Waziri wamemdanganya
Wenyewe si ndo wanaotambua kila siku, kuwa umeme tunao' wa kumwaga na ziada '.. lakini mambo on the ground ni tofauti. Tupunguze siasa kwenye mambo haya ya msingi...' Action speaks louder than words'.. hakuna haja ya kutuambia mambo ya umeme wa ziada, wananchi tutaona tu ukweli on the ground! Nyie ndo mnamwangusha Mh. Rais kwenye sana yake ya uchumi wa viwanda.
 
Waziri amenukuliwa akisema;

"Matengenezo yakamilike, sitaki kuona kuna mgao wa umeme, matengenezo yakamilike hali ya umeme irejee kama kawaida"

Pia soma >TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani ameagiza kuwa, matengenezo ya mitambo mbalimbali ya kufua umeme nchini yakamilike ndani ya siku Tano ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika.

Dkt. Kalemani ametoa agizo hilo tarehe 2 Machi, 2021 mkoani Dar es Salaam, mbele ya Bodi na Menejimenti za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Songas, baada ya kukagua kituo cha umeme cha Songas ambacho mitambo yake miwili inafanyiwa matengenezo na hivyo kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 115 badala ya 180.

Akiwa ameambatana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja, Waziri Kalemani amesema kuwa, hataki kusikia wananchi wakilalamika kukosa umeme kwa sababu tu ya matengenezo ya mitambo, hivyo matengenezo hayo yakamilike ndani ya siku alizoagiza au kwa siku chache zaidi.

Aidha, kuhusu muda wa kufanya matengenezo ya mitambo ya umeme nchini, Dkt. Kalemani ameiagiza TANESCO na Songas kupishanisha muda wa matengenezo ili kutoathiri hali ya upatikanaji wa umeme nchini.

Vilevile, Dkt.Kalemani alisisitiza kuhusu utekelezaji wa agizo alilolitoa kwa TPDC la kuhakikisha kuwa vifaa mbalimbali vinavyotumika kwenye miundombinu ya gesi nchini kama vile valvu na mabomba vinatengenezwa nchini ili kurahisisha upatikanaji wa vifaa husika.

Vilevile, amesema kuwa, Wizara ya Nishati haitaacha kufuatilia kwa karibu utendaji kazi wa Taasisi zilizo chini yake kwani lengo ni kuhakikisha kuwa Taasisi hizo zinafanya kazi kwa ufanisi na wananchi wanapata huduma wanazostahili.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Songas, Anael Samuel, alimueleza Waziri wa Nishati kuwa, matengenezo ya mitambo miwili ya umeme kwenye kituo hicho, yanaenda sambamba na matengenezo katika bomba la Gesi kutoka Songosongo linalopeleka gesi kwenye mitambo hiyo ya Songas ili kuzalisha umeme.

Alisema kuwa, kutokana na bomba hilo la gesi kutoka Songosongo kufanyiwa matengenezo, kwa sasa megawati 115 zinzozalishwa kwenye kituo hicho zinatokana na mitambo ya gesi ya Shirika la Maendeleo Tanzania (TPDC).

“Nazipongeza Taasisi za TPDC na TANESCO kwa kushirikiana na Songas kwani tulikaa pamoja kama wadau ili kuona namna tutakavyotatua tatizo hili, na ndiyo maana angalau megawati 115 zinaendelea kuzalishwa kwa kutumia mitambo ya TPDC.” Alisema Samuel

Aidha, alisema kuwa, ukarabati wa mitambo hiyo unafanyika kwa ratiba maalum ili kuweza kutoa uhakika wa mitambo hiyo kuendelea kuzalisha umeme kwa muda mrefu zaidi.

Kwa upande wake, Meneja Mitambo wa Songas, Michael Mngodo alisema kuwa kituo cha umeme cha Songas kina mashine Sita ambapo kwa sasa mashine zinazofanya kazi ni nne na zinazofanyiwa matengenezo ni mashine mbili.

Mpekuzi

My take:

Tanesco walikuwa wanaficha kitu gani kama kuna mgao wa umeme uliosababishwa na upunguaji wa Megawati zinazozalishwa kwa siku kutoka megawati 180 mpaka megawati 115 zinazozalishwa sasa.

Siku nyingine wawe professional kwanye kazi zao, mficha maradhi kifo humuumbua.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja,na Naibu waziri wa Maliasili na utalii anaitwa Mary masanja.
 
Isingekuwa aliyemweka hapo kuwa na Undugu nae ( wa Kiukoo ) kwa haya Mauzauza ya Umeme nchini hivi sasa angeshakuwa ameshatumbuliwa Kitambo ( zamani ) sana tu. Kuna tatizo Kubwa mahala au Jambo fulani haliko sawa pia.
Na juzi katuambia umeme upo wa kutosha. Leo ana gombana na TANESCO. Hawa jamaa hutuona sisi ni mazwazwa sana
 
inawezekana kuna baadhi yao wanataka kumuhujumu
kuwa macho sana. safisha takataka
 
Na juzi katuambia umeme upo wa kutosha. Leo ana gombana na TANESCO. Hawa jamaa hutuona sisi ni mazwazwa sana
Alisema Tanzania ina jumla ya Megawatts 1680 ambapo Mahitaji ya Siku ni Megawatts 1604 sasa nashangaa Leo kusikia ( kushuhudia ) Umeme unakatika au una Changamoto yoyote ile ya upatikanaji wake. Binafsi huyu Waziri Kalemani sioni akifanyacho katika hiyo Wizara na hatoshi vile vile hapo. Ana Usanii mwingi, Maneno mengi ila hana Utendaji wa Kivitendo wenye Ufanisi hasa kwa Huduma hii Muhimu ya Nishati nchini.
 
Mwanasheria anamwagiza Mhandisi wa mitambo an umeme matengenezo ya vyanzo vyote vya umeme yafanyiwe ukarabati ndani ya siku tano. Is it realist ou mihemku. Je ilichukua siku tano? Hizi kauli za kisiasa hizi ni hatari.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom