Waziri Jafo atoa siku 68 kwa Halmashauri 4 nchini kurudisha fedha za mradi wa Equip

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
WAZIRI wa nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ametoa siku 68 kwa halmashauri 4 za Kigoma Ujiji, Butiama, Liwale na Bahi kurejesha fedha za mradi wa elimu (Equip)zilizotumika kinyume na utaratibu.

Aidha ametoa wiki moja kwa Mweka Hazina wa Manispaa ya Iringa ambaye awali alikuwa akifanya kazi Halamshauri ya Bahi, Saad Ishabairo kuchunguzwa akidai utendaji wake una mashaka

Halmashauri hizo ni kati ya halmashauri 8 zilizotumia fedha kinyume kiasi cha milioni 912.7 ambapo halmashauri 4 zilitekeleza agizo lake na kurejesha fedha.

"Halmashauri hizi wamenihuzunisha sana kwa kutotii maelekezo, naziagiza mpaka machi 28 mwaka huu wawe wamerejesha ili fedha hizo zitekeleze miradi iliyokusudiwa, "amesema Jafo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo pesa za wafadhiri zitawatokea puani halmashauri zetu.
Maana za serikali kuu zimekuwa kaa la moto kama sio ndoano. Wadau wanazipiga hizi Jaffo kastukia mchezo. Hata rejesheni fedha za majengo, warsha za walimu na ruzuku za waratibu.
Walishaweka kwapani wao wa halmashauri
 
Kwenye hiyo listi halmashauri ya CHAMWINO haipo dah? Maana DEO alietoka hapa CHAMWINO ndiye alienda kuendeleza uhuni huo Bahi na kuna mazalia kayaacha hapa.
 
Hizo pesa za wafadhiri zitawatokea puani halmashauri zetu.
Maana za serikali kuu zimekuwa kaa la moto kama sio ndoano. Wadau wanazipiga hizi Jaffo kastukia mchezo. Hata rejesheni fedha za majengo, warsha za walimu na ruzuku za waratibu.
Walishaweka kwapani wao wa halmashauri
Yakirekebishwa yafutayo hili la misuse of Donor fund itapungua;

-Kupunguza ziara za viongozi zisizo na tija ambazo Council ndio wanagharamia kwenye viburudisho+posho (indirect)

- utegemezi wa DC kwa mafungu ya DED upungue (MaDc wajikite kwenye kutumia ruzuku yao, lkn pia serikali iwawezeshe ruzuku ya kutosha ht km siyo kwa 100%.

-Serikali ipunguze maagizo yasiyo na tija, yasiyoweza kutekelezeka kwa bajeti ya mwaka husika!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo pesa za wafadhiri zitawatokea puani halmashauri zetu.
Maana za serikali kuu zimekuwa kaa la moto kama sio ndoano. Wadau wanazipiga hizi Jaffo kastukia mchezo. Hata rejesheni fedha za majengo, warsha za walimu na ruzuku za waratibu.
Walishaweka kwapani wao wa halmashauri
Kama hizo za waratibu zinatafunwa waziwazi na wanaambiwa atakae lalamika atatolewa uratibu hipo halmashauri ya CHAMWINO hiyo alafu uwezi amini jamani watu sio waoga ofisi kuu ya magu IPO jirani tu ila kuna watu naona matundu yao yanatafuta cha kupitisha soon!
 
Hahaha
 
Yakirekebishwa yafutayo hili la misuse of Donor fund itapungua;

-Kupunguza ziara za viongozi zisizo na tija ambazo Council ndio wanagharamia kwenye viburudisho+posho (indirect)

- utegemezi wa DC kwa mafungu ya DED upungue (MaDc wajikite kwenye kutumia ruzuku yao, lkn pia serikali iwawezeshe ruzuku ya kutosha ht km siyo kwa 100%.

-Serikali ipunguze maagizo yasiyo na tija, yasiyoweza kutekelezeka kwa bajeti ya mwaka husika!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Donors wamekata funds zao. Mjitegemee
 
Back
Top Bottom