Waziri Jafo: Wananchi nunueni Majokofu mapya yale ya mitumba yanachafua hali ya hewa!

Ukweli ni fridge za mitumba/magari mabovu yanaharbu sana mazingira,Serikali izidi kufikia jicho maeneo hayo na ikibidi yasionekane kabisa town
 
Waziri wa mazingira mh Jaffo amewataka wananchi kuacha kutumia majokofu ya mitumba kwani yanachafua hali ya hewa na hivyo kuharibu mazingira.

Jaffo amesema ni vema wananchi wakanunua majokofu mapya kwa ajili ya usalama wa afya zao.

Source: Upendo tv
Kwahiyo kama yanaharibu na kuchafua mazingira yanakujajekujaje?yanapitajepitaje?
 
Kuna mzee aliwahi kuniambia mwanaume mweny3 wake au wapenzi kuanziq wanne ...huwa n dhaifu Sana kiuongozi !
Sijui Kama Ina ukweli hii nadharia!
Yuko sahihi mzee wako....ANAONEKANA ANA BUSARA SANA HUYO MZEE...KONGOLE KWAKO KUWA NA WAZEE KAMA HAO
 
Kinachosemwa ni kuwa mafundi wa majokofu wanapoyatengeneza aina ya gesi wanayoitoa kwenye kompresa ili waweke nyingine huharibu mazingira.
Kwa level yetu Tanzania na afrika kwa ujumla, tunaweza kujua na kutathmini athari ya mazingira yatokanayo na gasi!? Hii ni kutaka tu kuleta mtafaruku
 
Ukweli ni kuwa used friji zilizojaa Hapa nchini Ulaya azitakiwi tena 1.zinakula sana Umeme 2.Zina Gesi Hatarishi zinazoharibu Ozone Layer....so sisi ni damping site..mbali na hizo friji pia kuna taka nyingi za kielectronic ambazo zinajaza nchi yetu bila faida bali hasara kwa mazingira yetu.
Just asking for a friend.
Kwani hiyo ozone layer itaharibika kwenye anga ya Tanzania pekee?
 
Kwanini wasipige marufuku au waongeze kodi kwenye hizo friji used..ili zisiweze nunulika..kusema tu haisaidii mana ndio zinapatikana kwa bei rahisi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ni vyema wakajua kwanza hali za raia wao kabla ya kufika huku...hawa viongozi wangekuwa smart wangetumia hata 20yrs kuuondoa umasikini kwanza kwa watanzania hapo wangekuwa wametatua matatizo meengi sana automatically..
 
Ukiangalia matatizo meengi wanayowatesa hawa viongozi yametokana na jamii kuwa masikini....Competancy huwezi kuipata kama watu wako wengi ni masikini, hivi vitu vibovu vinakuja kwa kuwa huku ndio dampo wanakoishi waokota makopo ndio sisi sasa...umasikini huleta incompetency maana mtu mwenye njaa hawezi kufikiri wala kusoma vizuri...Vijana wetu wengi vyuo vikuu wanasoma wakitokea kwenye umasiki na wanasoma pia wakiwa na njaa..unaanzaje kuelewa hapo?
 
Waziri wa mazingira mh Jaffo amewataka wananchi kuacha kutumia majokofu ya mitumba kwani yanachafua hali ya hewa na hivyo kuharibu mazingira.

Jaffo amesema ni vema wananchi wakanunua majokofu mapya kwa ajili ya usalama wa afya zao.

Source: Upendo tv
Gas inayotumika sasa kwenye majokofu ni rafiki kwa ozone layer. Gas f12 ilibainika siku nyingi haifai na ulaya wakatunga sheria mwisho wa kutumia majokofu yanayotumia f12 ni mwaka 2025. Naamini serikali ililijua hilo, lakini majokofu yaliokuwa yanaingizwa nchini kama mitumba (mengine yakiwa ni mapya kabisa), ilikaa kimya. Serikali inawajibu wa kuwalipa fidia wananchi ili waondokane nayo. Lakini kwa vile ni serikali ya kutofata sheria (rejea maamuzi ya viroba na mifuko ya plastic), haitashangaza kuona inaagiza marufuku na kuingia majumba ya watu kuyakamata.
 
Zuia yasiingie nchini.
Simple.
Hivi Jafo ana elimu gani au alisoma chuo gani?
Ni zaidi ya miaka 20 tangu EU ipige marufuku matumizi ya gas ya f12, Tanzania ikawa dumping site ya majokofu hayo, wizara ya mazingira ilikuwepo ikivinjari. Leo ndio Jafo analiona.
 
Waziri wa mazingira mh Jaffo amewataka wananchi kuacha kutumia majokofu ya mitumba kwani yanachafua hali ya hewa na hivyo kuharibu mazingira.

Jaffo amesema ni vema wananchi wakanunua majokofu mapya kwa ajili ya usalama wa afya zao.

Source: Upendo tv

Kwani tozo za miamala wameshaziondoa? Au anadhani na sisi hatulipi kodi kama yeye na wenzake huko serikalini?
 
Back
Top Bottom