Waziri Jumaa Aweso, unajua kero hii huduma ya kuunganishiwa maji?

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
3,691
2,000
Habari za Asubuhi waungwana,

Kama kichwa cha habari kisemavyo.

Serikali imekuwa ikijipambanua kuongeza kasi ya upatikaji wa maji kwa wananchi wake.

Lakini mpaka leo kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo katika maeneo kadhaa ya mjin kwa kisingizio cha uhaba wa vifaa vya kuungwanishiwa huduma hiyo muhimu hata kama ukiwa umeshafanya malipo ya kuunganishiwa huduma hiyo.

Wakati waziri akiwa busy kusimamia sekta hiyo, ajabu mamlaka kama ya DAWASA Kibaha Mjin ukilipia huduma iyo unaambiwaa usubirie mpaka vifaa vipatikane ndio utapigiwa simu ili ukaunganishiwe maji na wanadai inachukua muda usiopungua WIKI MBILI na kuendelea.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom