Waziri Jenister Mhagama kumbuka ahadi yako kuhusu pensheni ya PSSSF kwa watumishi siku ya Sabasaba

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Tuna kukumbusha Mhe. Waziri Jenister Mhagama siku ya sabasaba ukiwa na mkurugenzi mtendaji wa PSSSF kwenye banda lao, mlisema kwa sasa mnafanyia kazi marekebisho ya malipo na maelekezo ya Mhe Samia Suluhu Hassan kuhusu kuwalipa wastaafu.

Walio staafu kuanzia mwezi 3 hadi sasa hawajalipwa, je ni siasa mnaifanya majukwaani au ni utendaji wa kweli. usisahau mhe jenister mhagama kwamba swala la kikokotoo ni wewe ulikisimamia kidete kuwa kitumike wananchi wakalalamika sana sana.

Tunaomba hizo pensheni mliahidi mtu akistaafu haitazidi mwezi watakuwa wamelipwa sasa ni tofauti na kauli zenu za kwenye mikutano ya ndani na nje. Ninyi kama Mawaziri haiwahusu maana mnapewa chenu mapema ila sisi wananchi watumishi tunaumia sana.

Rekebisheni tafadhali vinginevyo tutakushtaki kwa wananchi wa PERAMIHO
 
Back
Top Bottom