Waziri Kabaka, yaani Hata Walinzi na Housegirls tuna-Import???

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,934
63,828
Wiki tatu zilizopita kazini kwetu kuna jamaa alikua anatafuta HG na akaletwa Binti mmoja kwa jina la Esther Banda ambaye nilikuja kugundua kuwa ni M'malawi na alishafanya kazi za ndani kwa watu kadhaa, lakini pia nilikwenda mahali fulani kwa mtu na kukuta nae HG wake ni Mkenya, nikaendelea kukaa kimya ila nikakumbuka kuwa Mama Kabaka alisema kuwa hakuna Foreignres wanaoweza kuja kufanya kazi bongo bila work permit na ruhusa nyinginezo.

Nikapeleleza wee nikakuta kumbe Hata Directors wengi hasa HR na wale wa Utawala ni Wageni, nikaona hivi kweli huyu Mama halioni hili au haambiwi hili?

Sasa Jumatatu nilikua kwenye Ubalozi fulani, yaani eti Walinzi wa KK Security na G4S nayo imeajiri walinzi toka Kenya? Walinzi wa kawaida kabisa? No No hii sasa ni too much jamani, sisemi kumsingizia Mtu ila huo ndio ukweli, nimezitaja kwa makusudi ili kuondoa mzizi wa fitina japo najua kuwa wamiliki wao au wenye hisa pengine ni Wakenya but sidhani kama wanakibali cha kuleta hadi walinzi toka Kenya. Nina uhakika na ninachokiongea

It pains hata kama wanasema Tu wavivu but huu sasa ni uonevu
 

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,637
Hao waliowaajiri ni wabongo au wageni? kama wameajiriwa na wabongo hii sio issue ya kabaka tena.
 

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,957
4,622
Si ndio serikali mliyoichagua hiyo?
Sheria za kazi za nchi hii zipo wazi kabisa tena very strictly lakini hazifuatwi na hakuna wa kuzisimamia.
 

afsa

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
1,965
1,526
Hata kama tukipiga kelele za kila aina haitusaidii wao wameridhika na maisha ni vigumu kutukumbuka sisi walala hoi, cha msingi ni kutafuta njia sahihi ya kuwaondoa madarakani.
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,934
63,828
sichagui uchafu huu ni afadhali kura yangu nisiipige kabisa kuliko kuwapigia wahuni hawa
Si ndio serikali mliyoichagua hiyo?
Sheria za kazi za nchi hii zipo wazi kabisa tena very strictly lakini hazifuatwi na hakuna wa kuzisimamia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom