Waziri Jafo: Kuna watu wanadhani watakaoingia mbinguni ni wale wanaosali sana kumbe watenda kazi kama Rais Magufuli wataenda peponi!

“Njia ile ni nyemba mba iendayo uzimani, wauwaji na wazinzi hawapiti njia ile”.

Kutoka kwaya ya Assemblies of God
 
Nakubaliana kabisa na kauli hii ya mh Jaffo kwamba Rais Magufuli atakwenda peponi kutokana na kujitoa kwake kwa hali na mali katika kuwatumikia wananchi wanyonge.

Hata Yesu alisema si kila amuitaye Bwana....Bwana ataingia katika ufalme wa mbinguni bali wale wayatimizayo mapenzi ya Mungu.

Mh Jaffo jina la Yesu likubariki.

Amen!
Bwashee uko sawa kweli !!!?
Malaria inaua tembelea kituo cha afya kilicho karibu.
 
Amesema kweli kuwa kuingia mbinguni hakutegemei na kusali sana. Nijuavyo ni kwamba mtu atakaye ingia mbinguni ni yule atakaye tenda mapenzi ya Mungu.

Hilo la Rais kuingia mbinguni napingana nalo labda kama hiyo mbingu imejengwa kwa mabox na ccm
Dah
 
Nakubaliana kabisa na kauli hii ya mh Jaffo kwamba Rais Magufuli atakwenda peponi kutokana na kujitoa kwake kwa hali na mali katika kuwatumikia wananchi wanyonge.

Hata Yesu alisema si kila amuitaye Bwana....Bwana ataingia katika ufalme wa mbinguni bali wale wayatimizayo mapenzi ya Mungu.

Mh Jaffo jina la Yesu likubariki.

Amen!

Kuna waziri wa zamani wa Moi ya Kenya (Aloo Aringo) aliwahi kumwambia Moi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara: "mtukufu rais, hata ndege na miti ikikuona inaimba 'nyayo nyayo nyayo'".

Endeleeni tu kumuabudu mungu wenu Magufuli lakini matokeo yake mtayaona hivi karibuni.
 
Una uhakika mkuu au unaskiliza stori za vijiweni

Ulishawahi kumsikia Magufuli anakemea au kulaani kupigwa risasi Lissu au kupotea kina Azory? Kwa nini serikali yake ilikataa msaada wa uchunguzi kutoka nje? Kwa nini kamera ziling'olewa baada ya tukio la Lissu kupigwa risasi?
Hiyo laana itamhusu Magufuli na vizazi vyake hata cha tatu na cha nne asipotubu.
 
Hata waliopanga kumuua Tundu Lissu wataenda mbinguni wakati amri za Mungu zinakataza kuua? Mtoa mada unachekesha kweli.
Nakubaliana kabisa na kauli hii ya mh Jaffo kwamba Rais Magufuli atakwenda peponi kutokana na kujitoa kwake kwa hali na mali katika kuwatumikia wananchi wanyonge.

Hata Yesu alisema si kila amuitaye Bwana....Bwana ataingia katika ufalme wa mbinguni bali wale wayatimizayo mapenzi ya Mungu.

Mh Jaffo jina la Yesu likubariki.

Amen!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbinguni sio kwa lumumba au kwa mzungu.

Wauaji, waasherati, wazinzi, waongo, wanafiki, wezi nk hawataingia ufalme wa mbinguni!
Biblia imesema.

Sasa nyie jipeni moyo tu. Utafikaje mbinguni wakati mamilioni ya watu wanakunungunikia, wakisema wana njaa unasema wavivu, wakisema wanashida na uchumia vyuma vimekaza, unasema tuweke gilisi,

Sasa huko mbinguni ni babu au mjomba angu.
Na bado anasema ETI mshahara wake haumtoshi...
 
Back
Top Bottom