Waziri kadhihirisha:ni kweli wizara ya habari haina kazi, na watanzania hatuhihitaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri kadhihirisha:ni kweli wizara ya habari haina kazi, na watanzania hatuhihitaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by akili, Jul 16, 2009.

 1. a

  akili Member

  #1
  Jul 16, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NI KWELI WIZARA YA HABARI HAINA KAZI, NA WATANZANIA HATUHIHITAJI

  Kuna wanaolalamika kwamba ni kuionea CCM kudai kuwa serikali yake ni kubwa mno na viongozi hawana uwezo wa kumsimamia kila mtu.

  Ingawa kuna wanaoamini kwamba ukweli ndio huo. Tanzania haihitaji wizara 30 na ushee. Na ushahidi kutokana na majibu ya Waziri wa Habari, Utamaduni na nanihino unatosha kudhihirisha ukweli huu. Ni wizara ambayo ipo ipo tu kwa ajili ya sababu za kisiasa. Kukataa sheria ya Uhuru wa Habari na kutaka kwake kuanzisha sheria/chombo cha kudhibiti vyombo vya habari ni tangazo la kumtaka Mheshimiwa Rais kuifuta wizara hiyo.

  Yapo madai ambayo bado sijayathibitisha kuwa Wizara nyingi zipo ili kuipitishia CCM fedha zinazoisadia kufanya vitu vyake ili ishinde uchaguzi kila baada ya miaka mitano. Nyingi kati ya Wizara zinaweza kufanywa kama BRELA, TRA, TCRA na zikawajibika na kufanya kazi nzuri kuliko kuwa wizara zinazokula kodi ya wananchi bila ya sababu japokuwa zinamwagiwa fedha kedekede na wafadhili kama vile Wachina, Wakuba, Wajapani na Wahindi.

  Waziri anabisha kwamba TBC haina mwanabodi Mwislamu hivi anamdanganya nani. Atuletee kumbukumbu za vikao vya bodi kama vitaonesha kama kuna siku hata moja huyo bwana Hassan Mitawi keshawahi kuhudhuia vikao vya bodi hiyo toka iundwe. Kwani wabunge wanadanganywa kama watoto ?

  MATANGAZO mengi ya serikali, japo waziri kapiga chenga swali hili ni kweli kabisa wanapewa wanasiasa wenye magazeti na tunawajua fika. Na inakuwa hivyo ili baadaye kiasi cha fedha fulani kilicholipwa kirudi tena CCM.

  Waziri anapovilaumu vyombo huru vya habari na kisha wao kuwafanyia wenye vyombo hivyo uonevu na dhuluma waziwazi juu anaona raha gani na anakijengea heshima gani chama chake ambacho baadhi ya wanachama wake ni wamiliki pia wa vyombo vya habari visivyonufaika sana na matangazo toka serikalini.

  Katika miaka hii ya SIMU ZA MKONONI serikali inaweza isitoe tangazo hata moja kwenye magazeti wala redio ila kwenye SIMU ZA MKONONI tu na matangazo hayo yakawafikia Watanzania wengi zaidi kuliko ilivyo sasa.

  Mheshimiwa Rais kama unang'ang'ania kuwa na Wizara ya Habari basi chagua waziri kijana anayejua dunia ya habari na mawasiliano ya umma inakwenda wapi na sio waziri wa enzi za ujamaa anayejua tu kutetea umoja na mshikamano. Huo umoja na mshikamano wa uongo na kweli kila Mtanzania sasa hivi anajua hawezi kuufanya ugali wala maharagwe. Hawezi kuula huo umoja na mshikamano wa danganya toto, ila umoja na mshikamano huo upo ili kumla yeye. Hii hali ya kuwa na 'wajamaa' kwa maneno, lakini mabepari wa kutisha kwa vitendo hakuna anayeikubali tena. Na uanasiasa bora siku hizi mtu asikudanganye sio maneno na hotuba nzuri bali vitendo na tabia inayoendana na kile jamii inachokitarajia toka kwa viongozi waadilifu na waliopo madarakani kwa ajili ya wananchi na sio kwa ajili yao wenyewe na jamaa zao.

  Na kichekesho cha mwaka ni pale inaposemwa waandishi wa habari wawezeshwe kuanzisha vyombo vyao wenyewe vya habari wakati sheria na projecti zote za waziri anazozianzisha na alizozianzisha ni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba anawazuria waandishi wa habari kujiunga na kuanzisha biashara zao za habari wao wenyewe. Hkuna sisi waandishi wa habari zuri tunalotegemea kutoka kwa serikalli hii au nyingine vya CCM zikiendelea kuwa na watu kama hawa ila sisi kuendelea kutumiwa tu na kisha kutupwa baada ya watu hawa kurudi tena madarakani.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuchika ajibu pumba, aokolewa aibu na naibu Spika

  Waziri wa habari utamaduni na michezo, George Mkuchika alijikuta katika wakati mgumu Bungeni baada ya kubanwa na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na swali ambalo alilijibu kwa ubabaishaji mkubwa.

