Waziri Kalemani: Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15, 2021. Umeme wa maji ni nafuu kuliko wa vyanzo vingine

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,595
2,000
Waziri nishati Dkt. Kalemani asema Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15 mwaka huu wa 2021 aeleza gharama za kuzalisha umeme kwa kila chanzo bunge lamshangilia sana.

Asema lengo la Serikali ni kutumia vyanzo vyote ili mradi vilete umeme wa uhakika na wa bei nafuu kwa mwananchi

Asema umeme wa maji ndio wa nafuu kuliko vyanzo vingine vyote

Alizitaja gharama za kuzalisha umeme kwa unit kwa shilingi za kitanzania kwa kila chanzo ni kama ifuatavyo:
  • Maji ni shilingi 36 kwa unit moja
  • Nyuklia ni shilingi 65 kwa unit moja
  • Solar na upepo shilingi 103 kwa unit moja
  • Makaa ya mawe shilingi 118 kwa unit moja
  • Joto Ardhi shilingi 119 hadi 120 kwa unit moja
  • Gas shilingi 147 kwa unit moja
  • Mafuta mazito shilingi 546 kwa unit moja
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
5,108
2,000
Kwa nini tusitumie nyuklia , pale Songea ipo ya kutosha au mnaogopa yasije kutokea ya Japan mwaka 2011 , vinu kufumuka , hata hvyo hyo ilikuwa accidentally from tsunami wave shock
 

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
5,961
2,000
So kumbe nyuklia ndo cheaper kuliko hata gas na tuna uranium Tele songea
Sidhani kama uko sahihi kwenye hili, uranium kama ilivyo haiwezi kukusaidia kuzalisha umeme, itabidi hiyo uranium isafirishe kupelekwa kwenye nchi zinazo chengenua na kutengeneza FUEL RODS, halafu wakuletee utumie kuzalisha umeme. Na dunia kwa jinsi huo mpango wa fuel road uko sensitive, ni nchi chache sana wanaruhusiwa kufanya hivyo. Hapo hapo hujaweka gharama za kujenga mtambo wa umeme wa nuclear pamoja na gharama za maafa kama iliyotokea India, Russia na Japan
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
54,361
2,000
shida tulio nayo ni wataalamu kujenga hoja za maana kwa wanasiasa ili waweze kutekeleza miradi yenye tija kwa taifa.
kibaya zaidi tumekubali siasa inalipa zaidi kuliko taaluma!
Sawa basi
Tuweke mchanganuo wako wa gharama
Tutofautishe na ya waziri

Ova
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom