Waziri Kalemani: Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15, 2021. Umeme wa maji ni nafuu kuliko wa vyanzo vingine

Sidhani kama uko sahihi kwenye hili, uranium kama ilivyo haiwezi kukusaidia kuzalisha umeme, itabidi hiyo uranium isafirishe kupelekwa kwenye nchi zinazo chengenua na kutengeneza FUEL RODS, halafu wakuletee utumie kuzalisha umeme. Na dunia kwa jinsi huo mpango wa fuel road uko sensitive, ni nchi chache sana wanaruhusiwa kufanya hivyo. Hapo hapo hujaweka gharama za kujenga mtambo wa umeme wa nuclear pamoja na gharama za maafa kama iliyotokea India, Russia na Japan
Uko sahihi. Hata Muhongo hajawahi kuikazania nyukilia. Anajua. Yeye anahamasisha vyanzo vingine, kubwa gesi
 
Prof Muhongo yupo Bungeni maana siku kadhaa nyuma nilimsikia kwamba umeme wa gesi ndio wa gharama nafuu na wa uhakika ukilinganisha na huu wa kizamani wa maji.
Muhongo hajawahi kusema kuwa umeme wa maji ni ghali au usiendelezwe. Yeye anataka energy mix ya vyanzo vingi vya kisasa, siyo kuweka mategemeo kwenye maji pekee. Kwanza maji hupunguzwa na shughuli-ongezeko za binadamu au ukame.

Kwa sababu hiyo wale wajuaji wa America na Ulaya walishabakisha asilimia ndogo sana, chini ya 10%, ya umeme ambayo inatokana na maji. Ni Norway peke yao ambao umeme wao karibu wote ni wa maji. Energy mix ndio ushauri wa wataalamu kama Muhongo
 
Prof Muhongo si aliapa kuwa hatatoa siri za Baraza la mawaziri
Muhongo ni Mtaalamu wa Madini, siyo Umeme. Anachokisema siyo kwa ajili ya taaluma yake. Hana huo utaalamu.

Enzi akiwa Waziri wa Nishati alizungumzia kutuletea umeme toka Ethiopia, ambao ni wa maji akidai kuwa ni utakuwa wa bei nafuu. Kitendo cha yeye kuusimanga huu mradi inatia wasiwasi sana na nia yake hasa kwenye hii issue.
 
Nchi ya china inatarajiwa kuzindua Bwawa jipya la kuzailisha umeme kwa kutumia maji.

Je kwetu kazi iendelee au isiendelee?

Bwana jipya la kuzalisha umeme wa maji (HEPD) la Nchini China kuzinduliwa July 2021

Ngoja tuwajuwe wachawi wetu...

RIP BABA YETU MPENDWA JPM

Screenshot_20210415-125641_YouTube.jpg
 
Hii ya kujaza bwawa naifananisha na ile hekaya ya kuwa treni ya SGR kipande cha Dar-Moro kitaanza kazi Nov 2019, ila mpaka leo hola. Kuna ile porojo nyingine ya bomba la mafuta toka Uganda litakamilika Dec 2020, mpaka leo ni kusaini mikataba tu!! Usanii mwingine bana
wamesema mwezi wa nane SGR safari za Dar-Moro zinaanza..
 
Nuclear ni cheaper zaidi..
Maji kuna gharama za mazingira kubwa Sana
Kufyeka heka zote zile utasema hakuna gharama?

Amepima loss yake? Kufyeka heka zaidi ya milioni?
Nuclear ki mazingira ni hatari zaidi kwakua effect yake ni generational...Belgium waliufinga mtambo wao wa nuclear miaka 5 iliyopita, Japan pia ili pata hasara kubwa sana.

Umeme cheapest ni maji, hakuna ubishi ila si nchi zote zina comparative and competitive advantage kutokana na kukosa geographical feature zenye kuwezesha miradi kama hiyo.

Norway karibia 100% ni hydropower na wanaiza umeme wao hadi nje ya nchi yao, sweden wanatumia biofuel kugenerate energy...Prof. aliitumia taaluma yake vibaya kulipiza kisasi japo he had a point...Dhamira yake ndiyo inayomhukumu
 
Watu wengi wanaokazania mambo ya gas inatilia shaka sana, pengine wana miradi yao humo ndani binafsi, labda hilo lingechunguzwa kwanza.

Na kisha mkataba wake uwekwe wazi kwani sheria ya sasa inaruhusu hivyo. Kama wapo bold enough na wana dhamira njema waiweke wazi mikataba yote hiyo ya zamani watanzania waone na waamue kipi ni kweli kipi si kweli na kwa faida ya nani
 
Waziri nishati Dkt. Kalemani asema Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15 mwaka huu wa 2021 aeleza gharama za kuzalisha umeme kwa kila chanzo bunge lamshangilia sana.

Asema lengo la Serikali ni kutumia vyanzo vyote ili mradi vilete umeme wa uhakika na wa bei nafuu kwa mwananchi

Asema umeme wa maji ndio wa nafuu kuliko vyanzo vingine vyote

Alizitaja gharama za kuzalisha umeme kwa unit kwa shilingi za kitanzania kwa kila chanzo ni kama ifuatavyo:
  • Maji ni shilingi 36 kwa unit moja
  • Nyuklia ni shilingi 65 kwa unit moja
  • Solar na upepo shilingi 103 kwa unit moja
  • Makaa ya mawe shilingi 118 kwa unit moja
  • Joto Ardhi shilingi 119 hadi 120 kwa unit moja
  • Gas shilingi 147 kwa unit moja
  • Mafuta mazito shilingi 546 kwa unit moja
Hizo bei zimepangwa na EWURA?Tusipotoshe umma kwa propaganda mfu.Wakati wa ujenzi wa bomba la gas toka Mtwara tuliambiwa maneno matamu kuwa tatizo la umeme Tanzania limepata muarobaini wake,CCM hii hii leo wanaanza mradi Mpya wa HydoPower wanatulazimisha tuwaamini tena?
Bomba gas lipo under utilized,hilo hawalijadili wanapigia debe miradi ambayo kufanya ufisadi ni rahisi kuliko kuwekeza kwenye mitambo ya kuzalisha umeme kwa Gas wanasingizia kwamba imechukuliwa na wajanja.Pathetic Minister!
 
Waziri nishati Dkt. Kalemani asema Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15 mwaka huu wa 2021 aeleza gharama za kuzalisha umeme kwa kila chanzo bunge lamshangilia sana.

Asema lengo la Serikali ni kutumia vyanzo vyote ili mradi vilete umeme wa uhakika na wa bei nafuu kwa mwananchi

Asema umeme wa maji ndio wa nafuu kuliko vyanzo vingine vyote

Alizitaja gharama za kuzalisha umeme kwa unit kwa shilingi za kitanzania kwa kila chanzo ni kama ifuatavyo:
  • Maji ni shilingi 36 kwa unit moja
  • Nyuklia ni shilingi 65 kwa unit moja
  • Solar na upepo shilingi 103 kwa unit moja
  • Makaa ya mawe shilingi 118 kwa unit moja
  • Joto Ardhi shilingi 119 hadi 120 kwa unit moja
  • Gas shilingi 147 kwa unit moja
  • Mafuta mazito shilingi 546 kwa unit moja
Bado mwezi na nusu ifike hiyo Novemba.
 
 
Back
Top Bottom