Waziri Jafo na wanaCCM tuulizane: Tarehe 24/11/2019 tuwaambie nini wananchi tuliowahamasisha wajiandikishe kupiga kura?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mwenyekiti na Rais wetu aliagiza bila kuigiza kuwa wananchi wahamasishwe kujiandikisha kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika tarehe 24/11/2019. Mwenyekiti akatahadharisha kwa watakaofanya vibaya kwenye zoezi la uandikishaji. Tahadhari ya Mwenyekiti ikawatoa viongozi kwenye viti vyao vya enzi.

Viongozi kuanzia ngazi ya taifa wa chama na Serikali waliingia 'mzigoni' kuwahamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura hapo tarehe 24/11/2019. Wananchi wakahamasika na wengine 'kuhamasishwa' na hatimaye kuandikishwa na hata 'kuandikwa' kwenye Orodha ya wapigakura. Ikatangazwa kwa mbwembwe idadi na asilimia za walioandikishwa na walioandikwa.

Waziri Suleiman Jafo wa TAMISEMI, Waziri muhusika wa zoezi zima la uchaguzi wa Serikali za Mitaa, alitoa hadi zawadi bila ahadi kwa 'washindi' wa uandikishaji. Kilichofuata ni rafu tafu za kiuchaguzi. Kukatokea uchafuzi wa wazi wa kuwaengua wapinzani wetu karibu wote katika uchaguzi huo. Tukabaki CCM tukipita bila kupingwa. Wapinzani wakatangaza kujitoa. Waziri anataka wawepo.

Namhurumia Waziri Jafo kwa mambo mawili. Kwanza, ndiye Waziri mhusika. Kwahiyo mambo yakiharibika, atakuwa wa kwanza kuwajibika. Pili, alifurahishwa na hamasa na uhamasishaji wa kuandikisha wananchi. Sasa itakuwaje waliohamasishwa kujiandikisha wasipige kura? Hakika hilo linamtesa sana waziri Jafo. Ndiyo maana anatamani hata kuwarudisha waliojitoa kibabe.

Binafsi nimeshiriki hamasa hasa kwenye mikoa minne. Nilikesha kwenye hamasa kuhakikisha kuwa watu wanajiandikisha. Sasa, tuulizane ninyi makada wenzangu wa CCM na Waziri Jafo, kutokana na wapinzani kutokuwepo na sisi kupita bila kupingwa nchi nzima, tutawaambiaje wananchi waliohamasika na kujiandikisha? Maana, hawatapiga kura Novemba 24. Ni aibu sana hii!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Songea, mkoani Ruvuma)

 
Tutawaambia tumenunua midege, stigker gorge, SGR na kuhamia Dodoma. Tutawakumbusha alipoomba urahisi hakuahidi vyuma kukaza wala kuheshimu nyongeza stahili za kila mfanyakazi wa serikali. Tutawaambia watembee kifua mbele sisi ni dona kantre.
 
Kama tulivyohamasishwa tukajitokeza kwa wingu kujiandikisha, vivyo hivyo tuhamasishe watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura
P
Sasa kumpigia kura nani wakati kisheria sasa hivi wagombea wote kasoro wa CCM wamejitoa?
Hivyo CCM imeshinda kwa kishindo 100%
Hakika hii ni historia, hongera sana Magufuli, hongera CCM kwa kukubalika huku.
Pasco we 24/11 kashushie tuu na JD yako taratibu!
 
Wanapoteza hela zetu kujifanya kufuata Demokrasia,
ccm wapo njiani kujitoa wanadai wameonewa


Wanapoteza hela zetu kujifanya kufuata Demokrasia,
ccm wapo njiani kujitoa wanadai wameonewa



Wanapoteza hela zetu kujifanya kufuata Demokrasia,
ccm wapo njiani kujitoa wanadai wameonewa
 
Back
Top Bottom