Waziri Kagasheki ajiuzulu; David Mathayo, Nchimbi na Nahodha watimuliwa na Rais Kikwete!

tunataka mawaziri kama hawa wanaopenda kuwajibika.
ni mwanaume wa kweli. amekubali kuwajibika hata kama hahusiki
CCM waige mfano wake,,bado wale vinganganizi wengine tuwasikie kama nao watatoka
 
Waziri wa Maliasiri na utalii atangaza kujiuzuru rasmi akiwa ndani ya bunge.

Asema yeye ni mtu mzima na kasikia mengi, kateuliwa na rais kwa matakwa ya rais na hakuomba hivyo ana resign.

Jembe limeondoka,ni kweli huyu waziri alikuwa ni mpiganaji,sema tu watekelezaji wa saka saka ya majangili ndio tatizo.
 
Lete maneno mkuu,maana wengine tupo mbali kidogo!

Anasema wizara yake ina sera iliyopitishwa na Bunge mwaka 2006 hivyo anaishangaa kamati iliyoibua ubaya wa operesheni tokomeza ujangili ni kwa namna gani imemhusisha na imesema kuwa wizara anayoisimamia haina sera mpya hivyo inafaa ajipime.
 
Nimefurahi kwa kitendo cha waziri Kagasheki alichokiita ku-take political responsibility na kuamua kujiuzulu. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa siasa zetu za hapa Tanzania, yawezekana anahusika au hahusiki but I truly admire your decision!
 
Mathayo David Mathayo naona anabisha. Mpare kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku hajambo
 
Waziri wa Maliasiri na utalii atangaza kujiuzuru rasmi akiwa ndani ya bunge.

Asema yeye ni mtu mzima na kasikia mengi, kateuliwa na rais kwa matakwa ya rais na hakuomba hivyo ana resign.
Huyu mtani wangu amefanya uwamzi mzuri. Hii wizara hakuna Waziri atakaemzidi kagasheki kwa kujaribu kuzuia ujangili. Lililo wazi ni kwamba hii Wizara ni shamba la CCM. Anaejaribu kuziba mianya ya ujangili hawezi kudumu.
 
safi sana kagasheki, hata hivyo hana njaa anajua hata akisepa hawezi kuhangaika na maisha, hategemei ubunge wala uwaziri kuishi vizuri
 
Back
Top Bottom