Waziri Kagasheki ajiuzulu; David Mathayo, Nchimbi na Nahodha watimuliwa na Rais Kikwete!

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Wakati waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dr. Emmanuel Nchimbi alikuwa wa pili na wa Ulinzi akiwa wa kwanza kwa kuitwa na spika kuwa wa kwanza kuzungumza lakini ikaonekana wameingia mitini na kuitwa kwa waziri wa utalii na maliasili ndugu Balozi Hamisi Kaghasheki

Waziri wa Maliasiri na utalii atangaza kujiuzuru rasmi akiwa ndani ya Bunge.

Asema yeye ni mtu mzima na kasikia mengi, kateuliwa na rais kwa matakwa ya rais na hakuomba hivyo ana resign.

Mathayo yeye anadai ameshutumiwa mambo mengi kama sena na mgumo vyote vipo ila hakuhojiwa katika swala lolote , adai tatizo ni mfumo na swala la ardhi liko chini ya wizara ya ardhi na si wizara ya ardhi.

Na swala la mifugo na majosho ni swala la halmashauri na si wizara ya mifugo yeye anaonewa tu.

Asema hajawahi kupewa fedha za bajeti kama anavyoomba ajilinganisha na Yesu kuwa anasurubiwa lakini hana hatia.

Updates;

Waziri mkuu anaongea kwa kujumuhisha kwa mawaziri waliosalia na anaanza kwa kauli zake za kuzunguuuka na kuomba radhi kwa waliotendwa na operation tokomeza.

Anachojaribu kusema kama serikali wanatafakari na watafanyia kazi kama serikali kwani operationi ilikuwa chini ya wizara tatu.

Na anaendelea kutazama na kuangalia na anapendekeza iundwe tume ya kuthibitisha hayo kama alivyoshauri Mwanasheria mkuu wa serikali.

Updates:

Waziri mkuu atangaza kuwa rais ametengua uwaziri wa wizara tatu rasmi zikiwemo ya Ulinzi chini ya Nchimbi, ya ulinzi chini ya Nahodha, ya mifugo chini ya Mathayo na Kagasheki aliyojiuzuru ya maliasili na utalii
 
Kaaazi ipo. Kaamua ku-resign rasmi na atamwandikia barua rais soon.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
54 Reactions
Reply
Back
Top Bottom