  Alipokuwa akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya Mkuchika, Ole Sendela alitka kujua iwap[o hakuna mgongano wa kimasilahi kwa magazeti yasiyokuwa na usambazaji (circulation) kubwa, mengineyo yakimilikwa na mawaziri kupata matangazo ya hotuba za bajeti za wizara zaerikali huku yale yenye circulatuion kubwa kukosa.

  Ole Sendeka alisema magazeti yenye circulation ndogo hayawafikii wananchi wengi na hivyo serikali inatumia fedha za walipa kodi kwa tija ndogo.

  Akijibu swali hilo ambalo lilionekana liko wazi, Mkuchika aliondoka kabisa kwenye mada ya swali lenyewe na kuanza kuzungumzia swala la yeye kutonukuliwa na magazeti na kuhoji, “iwapo magazeti hayanitambui mimi kama ni serikali, sasa vipi yaje tena kuomba matangazo?”

  Akajitapa kuwa yeye ni mkweli kabisa katika utendaji kazi wake lakini baadhi ya magazeti hayataki kukubali kuitambua serikali na baadaye kulalamika kuhusu matangazo.

  Bila shaka Mkuchika alikuwa anazungumzia uamuzi wa jukwaa la habari mwishoni mwa mwaka jana la kutomnukuu baada ya kulifungia gazeti la Mwanahalisi, uamuzi ambao hata hivyo ulishaondolewa – haupo tena.

  Ole Sendeka hakuridhika na majibu yaliyoonekana ya “hovyo hovyo” ya Mkuchika na akasisitiza kuwa waziri alikwenda kwingine kabisa – yaani hayo masuala ya yeye kutonukuliwa na magazeti hayakuwamo katika swali lake.

  Alirudia swali lake, safari hii akiwa clear zaidi na kwa ufasaha mkubwa – akisema inakuwaje wizara zinatoa matangazo ya bajeti kwa vijigazeti vidogovidogo vilivyoanzishwa hivi karibuni, vingine vinamilikwa na mawaziri huku serikali ikijua wazi kwamba ujumbe uliomo katika matangazo hayo hautawafikia wananchi wengi kutokana na circulation ndogo ya vijigazeti hivyo? Aliongeza na kusema vijigazeti vingine huchapisha nakala chache tu baada ya kupata tangazo, nakala ambazo huuzwa Dar tu.

  Kabla ya Mkuchika kujibu swali hilo la nyongeza, naibu Spika alisimama na kusisitiza kuokoa muda na kwamba Mbunge atajibiwa wakati mwingine.
   
 3. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Zak Malang!

  CCM kwa ubabe huwawezi huyo jenesta ana uthubutu wa kumkatiza Ole Sendeka kwa vile hilo Bunge lenyewe it's a laughing stock!! Kama ulivyoweka Mkuchika ameongea pumba na CCM pumba wakafurahia'' Siku redamption day ikifika kila mtu atajibu kivyake!!!! Yes nilikwisha washauri hao wapuuzi waunde REGULATORY BODIES KWENYE : media,shule,hopitali; viwanda;vyote vinavyodhalisha bidhaa etc..etc..if hopeless EWURA and SUMATRA are trying to pull their muscles to regulate japo in a corrupt way then kuna haja ya wapumbavu TCRA kuamka huwezi ukawa Referee while you are a player hilo CCM HAWALITAKI kwa hiyo matatizo hayatakwisha milele.!!!
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Katika thread ya Jenerali Ulimwengu na makala yake kuhusu majigambo ya rais Kikwete kwamba hana mbia katika urais wake, nimezungumzia kuhusu kukosa uelewa wa tofauti ya rais kama mtu na urais kama taasisi.

  Mkuchika naye anaelekea kuwa katika mawazo hayo hayo ya kutoweza kutofautisha waziri kama mtendaji na dhamana ya cheo cha uwaziri.Inabidi Mkuchika aweze kuuangalia uwaziri kama sio yeye na kwamba yeye amepewa dhamana tu ya kuendesha wizara kwa muda. Watu wanakuwa na egos na antics kuliko some royals ambao wamepewa haki ya kuzaliwa kujitapa.

