Waziri January Makamba unakwenda kufeli kutokana na sababu hizi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nikiri January ana uwezo mkubwa wa akili ila siyo mjuvi wa mambo yote. January siyo mtaalamu ila ni Kiongozi wa kisiasa. Januari anazo sifa zote za Kiongozi wa kisiasa lakini Hana sifa zote za Kiongozi wa taasisi. Ana mapungufu, na mapungufu aliyonayo ndiyo yaliyopelekea muundo wa taasisi za serikali na binafsi kuchagua kuajiri watu mabalimbali katika maeneo mbalimbali ya taasisi ili waweze kumsaidia huyu binadamu ambaye ajakamilika anayeitwa Mkurugenzi,Waziri au vyovyote aitwavyo.

Wataalamu wa utawala na uongozi wakaenda mbele zaidi wakasema taasisi ikikosa team work uingia kwenye one man show au group of who they think themselves as exceptional from others. Kwa kiswahili chepesi taasisi ikiongozwa na mtu anayejiona ana jua kila kitu ufanya taasisi hiyo ififishe maono ya wengi na mwisho wake team work uondoka na taasisi kufa au kudidimi. Kwa maneno mengine ukiwa na kiongozi anayejiona ana exposure na anajua vingi basi mara nyingi uzaliwa udikteta. Kama kiongoz anajua kila kitu basi ukimpinga itabidi ukae pembeni usubiri siku utakapokuwa kiongoz ndipo utekeleze yale unayohisi anafanya sivyo.

January kuanguka kwake kunakwenda kuchangiwa na tabia ya kujua kila kitu. Tabia hii isipobaki kwenye nafsi yake ikaingia kwenye uso wa wizara na taasisi zake ambazo Zina wataalamu wengi Basi maono yake yatadumu na maono ya wengine kufifishwa. Lazima akubali kuwa msikilizaji sana lakini anaposikiliza ajitahidi Sana anayoyasikiliza yasimwondoe kwenye mpango wake au mpango wa wizara ila yabaki kuboresha kwenye kile anachoota.

Kujifanya unajua sana kunapelekea usijifunze sana na hivyo kubaki ukidhani unajua kuwa ulikuwa unajua ila kwa wakati uliopo ujui.

Jisahihishe uongoze watu kulingna na vipawa vyao na si kuongoza watu kulingana na vipawa ulivyonavyo. Believe on team work backed up with participatoery leadership
 
Hivi ulifufuka kumbe? Anyway, nausha ya dunia hii ni mafupi sana, kupata mda wa kuonea wivu mafanikio ya wenzako, badala ya kupambana
 
Sidhani kama uko sahihi. Nahisi imekaa kwenye mlengo wa kumchafua Waziri ambaye amehudumu kwa muda mfupi kwenye hiyo nafasi! Mh. January hana ujuaji unaousema kwa muda mfupi aliopo kwenye MoE hajaonyesha hayo,ndio kwanza ametoa dira na matumaini ya kuanza upya
 
Team Mwigulu vs Team January.

Kwanini Team Mwigulu mnamwogopa sana huyu kijana?

Mpeni muda.

Wewe Mwigulu umeshachambia upupu kwa matozo yako yasio na utu.
 
Mkuu, Kwanza nikupinge kwa kusema kuwa January Makamba anajiona anajua kila kitu, Hilo nakataa kabisa, January ni humble na Msikivu sana pamoja na kuwa na exposure kubwa ila still bado kijana ata lead hii Wizara kwa mafanikio makubwa, Asafishe masalia ya Waliopita ili wasije kumkwamisha
 
January simkubali tu, ile tabia aliyoonesha enzi za Magufuli kimsingi nilimuona ni selfish, kumchora kwenye vile vikatuni kwangu ilionesha alikuwa analalamika hapewi zaidi ya anavyostahili akiamini yeye ndie aliemuweka Magufuli madarakani kwa mchezo wao walioufanya kule Masaki wakati ule.

Ukiondoa kubebwa na jina la baba yake, bado sijauona utendaji wa January unaomfanya awepo serikalini kila awamu, ile wizara ya Muungano alipewa na Magufuli ilimshinda hakuna alichofanya, na alistahili kutumbuliwa, tatizo lake wanajiona wana hati miliki ya kuwa viongozi wa nchi hii mpaka kuota ndoto za kuwa Rais.

- Historia yake huko shuleni nayo sio nzuri, inasemekana aliiba mitihani na hajawahi kukanusha, hii peke yake ingetosha kumuondoa kabisa serikali, lakini kubebana na kuiba kwake kura ili wengine washinde ndio salama yake.

Kumuita msomi kama vile ndie pekee aliepo nchini kwa sasa ni uvivu wa kufikiri, kama taifa tunao wasomi wa kutosha wanaostahili kupewa hizo nafasi tuone utendaji wao, kuliko kurudia sura zilezile zilizofeli kila siku ndio maana hatusogei popote, tatizo wanawajaribisha kidogo then wanawaondoa wanawarudisha walewale.
 
Naona mada za kumsiliba Makamba humu zinazidi kung'aa kila uchao.
 
Mkuu, Kwanza nikupinge kwa kusema kuwa January Makamba anajiona anajua kila kitu, Hilo nakataa kabisa, January ni humble na Msikivu sana pamoja na kuwa na exposure kubwa ila still bado kijana ata lead hii Wizara kwa mafanikio makubwa, Asafishe masalia ya Waliopita ili wasije kumkwamisha
Huo usikivu January kaupata lini? Inawezekana humjui kabisa
Huyo January alifikia kipindi akawa anatoza watu pesa kuwakutanisha na raisi
Bure kabisa huyo
 
Back
Top Bottom