Waziri January Makamba hana msaada wowote kwenye Wizara ya Nishati. Tumechoka!

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Itoshe tu kusema kwa sasa hatuoni faida yoyote ya waziri wa nishati, huduma mbovu na za hovyo za sasa kwa mara ya mwisho tuliziona miaka ya 2012 huko

Hapa nilipo mpaka sasa hakuna umeme tangu saa mbili asubuhi sasa hivi inaelekea saa 12 jioni hakuna umeme,

Mnategemea sisi wananchi tutafanyaje uzalishaji?

Watu wana mitambo ya tofali wengine welding watu wana stationary na vengine vingi siku nzima umeme hakuna mnataka tuishije? na hiii sio mara ya kwanza ni mazoea sasa

Sasa hivi imezoeleka mtu ibapita siku nzima hujazalisha hata shilingi mia sababu ya umeme,

Mbona kama mnatulazimisha tumkumbuke Magufuli?

Tukiongea mnasema watanzania wamezoea kulalamika mbona hatuambiwi sababu ni nini ya mgao wa umeme?

Mi naomba niulize hivi huu mgao wa umeme ulikuwa umesubiri kalemani atoke ndio uanze?

Tunajuta ni bora hata angebaki Medard Kalemani

Makamba hamna kitu kabisa

CCM sio wa kuendekeza tena, tumechoka tumechoka
 
Mkuu uko arusha, sababu huku maeneo ya kjenge mwanamana toka udubui kitu hakipo kazi haziend,tunatzamana kama madume ya nyani.
 
Binafsi siamini kuwa ni ntu wa dili na kukatika umeme ni mpango wa kusambaza majenereta.

Naamini hatoniprove wrong na hili suala litakuwa stable. Atashinda haka kavita ninakokafikiri anapitia.
 
Watu wapo pale Tanesco kwa mambo yao... January,Mafuru,Maharage,Nehemia ni lethal combination....
Nikuhakikishie JPM angekuwa hai hili jambo lingekuwa tofauti sana....
Personally nakubali kwenye usimamizi JPM was real deal.
 
Back
Top Bottom