yamindinda
JF-Expert Member
- Jul 29, 2011
- 1,581
- 1,318
- Thread starter
- #81
Hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na misimamo na kutokwa jasho la damuKabudi amechemka na anadanganya mchana kweupe.Nyerere alisema hageuki jiwe lakini wananchi tunakumbuka kilichotokea,ukosefu wa vitu,kuporomoka bei ya mazao mpaka kufikia watu kukosa nguo za kuvaa.Pia hili lilizalisha ulanguzi mkubwa wa bidhaa muhimu.Mkapa alikubaliana na wakubwa mpaka tukafutia baadhi ya madeni.
Kinachostua ni hiyo qoute ya kusema wa ndani ni "enemies" na wa nje ni "opponents" na ukimsikiliza kwa makini ni dalili ya kutoa vitisho kwa watu wote wanaokosoa baadhi ya mambo.Hili si jambo jema kwani enemies wanakuwa eliminated na hii ikianza (kama bado haijaanza) ina maana nchi itaingia katika machafuko na Kabudi hatakuwepo kutueleza lolote.
Anazungumza kumfurahisha mteule lakini anapeleka nchi katika mgogoro wa kidiplomasia.