Waziri Kairuki: Almasi kutoka Tanzania imeuzwa USD Milioni 10. 2 huko Antwerp nchini Belgium

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema kuwa Almasi kutoka Tanzania yenye karati 39,557.96 imeuzwa kwa dola za Kimarekani milioni 10.2 katika mnada uliofanyika huko Antwerp nchini Belgium 7 Novemba 2017. Maafisa wa Serikali walikuwepo mnadani kusimamia uuzwaji wa Almasi. Kufuatia mauzo hayo, Serikali imepata mapato ya shilingi bilioni 1.614, kutokana na mauzo hayo.

******

Serikali kupitia Wizara ya Madini imesema imepata jumla ya mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 1.614 kutokana na mauzo ya Almasi za Kampuni ya Williamson Diamonds Ltd, zilizouzwa jana kwa njia ya mnada huko nchini Belgium.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema uuzwaji huo wa madini hayo ya almasi ulifanyika baada ya Serikali kutoa kibali cha kuruhusu Kampuni hiyo kuendelea na uzalishaji wa madini na kukubali kuuza madini hayo.

Madini hayo yakisafirishwa nchini Ubelgiji tarehe 20 Oktoba mwaka huu chini ya usimamizi wa maafisa wa Serikali.

Aidha, Waziri Kairuki amesema licha ya Serikali kuruhusu kampuni hiyo kuendelea na uzalishaji na uuzwaji wa madini ya almasi, lakini inaendelea kuzuia mzigo wa almasi za kampuni hiyo zilizokuwa zinasafirishwa kwenda Antwerp Ubelgiji Agosti 31 mwaka huu, kwa lengo la kujiridhisha kuhusu thamani halisi ya almasi hizo ambazo bado zinaendelea.

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki ameelezea tukio la ukamataji wa sampuli za miamba ya madini ya dhahabu takribani kilo 600 zilizokuwa zinasafirishwa na kampuni ya Wachina ya ZEM T LTD bila vibali kutoka wizara ya Madini Oktoba 29 mwaka huu.

Ambapo amesema baada ya kufanyiwa uchunguzi kutoka maabara ya Wakala wa jiolojia Tanzania uchunguzi ulithibitisha kuwa sampuli hizo ni miamba ya dhahabu kweli na kwamba Serikali imeamua kuwapeleka mahakamani Wachina hao ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
 
Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema kuwa Almasi kutoka Tanzania yenye karati 39,557.96 imeuzwa kwa dola za Kimarekani Milioni 10. 2 katika mnada uliofanyika huko Antwerp nchini Belgium tarehe 7 Novemba , 2017.

Maafisa wa Serikali walikuwepo mnadani kusimamia uuzwaji wa Almasi. Kufuatia mauzo hayo, Serikali imepata mapato ya shilingi bilioni 1.614
Kairuki now you are talking.Nchi unaipeleka mbali tinaanza kufaidi raslimali zetu hongera
 
..hawa ndio mawaziri wanaopewa vyeo kwa ajili ya propaganda na si merit....huko utumishi ameacha majanga kwa watumishi....sasa ameingia kwenye propaganda za madini....kazi tunayo.....kuuza madini yetu nje ni sehemu ya majukumu yao kwa nafasi zao....Na si kutambia umma kwa kuuza madini ya nchi nje....sijawahi kuskia waziri wa madini Na nishati akitangaza mauzo ya madini yetu miaka yote...haimaanishi kuwa yalikuwa hayauzwi.....propaganda kwenye uchumi ndio Sera ya awamu hii....
 
Yani dola million 10.2 unapata tax ya dola laki 4. Hii ni 0.5 percentage.
HABARI,
"NDEO,
Hiyo pesa tuliolipwa ni ya mrabaha wa wali,Ada ya ukaguzi pamoja na mrabaha baada ya almasi kupigwa mnada ila ile 25% Iko pale plae hizo rekodi serikali inazo ikifika muda wa gawio la faida tunachukua asilimia yetu 25 ambayo zitakuwa ni nyingi pia ukumbuke Rais alishasema asilimia zetu zirudi pale pale 50% kama zamani hapo mapato yatakuwa makubwa zaidi


LUMUMBA
 
Tushachoka na propaganda za huyu mama, ila tumvumilie kidogo maana soon ataenda maternity leave so tutapumzimka. Nahisi jin la mtoto atakayezaliwa litaanza na herufi J kama kawaida.
 
HABARI,
"NDEO,
Hiyo pesa tuliolipwa ni ya mrabaha wa wali,Ada ya ukaguzi pamoja na mrabaha baada ya almasi kupigwa mnada ila ile 25% Iko pale plae hizo rekodi serikali inazo ikifika muda wa gawio la faida tunachukua asilimia yetu 25 ambayo zitakuwa ni nyingi pia ukumbuke Rais alishasema asilimia zetu zirudi pale pale 50% kama zamani hapo mapato yatakuwa makubwa zaidi


LUMUMBA
Kumbe tunaanza kutusua taratiibu
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom