Waziri Kabudi: RITA Kuanzisha mfumo wa usajili wa ndoa kwa njia ya Mtandao

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Prof. Kabudi alibainisha hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya nne ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu yaliyoandaliwa na RITA na kusema mfumo huo utasaidia kutoa nakala mtandaoni kabla ya nakala ya cheti cha ndoa kutolewa.

“Kabla mfumo huu haujaanza kufanya kazi, wadau wote waitwe wapewe elimu ya pamoja ya namna ya kwenda na teknolojia hii," aliagiza Prof. Kabudi.

Alisema rejista inawahusisha wanaofungisha ndoa kwa sababu siyo kila mtu ana mamlaka ya kufungisha ndoa kwa mujibu wa katiba ya nchi.

“Kiongozi wa ndoa ambaye hajasajiliwa kufungisha ndoa, akifungisha hiyo ndoa ni batili. Wenye ruhusa tu ndio wafungishe. Ambao hawana mamlaka watume maombi RITA wapewe kibali cha kufungisha ndoa,” alisema Prof. Kabudi.

Alisema viongozi wengine wa dini ambao hawajasajiliwa wanaona kama ni usumbufu kufuata taratibu za kupatiwa kibali, lakini ni muhimu kwa ustawi wa taifa.

“Ndoa ni suala la hiari lakini kuvunjika kwake lazima serikali ihusike katika kuuvunja mkataba huo na wanaofungisha lazima nao wawe na kibali cha kufanya hivyo, siyo tu kila anayeongoza ibada anaweza kufungisha ndoa,” alisema Prof. Kabudi.

Alisema duniani kote suala hilo linasimamiwa kikamilifu kwa sababu ndio msingi wa familia inayozalisha raia wa nchi husika.

Sambamba na hilo, aliwataka RITA kuhakikisha wanaendelea na jitihada za kusajili watoto chini ya miaka mitano kwa njia ya mtandao.

Alisema usajili wa watoto hao umefika katika mikoa 20 na jumla ya watoto milioni 6.5, sawa na asilimia 55 wamesajiliwa toka asilimia 13 ya mwaka 2012.

Kaimu Mkurugenzi wa Haki za Kisheria wa RITA, Lina Msanga, alisema watahakikisha wanasogeza vituo vya matumizi ya teknolojia karibu ili watoto chini ya miaka mitano wapate hati za kuzaliwa kwa kutumia simu za mkononi.

Alisema malengo yao ni kuhakikisha wanaongeza mwamko wa kusajili vifo, ndoa, talaka na sababu za vifo.

Maadhimisho hayo yalifanyika sambamba na semina ya viongozi wa kitaifa wa vyama vya watu wenye ulemavu.

Chanzo: Nipashe

Mimi nimejikuta nacheka tu, sijui wanabodi wengine.
Hawa majamaa ndo aliosema Gwajima watupishe ama wapumzike, walishakosa credibility na wameishiwa pumzi. Kwani CCM hakuna wengine wanaweza kupata hizi nafasi
 
Hivi tukishapata idadi ya ndoa zote nchini inasaidia nini? Nieleweshwe tafadhali.
 
Hii inaweza kuja kuwa na faida kubwa mbeleni

Mipango ya nchi, Budget haswa kwenye huduma za kijamii kama afya na elimu, Umiliki wa rasilimali katika familia, Kazi, Mifumo ya kodi na mahitaji ya watoto kwa ujumla itaweza kuzingatia pia msingifamilia kwa urahisi zaidi haswa kwa kuzingatia nguvukazi na kipato walicho nacho.

Tusiwe tunapuuza au kukebehi kila kinachofanywa na serikali
 
Hii inaweza kuja kuwa na faida kubwa mbeleni

Mipango ya nchi, Budget haswa kwenye huduma za kijamii kama afya na elimu, Umiliki wa rasilimali katika familia, Kazi, Mifumo ya kodi na mahitaji ya watoto kwa ujumla itaweza kuzingatia pia msingifamilia kwa urahisi zaidi haswa kwa kuzingatia nguvukazi na kipato walicho nacho.

Tusiwe tunapuuza au kukebehi kila kinachofanywa na serikali
Wanaoishi bila ndoa ni wengi kuliko wasio na ndoa. Sijui itamsaidiaje huyu professor wa jalalani akishajua idadi ya ndoa
 
Wanaoishi bila ndoa ni wengi kuliko wasio na ndoa. Sijui itamsaidiaje huyu professor wa jalalani akishajua idadi ya ndoa
Hata hao wenye ndoa wengine kesho kutwa tu wanaachana kwa talaka tatu. Sasa watakuwa bado wanahesabiwa wako kwenye ndoa au? Huko RITA wanawekaje hizi kumbukumbu za ndoa zinazoachika mtaani? Kazi kweli kweli ipo ya kupata takwimu sahihi aambazo ni real time. Wawe tu wanatumia data za census kila baada ya miaka kumi kuona kama wanandoa bado wapo pamoja au wameachana tangu census iliyopita. Hiyo itawapa takwimu za ndoa ambazo kidogo zinashabihiana na ukweli. Lakini real time data ya ndoa, sijui kwa kweli
 
Back
Top Bottom