  Ukubwa una mengi, mojawapo ni lawama.Mtu yeyote anayetaka cheo na ukubwa ni lazima aweze kuwa na kifua cha kuzuia maneno bila kuwa na kinyongo kinachoweza kuharibu kazi.Mkuchika ameonyesha hamaki iliyoleta kinyongo kilichoharibu kazi kama alivyoweza kuonyesha kirahisi kabisa mbunge wa Simanjiro.Badala ya kuleta statistics za kupinga hoja ya swali (probably hamna statistics hizi kwa sababu swali limekuwa based katika ukweli) waziri huyu -ambaye kimsingi ni waziri wa propaganda- ameshindwa hata kuspin taarifa za wizara yake mwenyewe.I guess incompetency yake ni ya faida kwa taifa, maana sasa tumejua bila kificho kwamba serikali haiongozwi kwa ufanisi wa utendaji, bali kwa network za kisiasa na kuabudiana.

  Hongera mbunge Ole Sendeka wa Simanjiro.
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Baadhi ya Wahariri bado wamemnunia Mkuchika atafanyaje?
  Na yeye Bwana Kiburi (Mkuchika) mambo mengine hayafanyi yamekwisha anawaminyia makusudi eti watamjua yeye ni nani!
   
 6. H

  Huduma Member

  #6
  Jul 17, 2009
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunapenda kumkumbusha Waziri wa Habari kuwa TBC ni shirika linaloendeshwa kwa kodi za Waislamu na Wakiristo na asituletee hoja za ovyoovyo eti kwamba Watanzania tumeshavuka kwenye suala la kuulizana nani yuko shirika hili na nani yuko shirika lile.

  Sir George, hi sio Uingereza ambako Anglikana na wayahudi tu ndio wanaoruhusiwa kuwa kwenye bodi ya BBC.

  Unachotuonesha hapa ni kwamba huwa unaanguka tu saini bila kusoma na kujiuliza inasaini nini. Umechemsha, umefulia na umepiga pasi mpaka kuunguza nguo ya umoja na mshikamano kati ya Waislamu na Wakiristo na Wahindi na Mapagani. Pole mzee. AJUA!!!

  Tunaomba wakereketwa wakafanye sensa huko TBC na hatutashanga tukikuta wafanyakazi wanaoshika nafasi za juu asilimia 96 sio Waislamu maana ndivyo inavyokuwa kama mteua bodi kateua bodi bila tafakuri wala kuangalia balansi of power katika jamhuri husika.

  Katika nchi zinazobadilika Waziri wa Habari au Msemaji wa Ikulu huwa kijana aliyesomea tu sio uandishi wa habari bali elimu zingine na hasa falsafa ya ubishi na upangaji mambo kwa hoja. Watu wanaotumia hoja za nguvu ndugu yangu, rika letu, mheshimiw baba wa Tanzania sio mtu anayefaa kushika dhamana hii kila siku atakuwa anakorofishana na watu na siku zote anageuka nyuma akidhani vyombo vyote vya habari ni maadui zake.

  Yaani, waziri mzima analipiza kisasi kwa kutumia kodi ya wananchi ???? Ina maana gani waziri anapokiri kwamba kanyima magazeti na vyombo vingine vya habari matangazo eti kwa sababu vyombo vyote kwa pamoja nchini vilitamka vina mublacklist kiongozi huyo. Huu ndio uongozi gani jamani.

  Au hii ndio sera rasmi rasmi ya CCM kulipiza kisasi kwa wale wote wanaotofautiana nayo kimawazo au kimsimamo? MUngu tuepushe na chama na wanasiasa kama hawa.
   
 7. O

  OkSIR Senior Member

  #7
  Jul 17, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angalia asijekutufungia ndugu yangu.......yule bababa ana hasira za kipekee najiuliza sijui huko nyumbani wakoje na mkewe labda na yeye awe mwanajeshi ndio zitaenda....yaaani kila sehemu anataka kuwapeleka watu kijeshi jeshi...
   
 8. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yesterday I was shocked to hear what the minister replied in the perliament and it remainded me of one article written in Kulikoni newaspaper this week questioning the eligibility of some ministers holding the posts.

  I qiute agree with the Sendeka's concern that its true there are several new newspapers in the streets which have just arise during this advertisement harveasting time. Ask your self, why Sauti ya Kusini Newspaper and not MWANANCHI? oR IS IT THAT THEY ARE NOW ACCUMULATING FUND TO FINANCA THEIR CAMPAIGNS. pLEASE jf MEMBERS DO A REASERCH ON THIS YOU WILL BE SHOCKED.
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Du hivi Tanzania nnayoifahamu kuna suala la dini kwenye kuteuliwa kwenye Bodi?????? Mbona sielewi elewi? And well kama mtu au watu wa dini yangu wakiwepo huko hata asilimia 100 wanatusaidia nini if they don't deliver???????
   
Loading...