Waziri kabudi: Marekani yaridhishwa na hatua za Tanzania katika ushirikishwaji wa wanawake

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
1583748919480.png

Marekani imeeleza kufurahishwa na mafanikio ya Tanzania katika masuala ya ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi za uongozi wa kisiasa na maamuzi na hatua zilizochukuliwa kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata elimu bora na salama.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na mshauri wa Rais Trump kuhusu masuala ya maendeleo ya wanawake Balozi Kelley Currie mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Washington.

Mara baada ya kukutana na mshauri huyo wa Rais Trump kuhusu masuala ya maendeleo ya wanawake Balozi Kelley Currie Prof. Kabudi pia amekutana na kufanya mazungumzo na kundi la Washington Intergovermental Professionals Group wakiwemo maseneta na mabalozi kutoka nchi mbalimbali waliopo Marekani kwa lengo la kuwaelezea fursa za uwekezaji zilizopo nchini.

Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Willson Masilingi kwa upande wake amesema ziara ya Prof. Kabudi nchini Marekani kwa kiasi kikubwa imesaidia kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na Marekani na kwamba nafasi ya kukutana na makundi mbalimbali yatahamasisha wawekezaji wengi marekani kwenda Tanzania.
 
March 8, 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Prof. Palamagamba Kabudi baada ya kutoa ahadi na nia ya serikali ya CCM kubadilika mbele ya wadau wa maendeleo (wa nje), tutafuatilia kama mikutano ya kisiasa kama huu iwe ya kina mama au raia wote ambao si ya CCM itakuwa huru kufanyika bila kuzuiwa kufanyika kwa visingizio vyenye nia ovu kubinya demokrasia iliyotamkwa kwenye katiba ya nchi ya Tanzania.

Toka maktaba:
March 8, 2020

Mkutano wa Baraza la Wanawake CHADEMA



Source: Chadema Media TV
 
Participatory: Uchumi ukue sasa kwa dhati na usiwe uchumi wa makaratasini sasa. Uchumi ulenge mifuko ya watu kwa awamu hii ya tano kipindi cha pili. Kuwe na balance na siyo bias.
 
Kabudi is just a Parrot, big mouth full of lies. Asilete uongo haha. Wamarekani hawana ujinga huo
 
Back
Top Bottom