Waziri Kabudi: Tanzania haijazuia Maandamano wala Mikutano ya Kisiasa!

Nani anaandaa hizo taratibu,
Amemhusisha mdau gani,
Nani amelalamika kuwa zilizopo siyo rafiki?
Kabudi kabudi kabudi hiki kizazi siyo cha Mazuzu
Halafu ni Prof wa sheria. Anasema Ulaya maandamano wanafanyia nje ya miji. Asilimia kubwa ya watanzania ni ignorant wa elimu ya siasa na hawana exposure ya mambo ya nchi zingine, anautumia huo upungufu kuwaambia lolote analopenda.
 
Pole sana, ni vigumu kukuamini tena. Katiba mpya ndio dawa sio kwa aina yako tu bali hata nduguyo Ndugayi
 
Hatuhitaji maandamano ya kisiasa.

Tunahijati maji, umeme, ajira na uchumi mzuri.

Huko kuandamana mkaandamane wenyewe.
Iponsiku inakuja utasema hata hayo maji na umeme hauvihitaji unataka uhuru wa kuandamana.
 
View attachment 2017173

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palagamba Kabudi amesema Serikali haijazuia maandamano na mikutano ya kisiasa isipokuwa wanaandaa utaratibu rafiki utakaotumika pasipo kuvunja sheria za nchi.

Kabudi amesema kuwa inatambua umuhimu wa mikutano ya siasa na pindi utaratibu utakapokamilika watatangaza mfumo mpya.

“Maandamano na mikutano ya kisiasa haijazuiwa nchini ila inaratibiwa na imewekewa utaratibu. Ndio maana ninasema haijazuiwa. Hakuna jambo linalofanyika bila utaratibu. Tunasoma sura ya pili ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano kuhusu haki za binadamu bila kusoma ibara ya 30 iliyoweka mipaka ya wewe kufaidi uhuru wako,” alisema.

Alitaja mipaka iliyowekwa kuwa ni mtu kutoingilia uhuru na haki ya mwingine, maagizo ya umma, usalama na afya.

Waziri huyo amesema mipaka hiyo imewekwa pia katika uhuru wa kuabudu na imani ambapo mtu anatakiwa kuifuata anapotumia uhuru wake.

Ameongeza kusema kuwa hakuna uhuru usio na mipaka ambao kuepusha ghasia kwa watu wengine na mipaka hiyo haipo Tanzania pekee bali mataifa mengine pia.

Amefafanua kwa kusema kuwa Tanzania ni nchi pekee Kusini mwa Jangwa la Sahara yenye Sheria ya Vyama vya Siasa baada ya kurejea katika mfumo wa vyama vingi ambayo imeweka wajibu na majukumu huku vihakikishiwa ruzuku kwa vile vinavyoshinda ubunge na udiwani inayotokana na kodi za wananchi.

Kuhusu maandamano, amesema lazima kuwe na utaratibu ikiwamo kujulikana kwa mahali na siku ya kuyafanya.

Alisema kuna nchi zimeweka utaratibu maandamano ni Jumamosi tu ili siku za wiki watumishi wafanye kazi na kwa nchi za Ulaya maandamano yanafanyika nje ya mji.

Kuhusu utaratibu wa kufuatwa ili kuandamana, alisema Sheria ya Usalama Barabarani imeweka mwongozo.

“Ukiisoma vyema hata magari ya harusi yakizidi 10 inabidi ukaombe ruhusa trafiki kwamba leo mimi mtoto wangu atakuwa anaoa nitakuwa na magari kama 20 hivi,” alisema.
Stupid professor
 
tatizo vyama vya siasa hapa nchini,havijui kuheshimu Sheria za nchi,vikipewa Uhuru ,Basi vinautumia vibaya,wakipewa Uhuru wa kufanya mikutano yao na harakati zao Basi wanajisahau na kuanza kuichokonoa nchi .hawa bila kuelekezwa namna ya ku behave kamwe ,hawawezi kujiendesha.ni bola waendelee kudhibitiwa na kuelekezwa namna ya ku behave!!
Yaani na wewe hapo unaona umetoa mchango mzuri juu ya Kauli ya Kabudi, serious?

Sent from my PRA-LA1 using JamiiForums mobile app
 
View attachment 2017173

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palagamba Kabudi amesema Serikali haijazuia maandamano na mikutano ya kisiasa isipokuwa wanaandaa utaratibu rafiki utakaotumika pasipo kuvunja sheria za nchi.

Kabudi amesema kuwa inatambua umuhimu wa mikutano ya siasa na pindi utaratibu utakapokamilika watatangaza mfumo mpya.

“Maandamano na mikutano ya kisiasa haijazuiwa nchini ila inaratibiwa na imewekewa utaratibu. Ndio maana ninasema haijazuiwa. Hakuna jambo linalofanyika bila utaratibu. Tunasoma sura ya pili ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano kuhusu haki za binadamu bila kusoma ibara ya 30 iliyoweka mipaka ya wewe kufaidi uhuru wako,” alisema.

Alitaja mipaka iliyowekwa kuwa ni mtu kutoingilia uhuru na haki ya mwingine, maagizo ya umma, usalama na afya.

Waziri huyo amesema mipaka hiyo imewekwa pia katika uhuru wa kuabudu na imani ambapo mtu anatakiwa kuifuata anapotumia uhuru wake.

Ameongeza kusema kuwa hakuna uhuru usio na mipaka ambao kuepusha ghasia kwa watu wengine na mipaka hiyo haipo Tanzania pekee bali mataifa mengine pia.

Amefafanua kwa kusema kuwa Tanzania ni nchi pekee Kusini mwa Jangwa la Sahara yenye Sheria ya Vyama vya Siasa baada ya kurejea katika mfumo wa vyama vingi ambayo imeweka wajibu na majukumu huku vihakikishiwa ruzuku kwa vile vinavyoshinda ubunge na udiwani inayotokana na kodi za wananchi.

Kuhusu maandamano, amesema lazima kuwe na utaratibu ikiwamo kujulikana kwa mahali na siku ya kuyafanya.

Alisema kuna nchi zimeweka utaratibu maandamano ni Jumamosi tu ili siku za wiki watumishi wafanye kazi na kwa nchi za Ulaya maandamano yanafanyika nje ya mji.

Kuhusu utaratibu wa kufuatwa ili kuandamana, alisema Sheria ya Usalama Barabarani imeweka mwongozo.

“Ukiisoma vyema hata magari ya harusi yakizidi 10 inabidi ukaombe ruhusa trafiki kwamba leo mimi mtoto wangu atakuwa anaoa nitakuwa na magari kama 20 hivi,” alisema.

Kweli mheshimiwa anatuona mazuzu. Nchi gani ulaya inakataza maandamano katikati ya mji?

Amandla...
 
Uwendawazimu, hauchagui mtu wa kumpata. Unaweza kumpata ngumbaru au hata profesa kamili au profesa wa majalalani.
 
Katiba ya nchi hii iko wazi. Waliodhani tumesalimu amri habari hii na iwafikie live bila chenga:

IMG_20221213_193025_177.jpg

Nyote msiojua kutokuheshimu katiba ya nchi hakuna cha mswalia mtume, habari hii na iwafikie.

Kimsingi habari ndiyo hiyo.
 
Sioni sababu kwanini jambo lililo kisheria liandaliwe "taratibu rafiki" huu ni ujinga tu.

Kama wanataka kubadilisha sheria, waende kwenye bunge lao wakafanye hivyo, lakini sio kupindisha sheria.
 
Hawa ni WA kukutana nao head on. Busara kwao haina maana. Viapo kwao kuilinda na kuiheshimu katiba ya nchi kwao hakuna maana yoyote.
 
Back
Top Bottom