Waziri Jafo: Wananchi nunueni Majokofu mapya yale ya mitumba yanachafua hali ya hewa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,559
Waziri wa mazingira mh Jaffo amewataka wananchi kuacha kutumia majokofu ya mitumba kwani yanachafua hali ya hewa na hivyo kuharibu mazingira.

Jaffo amesema ni vema wananchi wakanunua majokofu mapya kwa ajili ya usalama wa afya zao.

Source: Upendo tv

======

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Seleman Jafo amewataka watanzania kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kununua bidhaa rafiki wa Ozoni (Ozone friendly) ili kulinda tabaka la Ozoni dhidi ya uharibifu.

Waziri Jafo amesema hayo jijini Dodoma Septamba 16, 2021 alipofanya ziara kwenye maduka ya vifaa vya umeme pamoja na mafundi wanaojishughulisha na uuzaji na utengenezaji wa majokofu na viyoyozi katika maadhimisho yakupambana na kulilinda anga la hewa (Ozone layer).

Amesema ozoni ni tabaka la hewa ambalo liko katika anga la juu la pili lifahamikalo kitaalamu kama Stratosphere ambalo linaweka aina ya tabaka ama tambara angani ambalo linazuia mionzi mikali ya jua inayoweza kuleta athari katika afya za binadamu na viumbe hai kuja moja kwa moja duniani.

Amesema kuwa uharibifu wa tabaka la Ozoni unapelekea madhara mbalimbali duniani ikiwemo kuongezeka kwa kiwango cha joto duniani pamoja na kuleta mabadiliko ya tabia ya nchi jambo ambalo ni hatari kwa afya ya binadamu na viumbe hai.

Amewataka Wafanyabiashara kuacha kuuza Majokofu na Viyoyozi vya mtumba kwani vimeonekana kuleta athari kubwa katika vizazi vyetu vya sasa na vijavyo, wafanyabishara wengi wamekuwa wakiuza majokofu ya mtumba yalikuwa yakitumia gesi R 22 ambayo yalikuwa ikiharibu mazingira.

Jafo ametoa wito kwa vijana ambao wanaojishughulisha na masuala ya ufundi wa viyoyozi kwenye Majokofu ya mtumba kutumia aina ya gesi inayoruhusiwa na viwango vya kimataifa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Remidius Mwema ambaye alimwakilisha , Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema Dodoma inakuwa kwa kasi hivyo kuna haja ya kutengeneza jukwaa la pamoja litakalosaidia kutoa elimu kwa wananchi.

“Ni kweli wananchi wamekuwa wakinunua Majokofu ya mtumba ambayo yameonekana kuwa na madhara na hiyo yote inatokana na kutokuwa na uelewa juu ya madhara hayo lakini sasa kama tutakuwa na jukwaa la pamoja la kutoa elimu juu ya madhara ya bidhaa hizi za mtumba ninaimani bidhaa hizo za mtumba hazitanunuliwa,” amesema Mwema.

Naye, Fundi anayejishughulisha na Ufundi wa Viyoyozi Matukuta Juma amesema kutokana na ushauri huo watahamasisha wengine kutumia mitungi ya gesi inayokubalika huku akitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuwapunguzia gesi ambayo haiharibu mazingira kwani inauwza bei ya juu.

Chanzo: Mtanzania Digital
 
Waziri wa mazingira mh Jaffo amewataka wananchi kuacha kutumia majokofu ya mitumba kwani yanachafua hali ya hewa na hivyo kuharibu mazingira.

Jaffo amesema ni vema wananchi wakanunua majokofu mapya kwa ajili ya usalama wa afya zao.

Source: Upendo tv
Hayo ya zamani tuyapeleke wapi?
 
Ukweli ni kuwa used friji zilizojaa Hapa nchini Ulaya azitakiwi tena 1.zinakula sana Umeme 2.Zina Gesi Hatarishi zinazoharibu Ozone Layer....so sisi ni damping site..mbali na hizo friji pia kuna taka nyingi za kielectronic ambazo zinajaza nchi yetu bila faida bali hasara kwa mazingira yetu.
 
Waziri wa mazingira mh Jaffo amewataka wananchi kuacha kutumia majokofu ya mitumba kwani yanachafua hali ya hewa na hivyo kuharibu mazingira.

Jaffo amesema ni vema wananchi wakanunua majokofu mapya kwa ajili ya usalama wa afya zao.

Source: Upendo tv
Kwa nini hawazuii kuagizwa?
 
Kuna jambo linakosekana,na kwakuwa waziri sio mtaalamu wa mazingira au mhandisi.
1.Fridge mtumba sio lazima iwe na gesi za kuchafua mazingira,japo fridge nyingi ZILIZOUNDWA ZAMANI zina gesi ya kuchafua mazingira.
2.Gesi za kuchafua Mazingira zinazotumika katika mfumo wa fridge na Air-conditioned ni hizi hapa R12,R22,zimeishapigwa marufuku kwenye nchi nyingi.Lakini itumike busara kuziuhudumia fridge zilizo tiyari sokoni angalau miaka mitano lakini bila kuagiza gesi hizo.
3.Mfumo wa Fridge inayotumia gesi hizo zinazochafua mazingira unaweza kubadirishwa kwa kubadirisha baadhi ya vifaa kama Thermal Expansion Valve au kufanya settings ikidhi hizo gesi masingira.
4.Gesi inayochafua mazingira haina madhara kama haitavuja na kwenda angani.Ni vyema mafundi fridge wakapewa elimu na tekinologia namna ya kuifadhi hiyo gesi kwenye mitungi maalum wakati wa service BILA KUICHIA ANGANI.
5.Inadaiwa gesi hizo zinaharibu OZONE LAYER.
 
Ukweli ni kuwa used friji zilizojaa Hapa nchini Ulaya azitakiwi tena 1.zinakula sana Umeme 2.Zina Gesi Hatarishi zinazoharibu Ozone Layer....so sisi ni damping site..mbali na hizo friji pia kuna taka nyingi za kielectronic ambazo zinajaza nchi yetu bila faida bali hasara kwa mazingira yetu.
Sasa ni kwa nini Waziri asijikite kwenye zoezi la kuzuia haya majokofu used kuingia nchini mwetu?

Kuwashauri tu wananchi kutonunua hayo majokofu, huku yakiruhusiwa kuuzwa nchini, mbona inamfanya Waziri aonekane Ndumilakuwili, na mtu asiye jielewa!
 
Kwahio hili nalo ni kipaumbele cha matatizo yetu?!!!!

Weka video isijekua unalako jambo.

Lete tusikie wenyewe.
 
Hapa alipowekwa ndio naamini jamaa ni kilaza licha ya mbwembwe nyingi za kwenye media kipindi yupo Tamisemi na ndio maana aliondolewa...
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom