Waziri John Magufuli hili la kuvunja jengo la TANESCO Ubungo tumia busara

Wahandisi, wakandarasi, wapima, wasanifu na wachoraji inabidi wafikirie nje ya boksi waje na kitu kama hiki ili kuokoa hayo majengo na barabara ya Morogoro, hasa kwa wale wanaopendekeza kujengwe makutano ya juu (flyover) ubungo. Angalia hizi picha ya barabara na michepuko yake iliojengwa nchini Japan. Baada ya hapo mshaurini Waziri wa Ujenzi afanye nini?
Japan na Tanzania wapi na wapi bwana/bi? NI kama kumlinganisha JK na JKN.
Na majirani zetu nao suala ni hilo hilo.
http://architecturekenya.com/2011/0...-in-bid-to-expand-city-highway-by-dave-opiyo/

http://allafrica.com/stories/201101170458.html
 
Soko la mahakama ya ndizi lishabomolewa leo alfajiri,watu ni wengi sana,ukipita barabara ya morogoro road utaona,hali ilivyo kuwa ni mbaya.
 
Mimi nilitegemea mpaka sasa hivi PM au JK mwenyewe wawe wamesha ingilia kati kuwawajibisha waliobariki ujenzi kweye hizo road reserves na kuitia hasara serikali lakini wapi bana....wako kiiiimya!! Matokeo yake sakata lote hili linaonekana kuwa ni la Magufuli peke yake!!

Ama kweli la kuvunda halina ubani!
 
Sijaluelewa mkuu, unajaribu kusema kwamba nikitumia pesa nyingi sana kuvunja sheria inabidi sheria itupwe ili mimi nisiwe nimepata hasara kwa kuvunja kwangu sheria?

Anachotaka kusema mwanzisha mada ni kwamba:
1.Serikali anayoItumikia MAGUFULI ni moja ile ile iliyokuwa madarakani kipindi haya majengo yanajengwa.
2. Sheria hizo hizo anazotaka kuzitumia kuyavunja zilikuwepo na wasimamizi wa hizo sheria wao na walikuwepo.
3. Uvunjaji wa sheria haukufanyika overnight kama muujiza.Umefanyika waziwazi na wenye kusimamia sheria waliangalia tena kwa kipindi kirefu hadi majengo yakamalizika, yakahamiwa na "kudumu" kwa miaka mingi hadi kuzoeleka kama sehemu ya mandhari ya DSM!
4. Serikali inapoangalia uhalifu ukitendeka au uvunjaji wa sheria ukifanyika mbele ya pua yake yenyewe na kukaa kimya miaka yote inamaanisha nini?
5. Haiingii akilini kuja leo na kutamka au kudhamiria kuyavunja.Huwezi kila siku ukachezea rasilimali adimu kwa taifa "linalojitakia" umasikini lenyewe halafu wananchi wake waone mantiki hata kama ni kusimamia sheria - ITS TOO LATE ndicho asemacho mwanzisha mada.

Bila hata kuingia kwenye mantiki ya kisheria katika jambo hili, binafsi hata mimi napata shida sana siyo tu katika hili la kuvunja majengo kama hili la TANESCO bali katika muktadha mzima wa usimamizi na utekelezaji wa sheria Tanzania.Nina uhakika kabisa kama tungejenga utamaduni wa kuwa na "PREVENTIVE LAWYERING" ambapo wanasheria na wenye kusimamia sheria - hasa wale waliopewa dhamana hii wangechukua hatua kuzuia badala ya kusubiri madhara yatokee ndipo tufanye rejea kwenye misahafu ya sheria kuona inasema nini, tungeokoa pesa na rasilimali nyingine na huenda ingepunguza umaskini katika ngazi hata za familia.Fikiria namna watu wanavyovamia maeneo wakajenga huku serikali ikiwaangalia.Wanamalizia rasilimali za familia katika ujenzi.Kisha serikali inaamka kutoka usingizi wa pono na kuandika kwa wino mwekundu BOMOA na X juu! Je hii inaingia akilini kweli?

LETS BE SERIOUS FOR ONCE!

Nawasilisha!
WoS
 
Nyie mbona mnadiscuss ujinga? mnalijua lile gorofa la masaki lililobomolewa kwa kuwa kule hakukutakiwa kuwepo jengo lefu kama lile? mnajua gharama za jengo lile? Nyie ni wafuasi wa serikali ambayo inawaonea wananchi na nyie mmekubali. Sheria haijalishi serikali au mtu binafsi. Unaponibomolea kijumba changu kidogo ni sawa na yule unayembomolea gorofa. Mmeshafanya projection in twenty five years mahitaji ya ile bara bara yatakuwaje?
Magufuli yuko sawa myie ndio mmepotoka


Hapo umepiga penyewe nakupigia salute.
 
Jamani bosi wake aliahidi hili........

SpagettiJuncREX_468x344.jpg
 
Mbona Nyaya Za Umeme Kwa Yule Mchungaji Wa Pale Mwenge aka Kakobe Hamkusema Zikwepeshwe? Hamkuona Pale Kuna Maelfu Ya Maisha Ya Watu Wakati Wa Ibada. Mkasimamia Sheria Na Nyaya Zikapita Pale Pale...
Vunja Maguguli Vunjaaaaa!!!
 
Mimi nilitegemea mpaka sasa hivi PM au JK mwenyewe wawe wamesha ingilia kati kuwawajibisha waliobariki ujenzi kweye hizo road reserves na kuitia hasara serikali lakini wapi bana....wako kiiiimya!! Matokeo yake sakata lote hili linaonekana kuwa ni la Magufuli peke yake!!

Ama kweli la kuvunda halina ubani!
HAKUNA ALIYEBARIKI, UKWELI NI KUWA MASTER PLANA YA JIJI LA DAR ES SALAAM YA 1979 INATAMBUA ROAD RESERVE NI FUTI 75 KAMA INAVYOTAMKWA NA IBARA YA 2 YA SHERIA YA KANUNI ZA SHERIA YA BARABARA YA 1967 (TAZAMA KIELELEZO KIMEABATANISHWA)) HIVYO JENGO LA TANESCO NA WOTE WALIOJENGA NJE YA FUTI 75 WAKAO HAPO KAHALALI.

BOMOA BOMOA UBUNGO HADI KIRUVIA

Ibara ya 2 ya Kanuni za Sheria ya barabara (Tangazo la Serikali Namba 161 la tarehe 5/5/1967) inatamka kuwa hifadhi ya barabara kuu zote hapa nchini (Trunk roads) ni Futi 75 kutoka katikati ya barabara. Vivyo hivyo Ibara ya 29 ya Kanuni za Sheria mpya ya barabara namba 13 ya 2007 (Tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009) (a) inatamka kuwa eneo la hifadhi ya barabara zote Kuu (Trunk Roads) za njia moja (Single Carriage way); na (b) kwa njia mbili (Dual Carriage ways) eneo la hifadhi barabara litakuwa ni Mita 60, yaani Mita 30 kila upande kutoka katikati ya barabara.

Ibara ya 27 ya Kanuni za sheria mpya ya barabara zilizotajwa hapo juu zinatamka kuwa upana wa njia moja ya barabara (lane) kwa barabara ya njia moja utakuwa si chini ya Mita 3.25 kwa njia moja ya kuelekea upande mmoja. Hivyo katika upanuzi wa barabara ya Morogoro, Mita 60 za hifadhi ya barabara zilizotengwa kama ilivyoelezwa hapo juu, zina uwezo wa kuzalisha njia 18 za barabara zenye upana uliotajwa hapo juu, yaani njia 9 za barabara za kutoka DSM kwenda Kibaha, na 9 za kutoka Kibaha kuja DSM.

Hivyo madai ya Wizara ya Miundo Mbinu kuwa msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro katika DSM na Kibaha husababishwa na wananchi waliojenga nyumba za makazi katika eneo lililo nje ya Mita 60, zilizotengwa kama hifadhi ya barabara hayana ukweli wowote. Eneo lililo nje ya Futi za 75 kutoka katikati ya barabara kwa mujibu wa Kanuni zilizotajwa hapo juu za 1967 liligawiwa kwa wananchi wakati Serikali ya awamu ya kwanza ilipokuwa kitekeleza sera ya Operesheni Vijiji.

Kimsingi Kanuni za Sheria ya barabara ya 1967 zilizokuwa zikitenga upana hifadhi ya barabara unaozidi Futi 75 (kati ya Mita 90 hadi 120) kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha zilikoma baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungo wa Tanzania kupitisha kwa Sheria inayolinda ugawaji wa ardhi uliofanyika chini ya operesheni vijiji kati ya Tar 01 Januari 1970 hadi kuanza kutumika kwa Sheria ya Ardhi namba 5 ya 1999 (Vifungu 15 na 16 vinatamka kuwa ugawaji wa ardhi uliofanywa mahali popote katika kijiji chini ya operesheni vijiji hata kama ni kwa kukiuka sheria yoyote ni halali na wenye kutoa haki ya wagawiwa kumiliki ardhi husika………).

Hivyo kitendo cha Wizara ya Ujenzi kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi Mita 90 hadi 120 pande zote mbili za barabara uliofanyika mwaka 2001, kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha na kupanda wa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara ya Morogoro pasipo kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa na Serikali za Mitaa ambazo zinzwafahamu na kuwatambua wananchi wanaohusika na sheria ya ardhi ya vijiji iliyotajwa hapo juu ulifanyika kimakosa na kusababisha athari kubwa sana za kijamii na kiuchumi kama vile kuwakosesha wananchi maeneo ya kutengeneza fursa za ajira, kujiajiri, huduma kama vile za kibenki, ATM n.k.

Mwaka 2010,ikiwa ni miaka 9 tokea uingiaji huo haramu, kitendo cha TANROAD kwa maagizo ya Wizara ya Miundo Mbinu kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi zaidi ya Futi 75 au Mita 22.86 na kufanya maendelezo yoyote ikiwemo ni pamoja na kuweka alama za X katika nyumba za wananchi ni haramu na ni cha kuwanyanyasa wananchi.
 
Matatizo bado hatujayaona!
Tutavunja kila mahali. Jenerali Ulimwengu miaka ya nyuma alipokuwa mbunge aliwahi kusema Bungeni kuwa ili DSM iweze kuwa na mpangilio mzuri unaoeleweka na mambo yaende vizuri, basi itabidi kuvunja karibu jiji zima! Hii ni zaidi ya miaka 20 iliyopita.Hebu tujiulize, ina maana miaka yote serikali ilikuwa imelala? Kipindi kile kama ingesikia na kufanyia kazi maoni na hat aushauri wa wataalamu yote haya tunayoyaona yasingetupata.Kipindi kile nadhani hata hili jengo la TANESCO lilikuwa halijajengwa! Ni mangapi serikali inapuuzia? Yanatugharimu sasa.
 
Nyie mbona mnadiscuss ujinga? mnalijua lile gorofa la masaki lililobomolewa kwa kuwa kule hakukutakiwa kuwepo jengo lefu kama lile? mnajua gharama za jengo lile? Nyie ni wafuasi wa serikali ambayo inawaonea wananchi na nyie mmekubali. Sheria haijalishi serikali au mtu binafsi. Unaponibomolea kijumba changu kidogo ni sawa na yule unayembomolea gorofa. Mmeshafanya projection in twenty five years mahitaji ya ile bara bara yatakuwaje?
Magufuli yuko sawa myie ndio mmepotoka
Ni kweli Mheshimiwa John Pombe Makufuri anafuata sheria, lakini si wanaweza kubadili kidogo ramani ili kuepuka kuitia nchi hasara, wakajenga hizo bararabara kando kidogo??????? Unakumbuka jengo la SUKA MOTEL pale Kimara, si walipindisha kwa kuwa wale ni waasisi wa nchi hii.
Makufuri anafanya kazi nzuri saana na huwezi kumwita eti ni mwendawazimu, yeye anafuata sheria, ila tunamuomba busara pia itumike kwa swala hili la mijumba ya TANESCO Ubungo!!!!!!
 
morogoro highway na mandela express way ni muhimu zaidi kuliko jengo la tanesco.
ukitaka kumwua nyani usimtazame usoni utamwacha na kesho utajutia kukuta mabua tu shambani. Usitazame uzuri wa jengo ila fikiria mfumo wa miundombinu ya uchumi wa nchi. Kiasi gani cha pesa kinapotea kwa sababu miundombinu mibovu.
Kwa aliyebuni ujenzi wa jengo la tanesco pale ni sifuri kwa vile hakuwa na upeo mkubwa wa kuangalia miundombunu mingine na lazima litabomolewa tu.

kubomoa ni kwa kulipa fidia kwa kuwa sheria upana wa hifadhi ya barabara anaosema magufuli ni wa 1967, na umepitwa na wakati na matukio. Master plan ya jiji la dar es salaam inatambua road reserve kuwa ni futi 75 tu kama inavyotamkw ibara ya 2 ya kanuni za sheria ya barabara ya 1967, na ni kwa kutumia master plana hioyo ndio tanesci walipatiwa hati miliki na buliding permit. Hivyo hakuna sheroia yoyote iliyovunjwa hico ni prpaganda za magufuli kujitafuti umaarufu wa kugombea urais 2015 tu.

Mita 60 za hifadhi ya barabara zinzatosha kuzalisha lane 18, 9 za kwenda kibaha na mjini. Kwanini awaguse walioko nje ya mita 60 kama sio kutafuta ummaarufu kwa kuwaumiza wengine.
Mradi wa mabasi ya kwenda kasi ulilipa fidia 2008 kwa wote walioko katika meneo hayo na fidia hizo ziliwahusu mpaka wapangaji, na wote waliokuwa wakitumia majengo hayo kwa shughuli za kiuchumi, mama ntilie alitoka na mgahawa na mwenyue grocery alitoka na baa. Ndio maan unaona hakuna anayelalamika kati ya ubungo hadi magomeni, wote walilipwa fidia. That is the precedence
 
ni kweli mheshimiwa john pombe makufuri anafuata sheria, lakini si wanaweza kubadili kidogo ramani ili kuepuka kuitia nchi hasara, wakajenga hizo bararabara kando kidogo??????? Unakumbuka jengo la suka motel pale kimara, si walipindisha kwa kuwa wale ni waasisi wa nchi hii.
Makufuri anafanya kazi nzuri saana na huwezi kumwita eti ni mwendawazimu, yeye anafuata sheria, ila tunamuomba busara pia itumike kwa swala hili la mijumba ya tanesco ubungo!!!!!!

hakuna sheria yoyote anayofuata mhe john magufuli. Sheroa ya barabara ya 1967 ilifutwa na sheria ya ardhi ya vijiji namba 5 ya 1999. Soma attachments hapa chini, anatumia mabavu tu. Bwana johnsecond anauliza kuhusu projection za barabara ya morogoro. Ilifanyika mwaka 2009 ambapo kanuni za sheria hiyo zinasema neo la hifadhi ya trunk road zote hapa nchini single and dual carriage ways ni mita 60 tu.

Kabla ya hapo sheria ya 1967 anayotumia magufuli ilifutwa na sheria ya ardhi ya vijiji namba 5 ya 1999, hivyo wananchi waliogawiwa ardhi na malaka za vijiji wana haki ya kulipwa gfidia kama magufuli nahitaji ardhi zaidi ya futi 75.
 
nilishasema tena na tena, watu ambao hawajasomea ujenzi na zaidi zaidi hawajasomea vitu kama urban planing na mwisho kumalizia kwa kusema mtu ambaye hajasomea road design, ni heri ukanywe maji na ulale salama.

Nashukuru kwa wale ambao wanachangia na unaona kweli ingawa hajasomea haya mambo, lakini kichwani zinachemka.

Mtu anakuja na kusema kuwa hapo kwenye jengo, basi barabara ipindishwe, khaaaa!!!!!

Kwenye barabara za mijini na mitaa, huwa ni zaidi ya barabara kama nyie mnavyoona.

Kuna siku, huko pembeni ndiyo kutajengwa drinage systems za maji machafu kutoka majumbani na ya mvua kutoka barabarani na kwenye majumba ya watu. Hii inapunguza maji kuzagaa ovyo na kutengeneza mazalia ya mbu.

Huko pembeni, kunatakiwa kuwe na mabomba ya nyaya za umeme, simu, internet, tv cables etc. Haya mabomba, yanatakiwa kuna umbali fulani kutoka bomba moja kwenda jingine.

Huko pembeni, siku moja itabidi kuweka bomba la njano, yes, bomba la gas. Hili nalo linataka umbali kadhaa kutoka kwenye mambomba mengine na umbali kadhaa kutoka mwisho wa lane za barabara.

Siku moja, wataweka bomba kubwa sana la maji kutoka mlandizi/ruvu juu. Hili nalo kwa sababu za kiusalama, inabidi liwekwe umbali kadhaa kutoka kwenye mambomba mengine na mwisho wa barabara.

Sasa jengo karibu namna hiyo, hebu fikiri likichimbwa na kutandikwa bomba la gas, likilipuka hapo, si jengo zima na watu ndani yake watakaangwa? Hivi nyie mnaishi karne ya ngapi?

Kitu pekee ambacho magufuli anachemsha ni kuwa, inabidi awaulize wajenzi, ni nani hasa aliruhusu ujenzi kuwa karibu namna hiyo na barabara? Akipatikana basi yeye na mali zake wafilisiwe. Hawa ndiyo wanaotia aibu fani ya ujenzi. jitu linakurupuka na kujenga vitu ndani ya barabara bila ya kujua, kuna siku barabara ile inabidi zijengwe hata lane 8 kuingia mjini na 8 kutoka mjini. Sasa kukiwa na lane hata 10 tu, inamaana 10x3=30m. Hapo ongeza na pavements, sehemu za waendesha baiskeli, na za kuweka hizo bomba hapo juu, tayari uko ndani ya jengo la pili.

Wanasiasa wameharibu sana fani ya ujenzi. Mtu kama mwiba angelikuwa rais, ndiyo walewale. Kuhalalisha kosa kwa sababu tu kulisahihisha ni aghali sana. Watu wanatakiwa kuwa wanafilisiwa ili kufidia gharama, basi watakuwa mahiri na kazi zao.

kanuni za sheria ya barabara ya 1967 inatamka wazi wazi kuwa reserev yatrunk roads zoite hapa nchjini ni futi 75 tu, hiyo ilikuwa captured kweny mastyer plan ya jiji la dar es salaam ya 1979. Kumbuka wakati huo ilikuw ahairuhusiwa kununua magari, siku ya jumapili magari yanatembea kwa kibali maalum ili kukoa mafuta na foreign exchange.

Hivyo kam sasa tymeruhusu every tom dich and harry anunue gari ndio barabar zikajaa, ili kuwa na miundo mbinu ya kutosheleza magari hayo kinachotakiw ani kuliopa fidia kama zile picha za majengo ya kenya alizotuwekea mchangiaji mmoja. Anachokosea magufuli ni kugezu sheria kama "menu katika migahawa ambapo mlaji huchagua chakula atacho na kuacha kle asichiopenda, na kutumiapropaganda na ubabe.
Soma attachemnts
 
images
74022114.jpg
images
images
images
images
images
images
images
images
images
images
images


taswira hizi zinaashiria wazi ujenzi wa miundombinu umeathiri mengi ikiwa ni majengo na makazi ya watu, uzuri huo ni kutokana na sacrifice otheri wise we can't get development we are dreaming daily. Watoto wetu wataabike kama tunavyotaabika? La hasha lazima kujitosa sasa.

sacrafice zinzotakiwa ni kuwa tayari kuwalipa fidia wenye majengo yao kama picha za majengoi yatakayoathirika kule kenya alizotuwekea mchangaji mmoja. Mbona mradi wa mabasi yaendayo kasi uliwalipwa fidia jamaa wote kati ya kimara hadi magoemni? Iweja mzungu awe na utanbuai wa sheri zetu wenyewe na haki za binadamu za watu wetu wakati sisi wenyewe tunashabikia kuvunjwa kwa hakli za binadamu za wananchi wetu?
 
Huku 'Tanesco Ubungo' na huku 'Ubungo Maji' na vyote ni vya umma....'patamu' hapo!

- Wote Tanesco Ubungo na Ubungo Maji wamejenga kwenye road reserve...hili halina ubishi bila shaka.
- Ukiacha Tanesco na Maji, wapo pia watu wengine wengie kando ya morogoro road waliojenga ndani ya road reserve...hili pia lipo wazi
- Barabara ya morogoro ni lazima ipanuliwe ili kupunguza msongamano wa magari ambayo inaleta sio tu adha kwa watumiaji lakini pia hasara kubwa kwa taifa sasa na hata baadae...hili pia halina ubishi.

Ukibomoa majengo mengine yote yaliyojengwa ndani ya road reserve na kuziacha Tanesco na Maji kama zilivyo na kisha ukafanya upanuzi wa barabara hiyo sehemu nyingine tu bado tatizo la msongamano halitapungua kwa sababu hiyo sehemu ya Tanesco na Maji itakuwa ni 'bottleneck' katika barabara ambayo kimsingi ndio kwa sehemu kubwa ina determine flow speed ya magari. Hata kama utapanua barabara inayoleta magari nane kwa pamoja laki halafu yakifika ubungo inabidi yapite mawili tu kwa mara moja, then overall barabara nzima ni kama inaendelea kupitisha magari mawili kwa wakati mmoja.

So kimantiki na hata kisheria huwezi kubomoa majengo mengine yote yaliyojengwa kwenye road reserve ya morogoro road halafu uiache tanesco na maji vikisimama halafu utegemee kufanya upanuzi wa barabara wenye tija! Pengine huo ndio mimi naona utakuwa uwenda wazimu zaidi.

Wangeweza kufikiria kuhamisha barabara ili kukwepa eneo la Tanesco na Maji lakini kwa upeo wangu mdogo option hiyo itakuwa costful kwa sababu watatakiwa kuwaliopa watu fidia ambayo kwa hakika itazidi hiyo majengo mazuri ya Tanesco na Maji hapo ubungo.
 
Huku 'Tanesco Ubungo' na huku 'Ubungo Maji' na vyote ni vya umma....'patamu' hapo!

- Wote Tanesco Ubungo na Ubungo Maji wamejenga kwenye road reserve...hili halina ubishi bila shaka.
- Ukiacha Tanesco na Maji, wapo pia watu wengine wengie kando ya morogoro road waliojenga ndani ya road reserve...hili pia lipo wazi
- Barabara ya morogoro ni lazima ipanuliwe ili kupunguza msongamano wa magari ambayo inaleta sio tu adha kwa watumiaji lakini pia hasara kubwa kwa taifa sasa na hata baadae...hili pia halina ubishi.

Ukibomoa majengo mengine yote yaliyojengwa ndani ya road reserve na kuziacha Tanesco na Maji kama zilivyo na kisha ukafanya upanuzi wa barabara hiyo sehemu nyingine tu bado tatizo la msongamano halitapungua kwa sababu hiyo sehemu ya Tanesco na Maji itakuwa ni 'bottleneck' katika barabara ambayo kimsingi ndio kwa sehemu kubwa ina determine flow speed ya magari. Hata kama utapanua barabara inayoleta magari nane kwa pamoja laki halafu yakifika ubungo inabidi yapite mawili tu kwa mara moja, then overall barabara nzima ni kama inaendelea kupitisha magari mawili kwa wakati mmoja.

