Waziri Jafo atoa wiki 2 kwa Uongozi wa Dodoma kuifanyia ukarabati Shule ya Msingi Nkuhungu na kuhakikisha inafikisha ufaulu wa asilimia 100

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo ameliagiza Jiji la Dodoma chini ya Mkurugenzi wake Joseph Mafuru kuifanyia ukarabati Shule ya Msingi Nkuhungu pamoja na kuhakikisha inafikisha ufaulu wa asilimia 100 kwenye matokeo ya mitihani ya darasa la nne.

Jafo ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati alipofanya ziara yake ya kukagua miundombinu ya shule hiyo pamoja na barabara ya Jamhuri na barabara ya Nkuhungu-Swai.

Kwenye barabara ya Jamhuri Waziri Jafo ameeleza kufurahishwa na ukamilikaji wa barabara hiyo ya kilomita moja iliyogharimu kiasi cha Sh Bilioni Moja huku akimuagiza Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Lusako Kilembe kuhakikisha barabara ya Nkuhungu Swai yenye ukubwa wa kilomita moja itayogharimu Sh Milioni 800 inakamilika ndani ya muda uliopangwa ambao ni Juni mwaka huu.

Akizungumza na viongozi wa Mkoa, Jiji, Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu, Waziri Jafo ameuagiza uongozi wa Jiji la Dodoma kuhakikisha madarasa yote ambayo paa lake limeharibika kufanyia matengenezo huku pia akiagiza darasa la awali nalo kufanyiwa maboresho na kuwa la kisasa.

" Ninafurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Jiji la Dodoma lakini Mkurugenzi wa Jiji tenga angalau kiasi cha Sh Milioni 25 au 30 kwa ajili ya kufanyia matengenezo shule hii ambayo inabeba wanafunzi wengi sana, ninatoa wiki mbili hadi kazi iwe imekamilika hapa na mimi Februari 20 nitakuja tena kuikagua.

Nimeamua kuwa mlezi wa Shule hii hivyo ninataka iwe na muonekano wa kuvutia na kiwango chake cha ufaulu kiwe juu, matokeo ya darasa la nne ufaulu wake ni asilimia 91 ninataka iwe mwisho sasa kiwango kifikie asilimia 100 hivyo Jiji na uongozi wa shule muangalie namna ya kuboresha ufaulu," Amesema Waziri Jafo.

Akitoa maelekezo yake kwenye miundombinu ya barabara, Waziri Jafo ameagiza TARURA kuhakikisha wanapanda miti ya matunda kwenye barabara zote nchini lengo likiwa ni kutunza mazingira lakini pia kupendezesha mandhari za barabara nchini.

" Nimeridhishwa na barabara ya Jamhuri kazi yake ni nzuri, lakini hii ya Nkuhungu Swai bado kasi yake siyo kubwa niwataka TARURA kuhakikisha mkandarasi anakamilisha kazi yake ndani ya muda uliopangwa bila kisingizio chochote.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde ameahidi kutoa kiasi cha Sh Milioni 70 za mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kununua madawati lengo likiwa ni kuondoa changamoto ya madawati kwenye shule za jiji la Dodoma na kuunga mkono juhudi za Rais Dk John Magufuli za kutoa elimu bila malipo.
 
Hawa watu ni vichaa! Vichaa kabisa. Wanashindana, huyu Gwajima, hapa Jokate, kule Mavunde, na anamalizia Jafo...
 
Sasa tumehamia kwenye shule za msingi baada ya Rais kutoa maagizo ya ujenzi na ukarabati wa ile shule ya msingi kule Ubungo. Rais akigeukia upande mwingine,viongozi wetu watageukia huko. Kwa kweli Rais hana watendaji wa kumsaidia bali wengi ni wasanii tu
 
Back
Top Bottom