Waziri Kabudi: Viongozi wa dini ambao hawajasajiliwa na RITA hawataruhusiwa kufungisha ndoa ya aina yoyote

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema viongozi wa dini ambao hawajasajiliwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) hawataruhusiwa kufungisha ndoa ya aina yoyote na endapo watafungisha ndoa bila ruhusa, ndoa hiyo itakuwa batili.

Kabudi.jpg
 
Hao wafungishwa ndoa watawajuaje sasa, anyway hilo linaeleweka kuwa ndoa ya ikfungishwa na mtu asiye na mamlaka manake ni batili from the way go
 
SHERIA ILIKUWA HIVYO MIAKA YOTE.
WACHUNGAJI NA MAASKOFU LAZIMA WAWE NA LESENI YA:

1. KUFUNGISHA NDOA
2. KUONGOZA MAZISHI.

SASA HUYU KABUDI NADHANI ANATUKUMBUSHA TU.
 
Hivi misukule inayofufuliwa pale Kawe, RITA wanaizingumziaje ? Wanawatambua kama waliofariki au wanawahesabia wamezaliwa upya ?
Hili ini swali zuri sana kuwauliza wenye mamlaka ya kulinda sheria zetu na kutuepusha na matapeli.

Siyo hivi wanaongelea mambo ambayo hata walio chekechea wanajua. Au waliachia tu wamekuja kushtuka sasa?
 
Hivi misukule inayofufuliwa pale Kawe, RITA wanaizingumziaje ? Wanawatambua kama waliofariki au wanawahesabia wamezaliwa upya ?
haaha inabidi RITA ihakikishe vyeti vyao vya kifo vya hao misukule vinafutwa na kuwasajili kama raiya wa kigeni kutoka mashamba ya giningi.
 
Kibudu ameenda kwenye eneo lake. Huyu ni prof. wa Family Law (Ndoa na mirathi), ni branch ambayo inasomwa na wenye uwezo mdogo wa kimasomo.
 
Back
Top Bottom