Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,113
- 33,621
Kama Waziri wa nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Waziri Suleiman Jafo unayo fursa pekee ya kuzuia Rais John Magufuli kudhalilishwa na Uhuni unaofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya wananchi wa Iringa.
Jafo wewe ni "Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais" au kwa maana nyingine ni Waziri mdogo wakati Waziri mwenyewe akiwa ni Rais Magufuli. Inaposemwa Waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa, huwa inamaanishwa anayetajwa ni Rais na siyo wewe.
Kwa maana nyingine mambo ya kihuni kama kumuondoa Meya wa Iringa kama ilivyo kwa yule wa Darisalama yasipochukuliwa hatua, huwa inaonekana ni kama Rais Mwenyewe ndiyo anayafurahia wakati kumbe wewe ndiyo unayepaswa kufanya maamuzi kwa wakati ili Rais asiabishwe.
Hapa Iringa Manispaa baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2015 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilipata viti 14 vya Udiwani dhidi ya viti 4 vya udiwani vya CCM. Kwa maana nyingine kwenye Kata 18 zilizopo CCM ilikataliwa kwenye Kata 14.
Lakini hapa kwa ufupi sana nitaelezea uhuni uliofanyika kuzuia Meya kuwa Meya kinyume cha sheria na ustaarabu!!
Meya wa Iringa ameondolewa bila ya kuwa na hoja za msingi za kuondolewa kwake wala ushahidi wa kuthibitisha tuhumu alizokuwa anatuhumiwa nazo. Kimsingi Alex Kimbe kisheria bado ndiyo Meya wa Iringa Manispaa.