So kimantiki na hata kisheria huwezi kubomoa majengo mengine yote yaliyojengwa kwenye road reserve ya morogoro road halafu uiache tanesco na maji vikisimama halafu utegemee kufanya upanuzi wa barabara wenye tija! Pengine huo ndio mimi naona utakuwa uwenda wazimu zaidi.

Wangeweza kufikiria kuhamisha barabara ili kukwepa eneo la Tanesco na Maji lakini kwa upeo wangu mdogo option hiyo itakuwa costful kwa sababu watatakiwa kuwaliopa watu fidia ambayo kwa hakika itazidi hiyo majengo mazuri ya Tanesco na Maji hapo ubungo.

MIMINAPINGA KUWA TANESCO A MAJI HAWAJAJENGE KWENYE ROAD RESERVE. KUMBUKA ANAYOTUMIA NI KANUNI TU, ILIHALI MASTER PLANA YA JIJI LA DAR ES SALAAM IMETENGENEZWA KW AMUJIBU WA SHERIA ZILIZOTUNGWA NA BUNGE NA KUZIPATIA MAMLAKA ZA MIJI NA WILAYA NA MADIWANI MADARAKA YA KUTENGENZA NA KUPITISHA MASTER PLAN YA JIJI KAMA LA DAR ES SALAAM, AMBAYO INATAMBUA KUWA ROAD RESERVE NI FUTI 75 NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM. hIVYO TUACHE KUSIKILIZA PROPAGANDA NA WISHFUL THINKING ZA MAGUFULI.

NDIO MAANA WAFADHILI WA DART WALILIPA FIDIA WATU WOTE WALIOKUW KTK ROAD RESERVA KATAI YA KIMARA HADI MAGOMENI. WAO SIO WAJINGA HAWAKUTAKA MAMABO YA KUCHELEWESHANA MAHAKAMANI.
 
MIMINAPINGA KUWA TANESCO A MAJI HAWAJAJENGE KWENYE ROAD RESERVE. KUMBUKA ANAYOTUMIA NI KANUNI TU, ILIHALI MASTER PLANA YA JIJI LA DAR ES SALAAM IMETENGENEZWA KW AMUJIBU WA SHERIA ZILIZOTUNGWA NA BUNGE NA KUZIPATIA MAMLAKA ZA MIJI NA WILAYA NA MADIWANI MADARAKA YA KUTENGENZA NA KUPITISHA MASTER PLAN YA JIJI KAMA LA DAR ES SALAAM, AMBAYO INATAMBUA KUWA ROAD RESERVE NI FUTI 75 NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM. hIVYO TUACHE KUSIKILIZA PROPAGANDA NA WISHFUL THINKING ZA MAGUFULI.

NDIO MAANA WAFADHILI WA DART WALILIPA FIDIA WATU WOTE WALIOKUW KTK ROAD RESERVA KATAI YA KIMARA HADI MAGOMENI. WAO SIO WAJINGA HAWAKUTAKA MAMABO YA KUCHELEWESHANA MAHAKAMANI.


So unachosema sio tu Tanesco na Maji bali wote kando ya morogoro road hawajajenga ndani ya reserve? Hata kwa kuangalia tu kwa macho huwezi kuona tofauti kati ya jengo la Tanesco na mengine ambayo yameshawekwa "X". Kwa mfano huwezi kusema tanesco ipo nje halafu hapo hapo ukasema lile kanisa (walikuwa wanaliita la misukule!) lipo ndani ya reserve!

Kwa hiyo unachotaka kutuaminisha ni kuwa kanuni anazotumia Magufuli hazipo kwa mujibu wa sheria?
"We know of some of the government buildings which are on the road reserves such as, Tanesco Headquarters and the Ministry of Water offices. If need arise, these structures will be demolished as well," he said.

Dr Magufuli said that as a minister he took oath to observe the law and that to show his ministry's seriousness on the matter, they have already demolished the Dar es Salam-Tanzania National Roads Agency (TANROADS) regional offices at Ubungo to pave way for expansion of commuter buses' stand.

He noted further that, his ministry will continue to ensure that all the roads under Tanroads are free from haphazardly raised billboards, saying that the revenue acquired from the business was nothing when compared to trouble that is being caused by them.

Source: Daily News Online edition
 
hivi wewe ujenge barabarani na kutupa tabu wengine,kwa sababu ya upuuzi wako usiokuwa na msingi
km zimejengwa ndani ya barabara zivunjwe tu,sheria msumeno,zingekuwa za mtu binafsi si mngeshangilia na kusema avunje sababu lazima kuna ufisadi ulifanyika,basi hata hizi zinapaswa kuvunjwa pia

tatizo serikali yetu kila sehemu na kila kitu ni dili,waliosababisha hayo wachukuliwe sheria na maghorofa yavunjwe,mbona za Masaki mlivunja

Vunja baba,mapunguani ni hao wanaojenga barabarani
 
Nakumbuka msemo wa kikwetu usemao "...Ukimsifu mgema tembo hulitia maji...! Magufuli amesema yale majumba ya shirika la umeme yanayoleta mandhari ya aina yake hapa jijini yaliyojengwa kwa mabilioni ya shilingi ni lazima yavunjwe eti yamejengwa kwenye sehemu iliyohifadhiwa kwa ajili ya kupita barabara.

Huyu mtu kama hana wazimu atakuwa na kitu gani hivi anafikiria hela iliyotumika ni hela ya serikali, ? Au ya shirika la umeme ,akili za watu wengine zinakuwa za ajabu ajabu ,anachotaka ni kuwapa tanesco eneo jingine wajenge upya ,kwa maana kwa dau hilo hela ingine itapatikana na wajanja kupata chao.

Mtu huyu alikuwa wapi wakati majumba hayo yakijengwa ?Serikali ilikuwa wapi ?
Tanescobuild.jpg
Unaenda kuvunja mijumba hiyo kwenye nchi ambayo uchumi wake ni wa kubahatisha au wakuu mnataka na kutafuta njia mbadala ya kufanya ufisadi,

jamani magufuli atawali kwa kufuata sheria na katiba yake anafuata sheria na katiba ya Jtz,na aliapa kuuheshimu na kuitii,tatizo watanzania mnapenda mtu awe magumashi akifuata sheria mwamuona . .
 
Akivunja hili jengo nitamwona punguani!
Kuna tatizo gani hiyo barabara ikikwepeswa? Kama ana ubavu Ajenge ipite chini au juu. kama ni lazima ipite hapo.

Hivi si ni wewe pia unaelalamika kuwa dar kuna foleni!!!! hivi unafikiri kwa kutumia makalio au???? Tuache ujinga jamani. Kama hilo jengo lilijengwa katika eneo la barabara ni LAZIMA LIVUNJWE. Kwani ni Magufuli ndiye aliyeidhinisha kujengwa kwa jengo jilo? Alaa! Ni lazima tufike mahali ambapo kila mtu atawajibika kwa analofanya. Hata sie wananchi wakati mwingine pia tunasababisha mambo kama haya kutokea. Wacha livunjwe ili mtu ukitaka kujenga jengo lazima ufate taratibu zote. Si ajabu hata hao Tanesco walijua fika kuwa pale ni eneo la hifadhi ya barabara ila wakalazimisha kujenga kisa tu ni ofisi ya serikali. Sheria ni msumeno hakuna cha nani wala nani. Uzembe kama huo si wa kuuacha uendelee na pia ni mfano hata kwa taasisi nyingine za serikali zisione kama zenyewe zipo juu ya sheria.
Hongera Magufuli kwa kuonyesha mfano. Toa boriti jichoni mwako ndipo utoe kibanzi jichoni kwa mwenzio...
 
Back
Top Bottom