Waziri Jafo atangaza wiki moja ya "nyungu" season 3

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
5,038
2,000
2679302_IMG_20210130_130224.jpg

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ametangaza rasmi kuanza kwa kampeni ya nyungu season 3. Amesema hayo akiwa mkoani Tabora katika ziara ya kikazi Rais mkoani humo.

Waziri jafo alinkukuliwa akisema “Rais Magufuli juzi ulisema Watanzania tuko salama, angalia Umati huu wote tuko salama, hapa Corona haina nafasi, tutaendelea kumuomba Mungu na umesema Watu wajifukize sana, Jumatatu tunaanza Kampeni nyingine ya Wiki moja Season 3 , nyungu kama kawaida“

"Rais [Magufuli] naomba nikwambie, Jumatatu tunaanza kampeni nyingine ya one week season three, nyungu kama kawaida. Tunajifukiza, tunakula matunda, tunamuomba Mungu. Tunaanza tarehe 1 mpaka tarehe 7, hatupoi, kazi inaendelea."-
 

WAIKORU

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
1,385
2,000
Da!!!, mambo mengine kwa kweli unashindwa kujua hawa jamaa wanatuonaje....

Anasema "hapa korona haina nafasi"....akimaanisha hakuna korona

Hapohapo anatangaza wiki ya kujifukiza....wanasiasa kwa kweli wanacheza na akili za wadanganyika vizuri sana
 

sala na kazi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,910
2,000
Kiukweli nimeyapenda sana maneno ya Mh Waziri Jafo kule Tabora akiwahamasisha watu kupiga nyungu season 3 hayo ndio maneno ya kishujaa kabisa.

Rais Magufuli juzi ulisema Watanzania tuko salama, angalia Umati huu wote tuko salama, hapa Corona haina nafasi, tutaendelea kumuomba Mungu na umesema Watu wajifukize sana, Jumatatu tunaanza Kampeni nyingine ya Wiki moja Season Three, nyungu kama kawaida

Hapa Corona haina nafasi, tunajifukiza, tunakula matunda tunamuomba Mungu, Season Three, nyungu kama kawaida, tunaanza February 01 hadi February 07, 2021 hatupoi kazi inaendelea, uchumi wetu lazima usimame-Jafo

Nawatakia Kila la kheri

NAWASILISHA
 

Shift

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
1,074
2,000
“Rais Magufuli juzi ulisema Watanzania tuko salama, angalia Umati huu wote tuko salama, hapa Corona haina nafasi, tutaendelea kumuomba Mungu na umesema Watu wajifukize sana, Jumatatu tunaanza Kampeni nyingine ya Wiki moja Season Three, nyungu kama kawaida

“Hapa Corona haina nafasi, tunajifukiza, tunakula matunda tunamuomba Mungu, Season Three, nyungu kama kawaida, tunaanza February 01 hadi February 07, 2021 hatupoi kazi inaendelea, uchumi wetu lazima usimame

Nawatakia Kila la kheri

NAWASILISHA
Kwa Mwoga huenda Kicheko, kwa Shujaa huenda kilio
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom